Ni kweli Malaria haikubaliki au tunatangaza biashara?

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Ni kweli kwamba ubinadamu umetiwa hatarini kwa kuzingirwa na Malaria. Katika maeneo yote ya kitropiki, vimelea vya ugonjwa wa Malaria vinavyohatarisha afya ya mwanadamu na kusababisha vifo vimeenea, ambapo takriban watu milioni moja hufa kila mwaka duniani.

Wataalam wanasema kwamba Malaria huanza na homa yenye baridi kali sana na aghlabu humalizikia kwa kuviathiri vibaya viungo vya mwili na hata kifo. Nusu ya wanaokufa kutokana na ugonjwa huu ni watoto wadogo.

Kupambana na na kufanikiwa kuuangamiza ugonjwa wa Malaria, kunatokana pia kuyaangamiza mazalio ya mbu. Vita dhidi ya ugonjwa huu, kwa hivyo, ni vita dhidi ya mdudu: mbu aitwaye Anopheles. Kupambana na mdudu huyu ni jambo linalohitaji rasilimali na teknolojia, ambayo nayo pia inakosekana kwenye mataifa masikini kama Tanzania.


Mara tu mdudu huyu akidhibitiwa kikamilifu, dunia inaweza kujitangazia ushindi kwenye vita hii ngumu ya kupambana na Malaria. Asiyeumwa na mbu, hawezi kupata Malaria. Kwa hivyo, hapa ndipo linapokuja suala la umuhimu wa kutumia vyandarua na hatua nyingine za kuzuia kuumwa.


Chandarua kinaweza kukaa hata mwaka mzima bila ya kutoboka, lakini mbu mmoja hawezi kuishi ndani ya kipindi chote hicho. Anapokuwa ametaga mayai yake kwenye madimbwi au mahala popote, mayai hayo yanapasa kuangamizwa kwa dawa.


Licha ya dawa zinazotumika kwa kazi hiyo, kama DDT, kuthibitika kuwa na athari mbaya kwa mazingira, Shirika la Afya Duniani, WHO, limeidhinisha matumizi ya DDT likisema kwamba kama ikitumika vyema, basi haina madhara kwa binadamu na wanyama.

Juu ya yote, kwa mataifa masikini, bado hadithi inaendelea kubakia kuwa ile ile ya vipi wanaweza kuigharamikia teknolojia ya kinga na tiba ya Malaria; na vipi wanaweza kuwakinga watoto wao wasiumwe na mbu wa Anopheles, na hatimaye kuugua malaria, ambayo husababisha vifo vya watoto hao.

Majuzi nilipita mtaa mmoja ambapo nilibahatika kusikia maongezi ya vijana fulani waliokuwa kijiweni yaliyojikita katika vita dhidi ya Malaria, hasa kwa kuwa mmoja wao alikuwa akiugua Malaria. Walikuwa wakimshutumu mwenzao kwa kutozingatia kulala kwenye chandarua chenye ngao, jambo ambalo nakubaliana nalo ingawa nina shaka na kampeni inayoendeshwa kama nitakavyoeleza baadaye.

Nadhani walisisitiza kutumia chandarua chenye ngao kwa kuwa asilimia kubwa kabisa ya vita dhidi ya Malaria nchini imeelekezwa kwenye matumizi ya vyandarua vyenye ngao. Lakini swali la kujiuliza hapa, ina maana kila mmoja akitumia chandarua chenye dawa ya ngao, Malaria itakuwa imeshadhibitiwa?

Sitaki kuwajibia watu wengine lakini kwa mtazamo wangu ni kwamba si kweli. Sasa kwa nini kila mahali yametapakaa matangazo ya vyandarua vyenye dawa ya ngao, tena yakiwa yamepewa baraka na serikali kupitia wizara ya afya? Inasemwa kuwa wanatilia msisitizo wa matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya ngao ili kupambana na malaria kwa kuwa asilimia kubwa watu hupata malaria wakiwa wamelala.


Kitaaluma mimi ni tabibu, ingawa nimeacha kazi ya utabibu miaka mingi iliyopita lakini sikumbuki kusoma popote eti mtu huambukizwa malaria anapokuwa amelala. Sidhani kama kuna ukweli katika hili au kama kuna tafiti zozote zilizofanywa kuhusiana na hili.

Nijuacho ni kwamba mtu anaweza kuumwa na mbu aenezaye Malaria akiwa amekaa chumbani, pembeni mwa kitanda, sebuleni, barazani na mahali popote pale ambapo mbu waenezao malaria wapo. Hii ni kusema kuwa mahala popote mtu anaweza kupata malaria, si wakati akiwa amelala tu! Huu ni ukweli mtupu ambao hata hauhitaji utafiti.

Sasa kwa nini vita vyetu katika kudhibiti Malaria tumevielekeza katika vyandarua vyenye dawa ya ngao utadhani kuwa hilo ndilo suluhisho pekee? Kwa nini tusingeleekeza vita dhidi ya Malaria kwenye kuwaangamiza wadudu hawa kwenye maeneo wanayozaliana huku watu wakisisitizwa kutumia vyandarua vyenye dawa kwa uhakika zaidi?


Kwa nini matumizi ya vyandarua vyenye dawa ndio imefanywa kuwa sera na kuchukuliwa kama ndio suluhisho la kipekee la kutokomeza Malaria? Imefikia hatua ambapo nguvu kubwa na pesa nyingi zimekuwa zikielekezwa kwenye matumizi ya vyandurua vyenye dawa kwa asilimia kubwa kabisa!

Hata zile dawa za kuchoma tulizozowea kutumia siku hizi hazitumiki tena, kisa watu wanatumia vyandarua! Dawa za kupuliza nazo hazitumiki kuwaua mbu, tumeridhika kuwapo ndani ya vyandarua, tunasahau kuwa tukitoka nje ya chandarua tutawakuta mbu wanatusubiri.

Ukibahatika kuona tangazo lolote kwenye televisheni linalohamasisha matumizi ya dawa za kuwaangamiza mbu, utasikia ikisisitizwa kuwa mende, kunguni, na wadudu wote wanaoruka na kutambaa ndani wanaangamizwa. Si tangazo la vita dhidi ya Malaria bali ni tangazo la kibiashara, ambapo kampuni inatangaza bidhaa yake.

Vifo vingi vinavyotokana na Malaria ni sababu ya kushindwa kumdhibiti adui mbu (kwa kuharibu mazalia) kwa kiwango kinachotakiwa. Kwa nini vita hivi visielekezwe kwenye kumwangamiza mbu na makazi yake kuliko kujikinga na kutoumwa na mbu tunapokuwa tumelala? Kwani sebuleni, barazani n.k hakuna mbu wanaotusubiri? Au tuweke vyandarua kila mahali!

Malaria ina tiba, sasa iweje iangamize idadi kubwa ya watu pengine kuliko hata Ukimwi usio na tiba?

Nadhani kampeni hii dhidi ya Malaria kwa kutangaza vyandarua vyenye ngao ni mradi tu usio na mikakati sahihi ya kukabiliana na idadi kubwa ya wagonjwa wa Malaria na hata vifo.


 
Ndugu yangu Hongera kwa kuliona hili. Kweli hizi ni biashara ya wachache. Tuchukue mfano kulikuwa na dawa na kutibu Malaria (Chloroquine) ilikuwa ni nzuri sana na inaweza kutibu na kuzuia malaria asilimia 100.

Lakini kutokana na watu kuingiza biashara wakaipiga vita ile dawa kuwa haina uwezo wa kutibu Malaria tena, sasa hizi zilizopo sasa ndio hazifai kabisa kwa hazina uwezo 100% na pia zina side effect.

Miaka ya 1980's DSm kulikuwa na mradi wa kuondoa Malaria msaada toka nchi ya JAPAN, kwa ukweli ulikuwa ni mradi mzuri na zile dawa zilikuwa zinaweza kuthibiti Malaria 100% pamoja na wadudu wote ndani ya nyumba.

WAfanyakazi wa JIJI walikuwa wanapita mitaani na kunyunyizia dawa katika kaya zote bure, ile dawa ilikuwa iniafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja.

Hatukuwa na haja ya kuweka Chandarua dawailikuwa ni TOSHA kabisa

Sasa Serikali heri ingelifanyua utaratibu wa kuwasiliana na JAPAN ipatikane dawa ile hata kwa wananchi kulipia lakini inasaidia kiasi kikubwa sana kuliko Vyandarua.

Wito wangu kwa Serikali watafute njia mbadala na siyo kusisitiza matumizi ya chandarua lakini bado watu wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ndugu yangu Hongera kwa kuliona hili. Kweli hizi ni biashara ya wachache. Tuchukue mfano kulikuwa na dawa na kutibu Malaria (Chloroquine) ilikuwa ni nzuri sana na inaweza kutibu na kuzuia malaria asilimia 100.

Lakini kutokana na watu kuingiza biashara wakaipiga vita ile dawa kuwa haina uwezo wa kutibu Malaria tena, sasa hizi zilizopo sasa ndio hazifai kabisa kwa hazina uwezo 100% na pia zina side effect.

Miaka ya 1980's DSm kulikuwa na mradi wa kuondoa Malaria msaada toka nchi ya JAPAN, kwa ukweli ulikuwa ni mradi mzuri na zile dawa zilikuwa zinaweza kuthibiti Malaria 100% pamoja na wadudu wote ndani ya nyumba.

WAfanyakazi wa JIJI walikuwa wanapita mitaani na kunyunyizia dawa katika kaya zote bure, ile dawa ilikuwa iniafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja.

Hatukuwa na haja ya kuweka Chandarua dawailikuwa ni TOSHA kabisa

Sasa Serikali heri ingelifanyua utaratibu wa kuwasiliana na JAPAN ipatikane dawa ile hata kwa wananchi kulipia lakini inasaidia kiasi kikubwa sana kuliko Vyandarua.

Wito wangu kwa Serikali watafute njia mbadala na siyo kusisitiza matumizi ya chandarua lakini bado watu wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Hapo kwenye red ni kweli mi nakumbuka mara ya mwisho kuumwa malaria ilikuwa mwaka 2000 nanilitumia hizo dawa zilinisaidia sana,ila wanasema bado zipo hizo dawa,ila sijui zinapatikana wapi/hii nchi usanii umechukuwa sehemu kubwa sana kuliko hali halisi,na watu wengine wanao changia kufanya usanii (kutumaliza kiafya)kama sio kutuua kabisa ni TBS na kwasasa TFDA nao naona wanakuja kwa kasi.
 
Hapo kwenye red ni kweli mi nakumbuka mara ya mwisho kuumwa malaria ilikuwa mwaka 2000 nanilitumia hizo dawa zilinisaidia sana,ila wanasema bado zipo hizo dawa,ila sijui zinapatikana wapi/hii nchi usanii umechukuwa sehemu kubwa sana kuliko hali halisi,na watu wengine wanao changia kufanya usanii (kutumaliza kiafya)kama sio kutuua kabisa ni TBS na kwasasa TFDA nao naona wanakuja kwa kasi.

Hata mimi jana nilikuwa naongea na rafiki yangu kuhusu suala la Malaria na Dawa zake.

Aliniambia kuwa Chloroquine vidonge na sindano ipo Tanzania isipokuwa inapatikana kwa kificho sana. Ni heri Serikali iruhusu tu kuokoa maisha ya Watanzania.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mimi naona watu wanafanya business tuu. Msimamo wangu always umekuwa ni kwamba kama kweli tungekuwa na nia ya kuitokomeza malaria, sasa hivi tungekuwa tumeshafanya hivyo. Trust me, kuna baadhi ya wanasiasa na baadhi ya wataalam wa sekta ya afya kula yao inategemea kuendelea kuwepo malaria!! Huwezi KUITOKOMEZA malaria kwa kushadadia matumizi ya chandarua tuu bila kutia msisitizo kwenye kuangamiza mbu wanaoeneza malaria, na wahusika wanalijua hilo, ila sasa hawataki kufa njaa
 
Malaria ni ugonjwa unaoongoza kwa kuua idadi kubwa ya watu tanzania lakini angalia nguvu kubwa iliyowekwa kwa ajili ya ukimwi badala yake wamekuwa wanafanya biashara kwa manufaa yao binafsi huwezi kupambana na malaria kwa kuchapisha fulana au kutengeneza vyandarua njia pekee ya kupambana na malaria ni kuelimisha watu, kuua mazalia ya mbu, kuhakikisha watu wanapoumwa wanapata tiba sahihi pamoja na dawa zinazostahili sasa hivitumekuwa tunafanyiwa majaribio kwa kuletewa dawa ambazo hazidumu hata miaka mitatu zinabadilishwa mwisho ni kufanya tafiti na kutumia dawa asili ambazo baadhi zimekuwa zikitibu malaria vizuri bila kuwa na side effect
 
Malaria ni ugonjwa unaoongoza kwa kuua idadi kubwa ya watu tanzania lakini angalia nguvu kubwa iliyowekwa kwa ajili ya ukimwi badala ya ke wamekuwa wanafanya biashara kwa manufaa yao binafsi huwezi kupambana na malaria kwa kuchapisha fulana au kutengeneza vyandarua njia pekee ya kupambana na malaria ni kuelimisha watu,kuua mazalia ya mbu,kuhakikisha watu wanapoumwa wanapata tiba sahihi pamoja na dawa zinazostahili sasa hivitumekuwa tunafanyiwa majaribio kwa kuletewa dawa ambazo hazidumu hata miaka mitatu zinabadilishwa mwisho ni kufanya tafiti na kutumia dawa asili ambazo baadhi zimekuwa zikitibu malaria vizuri bila kuwa na side effect
Kuna wasanii wachache wanakuja na kampeni za kizushi wanajifanya wanatokomeza malaria hakuna kitu,yaani ni usanii uliopitiliza na serikali yetu inajua,lakini kwasababu wachache wananufaika wanakaa kimya,lakini raia wasio na hatia wanaangamia kwa kiasai kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom