Ni kweli maelezo ya hii picha yanaendana na picha yenyewe?

Kubingwa

JF-Expert Member
Apr 23, 2010
505
69

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ikulu Dar es Salaam jana kumuaga rasmi, baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibubni - Majira 20th January,2012.

<TBODY>
</TBODY>
 
majira siku hizi ndivyo walivyo computer zao zimeingia virus

Mimi naamini virusi haviko katika computers bali katika VICHWA VYA WAHARIRI!!!! Kwani wao hawa-hariri kazi za waandishi wao kabla ya uchapishaji???

Hii ni muendelezo wa UKANJANJA WETU WA Tanzania na kufanya kazi kwa mazoea!!!! KAMASI KABISA WAHARIRI WAZEMBE!!!!
 
makosa hata ktk kuandika yaliyojiri ktk picha waliobandika?
mhariri kazi yake nn? si kasomea au kalazimishwa kuhariri?
hata mtoto wa darasa la kwanza asingefanya upuuzi huu
atajua kabisa hapa mtu anapewa pole.
 
Sijaona lolote la ajabu zaidi ya kuelewa ni makosa ya kibinadamu.
Mkuu, Labda huelewi process inayotumika mpaka gazeti linaingia mtaani...ndio maana unaongea kirahisi rahisi kuwa ni makosa ya kibinadamu! kazi ya wahariri ni nini? kazi ya msoma gazeti kabla ya kuchapishwa ni nn?
...mkuu we ni mmoja ya watu wa ajabu sana! watu kama nyie hamtakiwi kupewa mamlaka yeyote chini ya hili jua!
unaupotosha umma wazi wazi hivi?? huu ni uzembe full stop!!!
 
Legacy ya mkweree kutoa vyeo na kazi kwa uswahiba matokeo yake ndio hayo mpaka magazetini!!
 
Hii sawa na wa operesheni ya mguu kufanyiwa ya kichwa na wa kichwa kufanyiwa ya mguu.........proffessional misconduct
 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ikulu Dar es Salaam jana kumuaga rasmi, baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibubni - Majira 20th January,2012.

<tbody>
</tbody>

Balozi wetu nchini kenya nae bwana!
 
Back
Top Bottom