Ni Kweli Machunde kajitoa Kamati ya Madini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Kweli Machunde kajitoa Kamati ya Madini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Nov 23, 2007.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna Taarifa Kwamba Machunde Ambaye Ni Mshirika Wa Karamagi Kajitoa Kamati Ya Madini, Kama Kuna Mwenye Taarifa Rasmi Atupe... Naendelea Kufuatilia
   
 2. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli ana uhusiano wa karibu atakuwa amefanya jambo la maana sana. Hatuwezi kuangalia maslahi ya wachache.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Kama kweli, basi bado Maria Kejo toka sheria na Salome Makange toka madini ambao nao walihusika kwa namna moja au nyingine kusaini mikataba inayopigiwa kelele.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 23, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  yote ni mazingaombwe, viinimacho, na wepesi wa vidole!
   
 5. F

  FundiwaKuketi Member

  #5
  Nov 23, 2007
  Joined: Nov 12, 2007
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa Kwa maoni yangu,
  Ni vyema wakawepo ili waweze kuwaelezea wajumbe wengine kwenye kamati ni kwa nini baadhi ya hivyo vipengele viliwekwa na kwamba wameona manufaa gani au upungufu gani kwenye hiyo mikataba.
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Inaelekea habari hizi ni za kweli.... Kuna mtu nimeongea naye anasema, "Subiri kesho ndio itathibitishwa".... Mwingine akasema... "lazima ajiuzulu maana mwenzake naye ana 'bifu' na bosi wetu, kwa hiyo kwa sasa chamoto watakiona."
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kaka umejaaliwa kwa VIJEMBE!!!! Yaani wepesi wa vidole kuwasilisha kabla havijaiva, ama hatari ya 'kulishwa kasa'kwa taarifa ambazo si sahihi?

  taarifa ni kwamba habari hizi, zimo katika moja ya magazeti ya kila siku toleo la kesho Jumamosi
   
 8. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Halisi

  Si wewe wepesi wa vidole ni hao Chama Cha Mafisadi, wakali wa mazingaombwe kama yale ya Richmond ya kutuletea mitambo ya ndege mbovu na kuita majenereta. Ni kweli, mimi nimeipata jikoni. Kwa kweli watajiju mwaka huu. Fisadi Machunde kakimbia mabovu, baba yake kwa ufisadi Karamagi anasubiri nini pale? Mafisadi wamejiweka wenyewe kwenye lenzi ya umma. Watakoma!

  Asha
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Nov 24, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Hivi hili neno "maslahi ya Taifa" lina maana tena?
   
 11. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2007
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anayo mifupa kabatini huyu, anaogopa itatolewa hadharani; sasa anabaki kubwabwaja bila mpango kama mbwia unga.

  yaani haeleweki kabisa. Anajiuzuru kwa sababu ya kusemwa na watu wa CHADEMA? Sasa huo uzalendo na kuipenda nchi upo wapi hapo?

  Hili neno 'uzalendo' linapoteza maana sasa.
   
 12. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  mzimu wa watu kujitoa unatoka wapi?hawa watu ni vigeugeu manaake kabla ya kuteuliwa nijuavyo mimi ,huwa wanaitwa pale pango la wanyang'anyi na kuelezwa khali halisi,kama yeye alijua kulikuwa na mgongano wa maslahi kwanini alikubali?
  hawa ndio kina Idrisa Rashid,PhD..Huyu jamaa anadharau bodi ya wakurugenzi kisa yeye swahiba wa Muungwana..nashangaa watu kumtetea ni msomi na anataka kutatua tatizo la TANESCO,Kwa kupandisha umeme kwa 40%??
   
 13. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2007
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  "Akizungumza kwa masikitiko, Bw. Machunde alielezea kusikitishwa kwake na mwelekeo wa mtizamo wa baadhi ya Watanzania kushutumiana na kutoaminiana na kujenga mazingira ya wao kujionesha kwenye jamii kwamba wana uchungu na nchi hii, ikiwa ni pamoja na raslimali zake, kuliko wengine.

  "Ni imani yangu, kwamba wote tunaipenda nchi yetu kwa kiwango kinacholingana...nimeumizwa na kufadhaishwa sana na dhana inayojengwa na kuenezwa na viongozi wa CHADEMA, kwamba katika ushiriki wangu kama mjumbe wa Kamati hii, nisingeweka maslahi ya nchi yetu mbele.

  "Hakuna tusi kubwa kama kudhaniwa kwamba unaweza kuisaliti nchi yako na kuitambua heshima na imani uliyopewa na Rais," alisema na kuwafananisha CHADEMA na genge la wababaishaji."


  Wewe Machunde pamoja na kisomo chako chote hicho unajifanya hujui dhana ya "conflict of interest?" watu wanaonyesha hawana imani nawe si kwa uzushi tu, bali kwa uhalisia ambao hata wewe unaufahamu, na ndiyo maana umejiondoa mwenyewe, sasa unashangaa nini tena?

  Kama unafiki hatuwezi kuuacha, walau tuupunguze basi inapokuja mizozo ya namna hii! Unaipenda nchi sawa na wengine? Una hakika na hicho kipimo chako, au ndo siasa zinakuingilia kimwili taratibu na wewe?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Nov 24, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  kuna watu wengine wana kiburi kweli, yaani kwa vile utaumizwa tuogope kuwaambia ukweli?
   
 15. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2007
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu Mwanakijiji,

  Hicho alichoonyesha naona si kiburi, ni UJINGA, kwa kuwa anadhani public haifahamu ilichokuwa inasema, wakati si kweli. Angekataa kujitoa ndo angekuwa na kiburi.

  Asingeweza kujiondoa kwa watu kusema sema tu, mambo ya kuzua. Halafu anasema ooh Chadema wamesema ! aah jamani!
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huyu ni mmwajiriwa wa Karamagi,na kwa taarifa ni kuwa huyu pia ni mwajiriwa wa kule wakala wa makontena kule bandarini.

  Rais alitudanganya kuwa huyu ni kutoka DSE kwani huyu ni broker tuu na sio mwajiriwa wa DSE lazima kuiangalia dhamira ya rais hapa.

  Nitawawekea sehemu ya ushahidi hapa ,naambiwa kuwa jana CHADEMA waliandika barua rasimi kwenda BRELLA kuulizia wamiliki wa kampuni la Vertex financial services, na Vertex securities ltd ambamo ndimo Machunde kaajiriwa na pia Ni kamapuni la Karamagi.
   
 17. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  --------------------------------------------------------------------------------

  Published: May 2000

  ICTSI in Dar es Salaam deal
  As briefly mentioned in last month's WorldCargo News, a group consisting of International Container Terminal Services Inc (ICTSI), ICTSI International Holdings Corp (IIHC), and Vertex Financial Services has won the concession to manage and operate the Tanzania Harbours Authority's Dar es Salaam Port Container Terminal in the United Republic of Tanzania...
  One requirement to
  be performed by the winning bidder is the formation and registration of the bidder's local operating company, which will be the official lessee. The group has registered a Tanzanian based operating company, Tanzania International Container Terminal Services Ltd (TICT). TICT will initially be 75 per cent owned by the ICTSI group and 25 per cent owned by Vertex, a Tanzanian company. The company will take over operations three months after the signing of the lease agreement, scheduled for May 5.....
   
 18. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Members Profile >> MP CV
  --------------------------------------------------------------------------------

  Karamagi , Nazir.
  EDUCATION
  School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
  University of Strathclyde MSc. (Finance) 1996 1996 MASTERS DEGREE
  University of Edinburg MBA. (Business Administration) 1985 1986 MASTERS DEGREE
  St. PetersBurg University of Mining MSc. (Engineering) 1975 1980 MASTERS DEGREE
  Kibaha Secondary School A-Level Education 1972 1973 HIGH SCHOOL
  Nyakato Secondary School O-Level Education 1968 1971 SECONDARY
  Rubale Middle School Primary Education 1965 1967 PRIMARY
  Rubale Primary School Primary Education 1961 1964 PRIMARY

  --------------------------------------------------------------------------------
  CERTIFICATIONS
  Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
  No items on list

  --------------------------------------------------------------------------------
  EMPLOYMENT HISTORY
  Company Name Position From Date To Date
  VERTEX Int. Securities Ltd Managing Director 1999 1999
  VERTEX Fin. Services Ltd Managing Director 1998 1998
  Tanzania Portland Cement Co. Ltd Corporate Manager 1995 1998
  Tanzani
  a Portland Cement Co. Ltd Business Manager 1989 1995
  Tanzania Portland Cement Co. Ltd R&D Manager 1987 1988
  Tanzania Portland Cement Co. Ltd Electronic Engineer 1980 1985
  Ministry of Energy and Minerals Minister 10/17/2006
  Ministry of Industry, Trade & Marketing Minister 1/1/2006 10/16/2006

  --------------------------------------------------------------------------------
  POLITICAL EXPERIENCE
  Ministry/Political Party/Location Position From To
  Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Parliament of Tanzania 2003 Todate
  Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of National Executive Council 2002 Todate
  Chama Cha Mapinduzi - CCM Commissar - TPCL 1991 1992
  TANU Chairman - TYL(Kibaha Secondary Branch) 1972 1
   
 19. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  link ya Karamagi na Machunde hii hapa,  Business & finance More in this Category!
  Sale of Barclays bond starts Wednesday
  Abduel Kenge
  Daily News; Monday,October 09, 2006 @00:03

  Barclays Bank Tanzania will start selling its bond to the public starting Wednesday.

  The offer will last for two weeks and will be known as the Barclays Bank Bond Primary Offer. The bond will last for five years.

  Vertex International Securities are the sponsoring broker of the medium term bond.
  Vertex’s Executive Director, Mr Peter Machunde, said the bond totalling about 10bn/- under a floated rate mechanism would be p
  aid twice in a year.

  ‘‘The coupon rate is pegged on Treasury bill of the six-month during the payable period,’’ Mr Machunde said. He said the bond redemption year is 2011.

  Mr Machunde said the medium term bond was good news to investors because they can compare its maturity with that of other fixed-income securities.

  ‘‘All other factors being equal, the coupon rate on MTN will be higher than those achieved on short-term notes,’’ Mr Machunde said.

  Currently, he said, interest rates are based on floating rate to give ‘‘either side flexibility unlike in the previous ones whereby the investor had to choose between fixed and floating rates.’’

  ‘‘Bonds attract more serious players like institutions and not individuals, but the first two Barclays bonds were oversubscribed at between ten and 20 per cent,’’ Machunde said.
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hana hili wala lile, kaona atazidi kuwa katika spot light na yeye mambo yake anayataka uyafanya chini kwa chini.

  aibu kuwa mtu hata ukichaguliwa nafasi nzuri huwezi kulitumikia taifa kutokana na madudu yako ya nyuma
   
Loading...