Ni kweli kwamba TRA hawajui au uzembe kutokusanya kodi za pango? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli kwamba TRA hawajui au uzembe kutokusanya kodi za pango?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mpendanchi-2, May 13, 2009.

 1. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huku Nchi ikiwa na matatizo lukuki ya kukosa pesa za huduma kwa jamii uchunguzi uliofanywa unaonekana kuna uzembe mkubwa sana TRA kwa kutotambua baadhi ya kodi na kuzifuatilia na kubaki wakiwakandamiza wafanyakazi kulipa PAYE kubwa ambayo ukusanyaji wake hauna jasho.

  Uchunguzi unaonesha kuwa Wamiliki wengi wa majengo , nyumba za kupanga, guest house na hata za makazi hawalipi kodi ( Income tax ) inayotokana na kupangisha watu. Yaani kama mimi nina nyumba nimekupangisha wewe umeweka duka , basi TRA wanafuata yule mwenye duka na kuchukua income tax itokanayo na duka tu, na wala hawahitaji kujua mwenye nyumba pato alilopata kutokana na upangishaji huo amelipa nini !!!

  Kuna mifano ya watu wawili nilio nao karibu sana :

  1. Ana nyumba pale Kariakoo, of course ni ya urithi ina frame za duka kumi, na kila frame amepangisha 400,000/= kwa mwezi, hivyo anapata 4,000,000/= kwa mwezi kama kodi ya pango kwa wateja wake.
  Lakini yeye haijui TRA na wala hajawahi lipa Income tax. Anachojua yeye ni kulipia kodi ya jengo inayolipwa Manispaa kwa mwaka ambayo huwa ni ndogo haizidi 100,000/= kwa mwaka. TRA wakifika wao na wenye maduka tu!!!

  2.Mwingine naye ni rafiki yangu na ana nyumba yake pale Ilala , naye ana maduka kama saba hivi, amepangisha 350,000/= kwa mwezi . anapata kama 2,450,000/= Tsh kwa mwezi kutokana na kodi ya pango naye haijui TRA kwenye mambo ya Income Tax.

  Na inaonekana ni karibu watu wote wenye nyumba za kupangisha hawaijui TRA , Je haya mapato yanayotokana na upangishaji wa nyumba hayastahiri kulipiwa Income tax??? Kama yanastahiri kwa nini TRA wasichukuliwe hatua kwa kuikosesha mapato Serikali na huku tukiwalipa mishahara minono ili wafanye kazi nzuri.??

  Na hili linaweza kuwa hata kwenye mahotel makubwa tunayoyaona ukaona kodi inayofuatwa ni ile ya biashara tu, lakini itokanayo na pango la nyumba usiisikie!!!

  Yes, hata mimi kanyumba kangu nimepangisha lakini sijawahi ona nikiulizwa mapato yake ili nilipie kodi. Sasa huu ni uzembe au hakuna sheria ya kodi ya pango.???
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mpendanchi concern yako ni sahihi kabisa!......pia last week tulijadili sana suala hili kny thread iliyoanzishwa na Kandambili kuhusu PAYE .....unaweza ukaipitia pia mkuu!

  Hawa TRA wanapenda sana miteremko ya kukusanya na kufuatilia kodi through organised systems kama kny makampuni, PAYE,Motor vehicles etc huko kny informal sector no one bothers kufuatilia kodi kabisa though huko kuna watu wengi wanapiga hela sana na it goes out untaxed!

  Kwenye issue tu ya rental income....!sheria ya kodi ya 2004 inataka mtu yeyote anayelipa kodi ya pango la nyumba, ofisi kuzuia kodi at the rate of 10% of gross payment. Kwa hiyo hao jamaa zako wa karikoo wanatakiwa income yao iwe reduced by 10% na mpangaji wao ambaye anatakiwa kuziwasilisha TRA!

  Lakini kama ulivyosema, hakuna anayefanya hivyo, na TRA hawagusi kabisa maeneo hayo....utadhani ni vipofu vile!

  This needs to change kwa kweli!
   
 3. B

  Bobby JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mpendanchi, TRA kama zilivyo government arms zingine mambo yao ni business as usual hakuna creativity wala nini, wao wameng'ang'ani magari, bia, sigara, mafuta, PAYE basi wakati kuna mabilioni kibao maenea mengine yanapotea bure. Mfano ni hayo mambo ya rent, tena afadhali umetaja hao wa kariakoo. I know someone ambaye ana wapangaji kama 20 ambao hivi ambao kila mmoja anamlipa USd 3000 kwa mwezi. U know what, halipi income tax zaidi ya rental taxi. Kwa hesabu za haraka haraka kwa mujibu wa sheria, kwa huyu jamaa peke yake serikali inapoteza USD 6000 kwa mwezi au USD 72,000 kwa mwaka sasa zidisha mara namba ya landlords wote its a hell of money. Hivi hali hii mpaka lini jamani? Kuna njia nyingi sana za kuwapunguzia makali ya maisha masikini badala ya kuendelea kuwaongezea mzigo wa kodi kila mwaka.
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  UBUNIFU ni ziro kwa uongozi wote Tanzania. Hela nyingi sana haikusanywi nchi hii. Wao ni kubana wafanyakazi tu. mimi mfano wangu ni wanamuziki na kazi za sanaa, hatimiliki ingeimarishwa, tax ingepatikana.
   
 5. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimeongea na jamaa yangu mmoja pale TRA anasema ni kweli hiki kitu kinajulikana na kitengo cha utafiti kilishafanya kazi yake nakujua hiyo source kubwa ya income lakini report tangu ilipokabidhiwa hakuna hatua zilizochukuliwa na uongozi. Hii ina maanisha uongozi ndiyo wenye matatizo!!
   
Loading...