Ni kweli kwamba NSSF wamesitisha fao la kujitoa kwa mikataba iliyoisha kuanzia December 2018 kurudi nyuma?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti, ninasikia NSSF wamesitisha fao la kujitoa kwa wale ambao mikataba yao ya kazi imeisha kuanzia December 2018 na miezi yote ya nyuma?

Nimeuliza hivi kwa maana kwamba kuna dada mmoja ni receptionist wa NSSF mkoa nje ya Dar ndiye amenijibu hivyo nikahisi kana kwamba anatengeneza mazingira ya rushwa.

Nimejaribu pia kuangalia kwenye notice board yao pale ofisini, hawajaandika kitu.

Mwenye taatifa sahihi naomba please.
 
Unasikia

Halafu December kurudi nyuma una maanisha 2017 au 2019
 
Pole hawa jamaa inaonekana pesa za kulipa hawana na sababu haZiwaishi na wanalipa wanavyotaka wao. Ambazo hawataki kulipa ni zile za mkupuo, wanasema wanafao la kukosa ajira na ile 1/3 pesa zako
 
Nenda NSSF dodoma watakupa form jaza baada ya mwezi unachukua mpunga wako, kikubwa uwe na barua ya kuisha kwa mkataba wako kutoka kwa mwajiri wako
Kwa kuwa kampuni ipo Arusha nikajia lazima nitumie NSSF offices za Arusha. Kumbe sio lazima nitumie offices za mkoa huo huo??
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Eti, ninasikia NSSF wamesitisha fao la kujitoa kwa wale ambao mikataba yao ya kazi imeisha kuanzia December 2018 na miezi yote ya nyuma?
Nimeuliza hivi kwa maana kwamba kuna dada mmoja ni receptionist wa NSSF mkoa nje ya Dar ndiye amenijibu hivyo nikahisi kana kwamba anatengeneza mazingira ya rushwa.
Nimejaribu pia kuangalia kwenye notice board yao pale ofisini, hawajaandika kitu.
Mwenye taatifa sahihi naomba please.
NSSF imefirisika kwani hata hao wazee wastaafu hulipwa baada ya makusanyo ya mwezi ya walio kazini.
 
ANKO anaua mifuko,amekomba fedha zote anaenda kujenga WHITE ELEPHANT Project ambazo hazina tija yeyote!! Mfano SELANDER Briji ni Wizi tu na upotevu wa fedha,STIGOLAZ GOJI muhimu ila fedha ni nyingi sana kazipiga cha juu,madege nayo kapiga cha juu na hayana faida yeyote.
 
Pole hawa jamaa inaonekana pesa za kulipa hawana na sababu haZiwaishi na wanalipa wanavyotaka wao. Ambazo hawataki kulipa ni zile za mkupuo, wanasema wanafao la kukosa ajira na ile 1/3 pesa zako
Mie nasubiria jamaa amalize muda wake 2025 ndipo nikakombe hela zangu zote.Naamini atakayekuja atabadilisha hiyo sharia kandamizi na kinyonyaji
 
Mie nasubiria jamaa amalize muda wake 2025 ndipo nikakombe hela zangu zote.Naamini atakayekuja atabadilisha hiyo sharia kandamizi na kinyonyaji
Halafu kuna mainzi ya kijani full kumwabudu, tutafika tu Tz ni yetu wote!!
 
Inasikitisha hata Mimi nadout juu ya hilo, maana mwanzo nilikua Nssf mwezi Wa NNE wakasema wanatenganisha mifuko , Wakaanzisha mfuko unaitwa PSSF et huo ni kwa ajili ya walioajiliwa serikalini na NSSF KWA ajili ya wasiokua serikalini!.. Sasa nataka nikombe ela zangu zilizopo nssf then nianze na moja pssf wamegoma... Na pesa za Nssf wamegoma kuzihamisha...
 
Awa jamaa nilienda kujiandikisha kwa mara ya kwanza,niliwahoji maswali kuhusu fao la kijitoa apo baadae kama ikitoe,awakunipa majibu sahihi walikuwa wanalukaluka tu,nikajua hawa awajiongozi ila wanaongozwa na mkulu.
 
Hahahahaha..wasanii sana hao jamaa, kuna siku nilitembelea ofisi za PSSF maeneo ya samora-posta DSM kuulizia je kweli ninaweza kupata stahiki yangu kutokana na jasho langu.

Basi nikapata wasaha wa kukutana na mhudumu pale dirishani, tulisalimiana kwa kujuliana hali,kilichofuta nikabidi nimueleze adhma ya mimi kuwa pale kuwa nimekuja kuulizia amana yangu ambayo ipo kwenye akaunti ya mfuko karibia milioni 5 hivi je taratibu zipi za kufuata, mhudumu yule akaniambia wewe huwezi kupata hii pesa yako mpaka utakapofikisha miaka 55 na hata ile sheria ya Fao la kukosa ajira hautaweza kupata kwa sababu uliachishwa kazi kipindi sheria hiyo haijapitishwa, kwakweli nilihuzinika sana ikanibidi nimuombe kwenda kuonana na supervisor wake kwa ufafanuzi zaidi, nilipata nafasi hyo ya kuonana na huyo supervisor alichoniambia tu kuwa serikali wanatunga sheria kandamizi za kiwaumiza watu.

Akaendelea kusema kutoka u-layman wake katika sheria ya fao la kukosa ajira linawalenga wote haijulishi huyu sheria imemtangulia kabla/baada basi akani printia hyo fomu ya fao la kukosa nijaze ili niwawasilishe kwa ajili mchakato wa malipo.

Kiukweli hawa jamaa sio wa kweli kila mmoja ana majibu yake ili muradi wakutoe kwenye reli, nami nimejiongeza kuwa pesa kwenye hiyo mifuko hakuna kutoka na kundi la wanaolalamika juu ya hayo mafao.

Lifumo lipo ndani nasubiri kusikia sauti za miungu watu wakisema wapeni ndio nitahangaika kujaza form na kufatilia kilicho changu.
 
Aisee, Mm namuonaga akihutubia watu wanapiga makofi nashangaa.
Mm naona kujiunga hii mifuko ya pensheni iwe ni hiari tusilazimishane
 
Back
Top Bottom