Ni kweli kwamba kikatiba bado hatuna Waziri Mkuu?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,961
48,763
Nawaza tu
Screenshot_20210716-152620.jpg
 
Kwanza 2025 atakuwa amekuwa waziri mkuu miaka 10. Inatosha sasa waje na wengine, ila kwa uchu wake wa madaraka atataka awe tena PM ( kama Urais wasipompa ridhaa, na hii ya Urais alishaanza kujipanga Marehemu akamgundua). Huyu inasemekana ni katika waliotaka Mama asiwe pale kwa 'namna' yeyote. Narudia tena kwa 'namna' yeyote ile, wenye akili mmenielewa
 
Hafai hata hiyo nafasi kapewa kubwa sn
 
Kwanza 2025 atakuwa amekuwa waziri mkuu miaka 10. Inatosha sasa waje na wengine, ila kwa uchu wake wa madaraka atataka awe tena PM ( kama Urais wasipompa ridhaa, na hii ya Urais alishaanza kujipanga Marehemu akamgundua). Huyu inasemekana ni katika waliotaka Mama asiwe pale kwa 'namna' yeyote. Narudia tena kwa 'namna' yeyote ile, wenye akili mmenielewa
walikuwa na mimacho na jafo hawakutaka
 
Ni kwa vile hakula kiapo kwake, au?
Kwa vile hakumteua yeye kwa mujibu wa katiba.
Niliwahi andika humu kuwa ilibidi baraza zima la mawaziri lijiuzuru ili rais aanze kwa kumteau waziri mkuu, halafu akishauriana nae waunde baraza la mawaziri baada ya waziri mkuu kukubaliwa na bunge na kuapishwa na rais
Nukuu ya katiba hii hapa
SEHEMU YA TATU

WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI

NA SERIKALI

Waziri Mkuu

51
.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano

atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na

ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais

kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa

na Bunge.

(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku

kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua

Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi

anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi

Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge

wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio

wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika

madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa

na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge

walio wengi.

(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri

Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi-

(a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;

Kwa hiyo Rais Samia alipoapa kushika kiti cha urais ndipo uwaziri mkuu wa Majaliwa ulipokoma.
 
Yule hata akila kiapo hata huwa sijui anafanya nini?
Huwa ni msaada sana kwenye kusema uongo! Unamkuta macho makavuuu!! "Tumeajiri walimu elfu 5 wiki mbili zilizopita" 😁😁😁

"Rais ni mzima wa afya! Anaendelea na shughuli zake kama kawaida. Au mlitaka mmuone Kariakoo akinunua mboga" 😁😁😁! Kumbe mzee tayari yuko katika mikono salama ya Izrael mtoa roho!
 
KATIBA ILIKUFA RASMI PALE CCM ILIPO MTEUA MWENDAZAKE KUWA MGOMBEA WA URAISI TANGU 2015 HADI LEO NCHI INAONGOZWA KWA UTASHI KABISA!!!
 
Huyu hajui kusoma katiba. Kifungu hicho 51(3)(a) kinachotumiwa na wasoma katiba mbumbumbu kama huyo kilitumika wakati JPM anaapishwa baada ya uchaguzi kwa mujibu wa kifungu 42(1), na kitatumika tena baada ya uchaguzi ujao.

Baada ya JPM kufariki, SSH alirithi mamlaka ya urais chini ya kifungu 37(5) ambacho hamtambui kama ni rais mteule bali ni makamu wa rais ambaye ana vacate nafasi yake kujaza nafasi ya rais, na hivyo kumtaka apendekeze jina la mtu atakayekuwa makamu wa rais.

SSH anaweza kufanya reshuffle ya cabinet yake wakati wowote kulingana na anavyoona yeye kiutendaji, lakini siyo kwa sababu watu waliokuwa wameteuliwa na SSH walipoteza sifa za kuendelea baada ya JPM kufariki. Bila hata kufariki, bado JPM angeweza kuondolewa madarakani na hao hao wateule wake kwa mujibu wa kifungu 37(2) halafu SSH akajaza nafasi hiyo kwa mujibu wa 37(5). Iweje cabinet iwe na power ya kumwondoa rais madarakani halafu na yenyewe isiwe halali tena baada ya kufanya hivyo?
 
Kwanza 2025 atakuwa amekuwa waziri mkuu miaka 10. Inatosha sasa waje na wengine, ila kwa uchu wake wa madaraka atataka awe tena PM ( kama Urais wasipompa ridhaa, na hii ya Urais alishaanza kujipanga Marehemu akamgundua). Huyu inasemekana ni katika waliotaka Mama asiwe pale kwa 'namna' yeyote. Narudia tena kwa 'namna' yeyote ile, wenye akili mmenielewa
Akiwa raisi huyo nchi itarudi kuwa ya hovyo kama mwendazake
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom