Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Jun 24, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  JADILI..
  Hii ni mada inayojadiliwa Star TV.Mawazo yanayotolewa yanatisha..
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama hujafunga ndoa...angalia machungu mwenzio anayokupa kabla hamjaoana...tafakari uyawaze..jiulize mkishaoana utaweza kuyavumilia?

  Ikiwa unaona utaweza kuyavumilia ( tamaa ya pesa/mali,lugha mbaya, ulevi, uongo, kutokua mwaminifu, uchafu, uvivu,kutokuwa na huruma, kutokuwa na kauli nzuri/tamu, kutokusema samahani, kutokujua kubembeleza, ubinafsi,uchoyo, ) BASI KAFUNGENI NDOA na hii ni kwa wote wanawake kwa wanaume.
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....nice one WoS, ...unajua mimi ningeulizaje?  Tena ningeweka na kura, Jibu la NDIO au HAPANA.

  ....nadhani kura zitafungana.

  AM
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mbu binadamu tunapokuwa kwenye mapenzi mara nyingi huwa ni raha tupu. Binadamu tunazijua kasoro zretu ambazo wapenzi wanaweza kuzikubali na nyingine ambazo hawatakuwa tayari kuzikubali hivyo kipindi hicho cha mapenzi moto moto ni nadra sana kuzijua kasoro za umpendaye. Sasa unapoamua kuolewa naye au kumuoa basi ndiyo sasa anaanza kuonyesha makucha yake na kama nilivyosema kuna kasoro nyingine zinavumilika kabisa maana hakuna binadamu ambaye yuko perfect. Kwangu binafsi sipendi uongo, uchafu, wizi, uhuni, ulevi, dharau, kutokubali makosa na kusema samahani , kutojua kupika, uvivu wa kupita kiasi. Hizi kwa kweli si rahisi kuvumilika kabisa ukiuingia mkenge kama huu ni bora kujinasua haraka sana kabla ya kukumbana na matatizo utakayoyajutia kwa miaka mingi baadaye.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Si kweli WOS wengine waliingia kwenye ndoa kwa sababu ya fashions na wao waonekane wanandoa :A S-rose:
  Wengine waliingia kwenye ndoa kwa kujilazimisha
  Wengine walibeba mimba ikawalazimu kuingia kwenye ndoa
  Wengine wamefata pesa au mali ndani ya ndoa
  Wengine wanajiegesha jua litulie kisha waendelee na safari
  Wengine wapo kwa ajili ya heshima ya wazazi.
  wengine ni kweli wanapendana..:A S-rose:
  NK. Nk.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  itabidi tuwe na poll on this at some point....
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Umenena vema Shostito!
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyeusi tiii BAK!
  Wapo wengi walioziona tabia hizi - kama siyo zote basi baadhi na kudhani watarekebishana mbele kwa mbele!
  Utakuta labda mfano tu: Mwanaume mhuniii kupitiliza lakini bashasha zake usipime, au mwanamke mvivuuuu hajui hata kupika uji lakini mwanaume kafa hasikiii kisa urembo wa bibie au lugha lainiii ..mahabat! Mwaume mleviii komba kasingiziwa lakini faranga ziko za kutupatupa...nadhani ni swala la kupima na kuona mtu anataka nini mwisho wa siku...... nahaya hupelekea ndoa chungu mwanzo mwisho.
   
 9. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama alivyosema FL1 kila mtu aliingia kwenye ndoa kwa sababu zake binafsi. lakini wapo walioingia kwa mapenzi makubwa lakini kumbe hawakujua tabia halisi za wapenzi wao na ndio chanzo cha machungu mengi kwenye ndoa.
   
 10. T

  Tall JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.wachache sana wanaopendana kwa dhati.walio wengi wapowapo tu.
  2.kabla ya ndoa unategemea mambo mengi sana.....baadae ukiwa ndoani unakuta ni sifuri au tano ya mia tu!!!
  3.mkiwa wachumba mabaya yote ya mwenzio yanaongezeka mara tatu hivi baada ya ndoa.
  4.baada ya ndoa sasa unapata hali halisi ya mwenzio. Usuke au unyoe ni hiari yako.
  5.hali hii inatokana na wachumba kujifanya watakatifu sana kabla ya ndoa.
  6.wakati fulani ndoa ni kama mchezo wa bahati nasibu ambapo baada ya kununua tiketi,huwezi kuichana ukigundua. Hujashinda.
  7.hata hivyo ndoa ni uhusiano mwema sana sana,utadhani wapo peponi,na ndio maana wenye wivu hutaka kuingilia
  8.upande mwingine hakuna jehanamu kama kwenye ndoa,wanandoa wengi huuana.ugomvi huanza taratibu mwisho kifo.
  9.ushauri:
  1.mpende sana sana mwenzio
  2.siku zote mtendee haki.
  3.mvumilie na msamehe.usilipize kisasi
  4.hata siku moja usihesabu mabaya yake.
  5.mtunze,mheshimu sana na umjali.
  6.usimdanganye na uwe mwaminifu hadi kufa.
  7.yeye kwanza kwa kila jambo.
  8.acha wivu wa kijinga
  9.epuka kumkwaza mwenzio.
  10.usimdharau mwenzio.
  hayo ni baadhi tu ya mambo na mkiweza hayo ndoa hiyo itakuwa ni raha tupu,raha ya ajabu sana.
   
 11. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ishu ya ndoa ni complex sana, si wote walio ndani ya ndoa wanapendana, ndoa nyingine ni kwa mashindikizo ya wazazi, mke au mume.Ndoa ukiiwaza sana kichwa kinauma na kama we bachela unaweza usioe, Muombe Mungu umpate mke mzuri.:dance:
   
 12. Tshala

  Tshala JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 246
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mwingine anafahamu mwenzie anatabia kadha wa kadha anajipa moyo kuwa maybe atachange, wakifika ndani inakuwe worse na hapo ndipo majuto huanza!!! FL1 you said it all!!!
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,982
  Likes Received: 23,684
  Trophy Points: 280
  Kabla sijamuoa huyu mama matesha wangu nilikuwa na mpenzi wangu niliyekuwa nampenda sana. Ki ukweli tulipendana sana. Na tuliachana bila kujua kimetokea nini. Niliumia sana, nilitaabika sana. Sikuwa nahitaji kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine awaye yote. Nilitamani kuwa padre.

  Mpaka alipotokea huyu rafiki yake nu huyo mpenzi wangu wa zamani. Alikuwa ananionea huruma sana, alikuwa ananifariji na kunipa moyo. (Tulipoachana na mpenzi wangu, mpenzi wangu huyo alitokomea kubeba mabox na mpaka leo hajarudi -RIP kama ameshakufa). Huyu rafiki yake ndio huyu mama matesha wangu.

  Nadiriki kusema nashukuru niliachana na mpenzi wangu yule wa zamani kwa kuwa huyu mke wangu wa sasa ndio ulikuwa mpango wa Mungu awe mke wangu. She is beautiful, loving and caring. Sitajuta kuonana naye (sijawahi kujuta miaka yote 15 ya kufahamiana toka urafiki, upenzi, uchumba mpaka ndoa.

  Hivi thread inasemaje?? Oooh Yes.... Mimi na mke wangu Tunapendana sana. Ndani ya ndoa yetu tunapendana. Period!!!
  (Am sore leo sina hangover ya kutosha)
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ni ngumu sana kujua tabia halic ya mpenzi wako mpaka mtakapoanza kuishi pa1, hapo ndio utauona uhalisia wa mtu!...lakini kuna vile vitu vya kuweza kuonekana kaam ulevi kupindukia/uchafu nk lakini bado hapo hapo anaweza ku petend kwamba amebadilika kwa nia ya kukupata mkishaingia ndani vyote vnajirudia kama awali...heee
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is a very strong post; na ukiisoma kijuu-juu utaogopa; lakini hii inaonyesha umuhimu wa kujuana kabla ya ndoa
  tunatakiwa tufike sehemu hata ukiambiwa partner wako kafanya kitu wala hushangai kwani mnajuana
  as always, to be committed to someone, one needs a checklist and the positives must outweigh negatives --- in totality yaani hata waliozunguka penzi lenu

  BUT ALL IN ALL, LONELINESS IS MORE SCARY AND SUICIDAL IN NATURE....

  THERE IS A SONG NI WA ZAMANI LAKINI K-CI WA JOCEDI ALIIMBA KWENYE SOUNDTRACK MOJA UNAITWA "IF YOU THINK YOU LONELY NOW" - LOVELY

  I just wanna dedicate this song to all the lovers
  tonight
  And I expect that might be the whole world
  Because everybody needs someone or something to love,
  yeah

  When its cold outside, girl, who are you holding
  Youll be holding me, well, well, well, well

  Said if yall dont mind, can I talk about this woman
  I have
  Shes always complainin bout the things she got
  And the things her girlfriend got
  But lady, I wanna let you know
  I cant be in two places at one time

  If you think youre lonely now, ooh, yeah
  Wait until tonight, girl
  If you think youre lonely now Oh, you better wait
  till tonight, yeah, baby
  Wait until tonight, girl Ill be long gone

  If you think youre lonely now Yes, I will
  Wait until tonight, girl You better wait until
  tonight
  When scary ghost come out of your closet, it chased
  you all around the room
  Memories sail like a ghost, ah, baby, baby

  If you think youre lonely now If you think youre
  lonely now
  Wait until tonight Wait until tonight, wait until
  tonight, baby
  If you think youre lonely now Yeah, yeah

  If you think youre lonely now Hold on, ooh, yeah
  Wait until tonight, girl Ooh, ha
  I wanna testify, I wanna testify
  I wanna testify to you, I just got one thing to say
  If you think youre lonely now

  If you think youre lonely now Baby, yeah
  Wait until tonight, girl Sugar, feel, oh
  If you think youre lonely now Ooh, yeah

  Wait until tonight, girl Oh, dont be a fool

  If you think youre lonely now Baby, please dont be
  a fool
  Wait until tonight, girl
  If you think youre lonely now I want you, baby,
  baby, baby, huh
  Wait until tonight, girl

   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,982
  Likes Received: 23,684
  Trophy Points: 280
  Unaona faida ya kumegana kabla ya kuoana?
   
 17. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  ,....:mmph:..Zile Mila za nini sasa
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,982
  Likes Received: 23,684
  Trophy Points: 280
  Mila na desturi lazima zienziwe. Mila zinaleta uzoefu na mbinu mpya katika pafomensi ya kudumisha ndoa...... Askofu unatakiwa kanisani mida hii
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  jibu: hapana
  wengine wapo kwenye ndoa kwa sababu wanahisi ni wajibu wao kwa jamii
  wengine wako kwenye ndoa kwa sababu wanataka watoto na wangependa kupata mwenza wa kuwasaidia kulea
  wengine wako kwenye ndoa kufuatia maslahi binafsi
  wengine wako kwenye ndoa kwa manufaa ya wazazi
  wengine wako kwenye ndoa kwa kuwa ameona labda inaweza kuleta mabadiliko katika maisha yake yaliyokuwa yamedorora
  wengine wako kwenye ndoa ili kukimu mahitaji ya mwili
  wengine wako kweenye ndoa kwa kukidhi mahitaji ya kiroho
  nakadhalika na kadhalika
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,982
  Likes Received: 23,684
  Trophy Points: 280
  Wewe uko kwenye ndoa / utakuwa kwenye ndoa kwa sababu gani?
   
Loading...