Ni kweli kuwa uandikishaji wa NIDA sasa hivi hauwezeshi watu kusajili simu zao?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,450
2,000
Nimeisikia habari hii kwa mshtuko sana, kwamba pamoja na kuongeza muda wa kufanya kazi wa NIDA bado wananchi wanataarifiwa kuwa namba wanaweza kuzipata baada ya wiki sita na vitambulisho miezi kadhaa.

Nimejiuliza kuwa kasi hii ya uandikishaji na hata kuongeza muda wa kazi ni ili kuwezesha watu wapate uwezo wa kusajili namba zao za simu kabla ya tarehe iliyo wekwa ya mwisho.

Sasa kama wanasimama mafoleni hadi usiku na hawataweza kupata namba zoezi hilo la nini? Hizi drama za katika kila jambo na mwishoni mnamshirikisha Rais ili kwanza akitamka apigiwe makofi lakini likifeli alaumiwe "yeye" kimya kimya kwa nini?

Watu waambiwe wazi kuwa waliokuwa hawana namba za NIDA habari ya simu zao wasahau maana zoezi hili ni usanii mtupu na hauhusiani na kuwasaidia kusajili namba zao zamani.

Unless wawaambie kuwa namba za simu zinafungiwa, lakini ukipata namba ya NIDA unaizindua tena simu yako.
 
Top Bottom