Ni kweli kuwa kila anayefariki anaacha pengo?

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Je ni sahihi kusema kuwa mtu anayefariki ameacha pengo? Naona ni kama vile tunamkufuru Mungu maana karibu kila anayefariki kwa mtazamo wangu ni kwamba amekamilisha jukumu/kusudi lake alilokusudiwa duniani.
 
Pengo ni kwa wachache sana kuna wengine huwa tunasema bora amekwenda ,mkeo mmeo pengo ni la muda tu hasa kama mlipendana kwa dhati pengo hilo linalosemwa ni ile lonliness tu na kukosa yale mambo muhimu walokuwa wanapata kutoka kwa marehemu.hivi kuna watu bado wanafikiri eti kanumba ameacha pengo!naamini kwa siku nzima kuna watu hata hawamkubuki.
 
pengo polkap cardinal,ameachwa na wengi basi kama ni hivyo
 
kaacha pengo au kaacha mwanya?
nawale majambazi wanakuwa wameacha nini?
 
kama alikuwa ni jino basi hakika atakua kaacha pengo...
 
Nimeshaeleza mtazamo wangu hapo mwanzo.

nadhani umeeleza vema kwa mtazamo wako na hata kwa namna ile ambavyo vitabu vya dini vinatufundisha. Kila binadamu amezaliwa ana kusudi maalumu hapa duniani la kukamilisha.
Yamkini anaweza akawa amemaliza kusudi lake lakini pia kwa familia ambayo ameishi ameacha pengo. Kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku, familia zetu ni muhimu sana na kwa kadri ya upendo tulionao juu ya ndugu zetu katika familia lazima tupate pigo pindi tunapompoteza mmoja wetu.
Hata hivyo, naomba ieleweke wazi kuwa kifo kama kifo, kuna kifo ambacho ni kusudi la Mungu muda wako ukifika na kama umelimaliza kusudi alilokuitia huna budi kufa. Lakini pia ibilisi anawawinda watu na kusababisha vifo ili wasipate neema ya kumjua Mungu na kuikaribia toba.
 
Inategemea kama ni jino la chini au la pembe ila nackia cku hz kuna meno bandia hivyo kuacha pengo ni kupenda mwenyewe
 
Ni kiswahili tuu
Kama ni mtu wa karibu lazima uhisi ukiwa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom