Mbega Mzuri
Member
- Aug 1, 2008
- 44
- 2
Wanajamii wenzangu nakuja na mada hii. Msinielewe vibaya, lakini kwa faida na ustawi wa jamii.
Ngono: ni neno linalozungumzia kwa mapana mambo mengi sana yakiwemo kutazama picha za ngono, kujichua na mambo mengineyo. Lakini kwa baadhi ya watu, wingi wa ngono na titendo vyake, vinavyochangiwa na utamaduni wa Kimagharibi umekuwa mtego, ambao ni mgumu kuweza kuukwepa. Utumwa au uraibu wa ngono baadhi wanauita ugonjwa uliojificha. Wengine wanauita dhambi isiyozungumza.
Wakati watu wengi huweka taswira ya wanyama waliopagawishwa na mapenzi, ukweli wa utumwa wa ngono uko tofauti. Wengi wa waathirika siyo wahalifu kifikra na siyo kwamba wazembe.
Lakini ni nani hawa watumwa wa ngono? Hapa ndipo naamua kuileta hoja mbele ya wanaforum ingawa jibu linaweza kukushangaza. Mtu yeyote anaweza kuwa mtumwa wa ngono, kwa sababu ndiyo njia ambayo tumekuzwa nayo tangu tukiwa watoto na tuliendelea nayo mpaka kwenye balehe. Siyo inatokea wakati tukiwa na umri wa miaka 40. Na wengine wanasema kwamba hiyo ndiyo sababu watu wasishangae kuhusu kashfa za ngono zinazotokea ndani ya jamii zetu. Mwathirika wa utumwa huu hawaelewi chochote, na kwa mtu wa kawaida, tabia hii inaonekana kuwa mbali sana na haisadikiki, hawawezi kusadiki.
Ukweli kwamba waathirika wengi wa utumwa wa ngono ni watu wenye familia zao, kazi zao na hata ni waumini ama viongozi wa dini unaweza kuwashangaza watu wengi sana na kuleta matatizo makubwa kwa wahusika wenyewe na jamii kwa ujumla.
Fikiria, unaweza kumkuta baba mzima mwenye familia yake na fedha zake akitangatanga na watoto wadogo, tena wale wa shule, huku akimwacha mama watoto wake akiwa hajui lolote. Mama mzima mwenye fedha na maisha ya hali ya juu, anamwacha mumewe na kutafuta vijana ili waidhi kiu yake ya mapenzi, kwa madai kwamba mumewe amechoka na akifika mshido mmoja yuko taabani kabisa!
Vijana wanakwenda kujiunga na kwaya kanisani kwa sababu tu ya kumpata binti fulani, na wengine hufikia hata hatua mbaya zaidi kwa kuamua kutangaza wameokoka ili wawe karibu tu na msichana mwenye msimamo anayemcha Mungu kwa bidii.
Mapadre wanasema kwamba hawaruhusiwi kuoa, lakini kutokana na utumwa wa ngono unaowasakama utakuta ama wanafanya mapenzi na watawa wa kike au kutafuta wanawake wa pembeni, na tayari kuna mashauri mengi hapa Tanzania ya aina hiyo. Wapo wachungaji wengi wa Kondoo wa Bwana ambao wamekwishashikwa ugoni ama wakiwa na wake za watu au wake zao kuwafumania na wahudumu wa kanisa. Wapo mashekhe ambao pamoja na kuwa na wake wanne kama dini ya Kiislamu inavyoelekeza, lakini utakuta wana vimada zaidi ya sita mitaani!
Lakini niseme tu kwamba, huu ni ule upande wenye giza. Ni upande ule wa kuzifurahisha tamaa zao za mwili ambazo zimetengana na fikra zao za kawaida, mpaka watakapokamatwa au kufumaniwa au kitu fulani kilete dunia hizi mbili pamoja na kuleta mgongano.
Wapo ambao utumwa wao wa ngono unatokana na mambo mengi: makahaba, picha za ngono, klabu za usiku ambako wanawake wanacheza uchi na kupendelea kuchukua wanawake tofauti kila siku (one-night stands). Lakini utumwa wa ngono haumaanishi kwamba mpaka ufanye mapenzi na mtu mwingine. Unaweza kuwa unajichua mwenyewe, kutazama picha na sinema za ngono na mambo mengine. Hizi ni tabia za mapenzi zinazozidi na kuhamasisha zaidi.
Kwamba mtu hatimaye huanzisha uhusiano na tabia hiyo na kuifanya tabia hiyo katika kuleta madhara makubwa. Mwathirika ataendelea kufanya ngono nje pamoja na uwezekano wa kuipoteza familia yake au kupoteza kazi na heshima pia.
Waathirika mara nyingi hupoteza maelfu ya fedha katika vitendo vyao, wakiziacha familia zao zikiteseka kwa kukosa msaada wa kifedha. Nyumba ndogo, kama wenyewe wanavyoita, hutaka kutimiziwa haja zao haraka sana bila kujali hali ya kipato ya mwanaume husika, na matumizi yao mara nyingi ni makubwa kuliko ya nyumbani kwao. Waathirika mara nyingi hupenda kutumia fedha ili kununua mapenzi na kuwaonyesha hao vimada kwamba wanawajali, lakini wakisahau kwamba huko nyumbani moto unawaka na paka kalala mekoni! Aibu na hatia huchukua nafasi haraka katika raha zao na baadaye huanza kujilaumu kwa vitendo hivyo, ambavyo hata hivyo huwa ni vigumu kwao kuviacha. Njia pekee ambayo wanaweza kuifanya katika kukabiliana na aibu, hatia na maumivu ni kuendelea kufanya vitendo hivyo.
Uga wa saikolojia umekuwa mgumu kukubali kwamba utumwa wa ngono ni uraibu kama ilivyo kwa pombe na dawa za kulevya, lakini wataalamu wanasema unaweza kubomoa maisha ya watu katika njia na kiwango kile kile kama pombe na dawa za kulevya.
Utumwa wa ngono siyo ni kiasi gani au mara ngapi mtu anafanya mapenzi. Utumwa wa ngono ni kuhusu mtu fulani kutumia mapenzi ili kukidhi haja zake za kiakili. Wanatumia kama kimbilio kupambana na msongo wa mawazo. Wanatumia kupambana na maumivu yaliyopita. Wanatumia ili wapendwe wakubalike. Wanakimbilia kwenye ulimwengu wa kufikirika badala ya ulimwengu halisi. Ni kama kuwa katika ukuta wa kioo. Unaweza kuuona ulimwengu, lakini huwezi kuugusa na wala wenyewe hauwezi kukugusa. Hivi ndivyo ulivyo utumwa huu. Unataka kuwafikia watu, lakini huwezi, unakuwa umekwama na unajiona kama maisha yako yamepotea na kubomolewa.
Ni kitu gani kinachosababisha tumwa huu? Kama uraibu mwingine, wanasaikolojia wengine wanaamini kwamba ubongo wa baadhi ya watu umeachiliwa huru kwa ajili ya uraibu, iwe pombe, dawa za kulevya chakula au ngono. Tatizo jingine kubwa ni unyanyasaji wa kimapenzi (tutakuja kujadili siku zijazo). Asilimia 82 ya waraibu wa ngono wameshawahi kunyanyaswa kimapenzi wakati wakiwa watoto.
Ninawaomba wanaforum, changieni suala hili maana linatuhusu sote wanajamii. Ninaamini inawezekana kabisa utumwa wa ngono ndio unaoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa hata maambukizi ya maradhi mbalimbali ya zinaa, ikiwa ni pamoja na umaskini ; wa fikara na kipato.
Karibuni sana !!!
________________________________________________
If a woman cant do her job, let other women do it for her!!