Ni kweli kuna kipimo cha kujua utimamu wa akili ya mtu?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,869
2,000
Mara nyingi tunasikia kwamba fulani anatakiwa kupimwa ili kujua utimamu wa afya yake ya akili. Hili hutokea hata katika mahakama zetu ambapo zimeshawahi kutolewa amri mtuhumiwa akapimwe akili

Suala hili huibuliwa wakati mtu kafanya jambo ambalo katika jamii linaonekana sio la kawaida na likawa na madhara kwake yeye mwenyewe, kwa mtu au watu wengine au hata kwa jamii nzima kwa ujumla

Naomba kuwauliza wataalamu wa afya kwamba kipimo cha akili ni kipi na kinaitwaje? Je kuna kifaa au mashine maalumu kwa ajili ya kipimo hicho kama vile MRI, CT Scanner, Microscope etc?

Je kuna sample yoyote hua inahitajika kutoka kwa anayetakiwa kupimwa akili kama vile urine, stool, blood au hata bone marrow?

Je ni sahihi pia kipimo cha IQ ya mtu(kama kipo) kinaweza kupima utimamu wa afya ya akili kwa binadamu?
 
Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
412
1,000
Mkuu, kupima akili (intelligence) ya mtu ni kazi ngumu. Mmoja ya sababu ya ugumu ni kwamba kuna aina nyingi ya intelligence :-

General Intelligence - akili ya kawaida - logic, kumbukumbu, hesabu, uelewa, nk - hii inawezwa kupimwa na IQ;

Emotional Intelligence - hisia, kufahamu mbaya na nzuri; kuishi vizuri na watu, nk (score yako kwenye hii itakuwa ya juu sana);

Artistic Intelligence - kuchora, kuandika, kuimba nk;

Spatial Intelligence ya kufahamu mazingira - mtu unamzungusha Kariakoo mara ya kwanza, na anapafahamu vizuri, na mtu mwingine (kama mimi) unamzungusha mara hamsini na kila mara anapotea.

Kwa sababu ya akili kuwa ya aina nyingi na tofauti, kupima kwa standard mmoja haiwezekani.

Halafu akili inaweza kubadilika na mazingira, wakati, nk - mtu mwenye akili timamu, kaamka vibaya na kufanya vituko, au kakutana na jamaa, kachafuliwa akili na kuanza kuropoka (temporary insanity)!

Wanasema kwamba ubongo wa Einstein imehifadhiwa na inachunguzwa kutafata siri ya akili yake. Binafsi naona hii kama matumizi mabaya ya bongo la Einstein, yaani hata baada ya kufa watu wamemandama! Asante and have a nice weekend, mkuu Zakazaka!
 
Asante sana Mkuu Shaka-Zulu nimefaidika na kuongeza maarifa kwa post yako hii
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,869
2,000
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚pole mkuu nahis siku marais wa Africa wakipimwa bongo zao matokeo ya Mfalme Nebkadreza yatatoa ERROR...!πŸ˜‚βœŒ..au komputa itacolapse
Hapo itakua na tafsiiri mbili ujue, ama Mfalme Nebkadreza unaemsema atakua na akili nyiingi sana kupitiliza hadi mashine inashindwa kusoma au atakua ziro kabisa hadi mashine inamshangaa! Na hapo itahitaji sasa mabingwa kwa kusoma hicho kipimo wajue wamuweke kwenye kundi gani kati ya hayo mawili:D:D:D
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,438

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜€πŸ˜€wtamrefer Sauzi kwa matokeo zaidi..arghhh kichefu chefu tupu
 
Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
412
1,000
Kuna watu ukiwaambia nikupe chemsha bongo, wanadhani unaongea supu!

Kwenye hoteli fulani, palikuwa panauzwa bongo la mjerumani, mchina na 'mheshimiwa fulani'! Bongo ya mjerumani ilikuwa na bei nafuu sana, ya mchina, wastani na ya mheshimiwa bei kali sana! Alipoulizwa sababu ya tofauti kwenye bei ya bongo yaliyofanana, mwenye hoteli akajibu, "Bongo la mjerumani imetumika sana, kwa hiyo bei ni kama ya chuma jakavu. Bongo la mchina, imetumika wastani na kwa hiyo ina bei ya second hand. Bongo la mheshimiwa haijatumika hata kidogo, na kwa kuwa it is as good as brand new, ina bei ya juu kabisa!"
 
Hahahaaa inawezekana watu wenye rangi nyeusi walikimbilia kupata brandi nyuu?
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,869
2,000
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Sipunda genius best sema tu amezid ukomedi
Sasa hebu nisaidie jambo moja mamii(I presume you are a lady), huyo Mfalme wako Nabkadreza ana control kila kitu kuanzia watu wanaomuunga mkono anawaburuza atakavyo, wanaompinga anawabana hawafurukuti, anakaa na fedha yote ya ufalme wake na kuitumia atakavyo bila kufuata mipango iliyowekwa na baraza la kutunga sheria za kwenye falme yake, upendeleo wa ndugu zake n.k

Wananchi wake wapo kiiimya kabisa na kunawanaomuimbia mapambio, huoni kua Mfalme huyo ni genius akili kubwa hasa ukizingatia ufalme wake unawatu mamilion meengi na miongoni mwao kuna wasomi waliobobea kwa kila fani na wote amewa control?
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,438
2,000
Sasa hebu nisaidie jambo moja mamii(I presume you a lady), huyo Mfalme wako Nabkadreza ana control kila kitu kuanzia watu wanaomuunga mkono anawaburuza atakavyo, wanaompinga anawabana hawafurukuti, anakaa na fedha yote ya ufalme wake na kuitumia atakavyo bila kufuata mipango iliyowekwa na baraza la kutunga sheria za kwenye falme yake, upendeleo wa ndugu zake n.k

Wananchi wake wapo kiiimya kabisa na kunawanaomuimbia mapambio, huoni kua Mfalme huyo ni genius akili kubwa hasa ukizingatia ufalme wake unawatu mamilion meengi na miongoni mwao kuna wasomi waliobobea kwa kila fani na wote amewa control?

πŸ˜‚πŸ˜‚Mie na uhenga huu nilionao naamini kbs tatizo kubwa kabisa kwenye ile nchi ya mfalme Nebu..tatizo ni watu wakaao mle..!walishazoea ujamaa na vitu kama hizo..woga wenye hof tu ya vita..!ndio maana mfalme ameshajua weakness yao basi hakuna wa kufurukuta..
Nadhan anataka kufanana na mfalme Herode wa kwenye biblia..!ila iko siku utawala wake utapinduliwa tu na falme itashikwa na wabarikiwa (wenye akili)..!sasa hv kisiwa kile wanaishi kwa hofu na uvumilivu mkubwa mno mno!..naifananisha na ile muvie ya miaka ileee inaetwa Escaping from Sobibor!

πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…hivi tukisema na yule Masilingi apimwe akili jaman πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚...πŸ™ŠπŸ™ŠπŸ™ŠπŸ™ŠπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘..ataandikiwa dawa za kumeza kwa miaka 10 mfululizo..mxiewwww
 
Dah! Kazi ipo kwakweli, ni hatari
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom