Ni kweli kuku wa mayai hutaga mara mbili kwa siku?

Al Adawy

Member
Apr 15, 2017
12
8
Nimesikia wafugaji wengi wa kuku wa mayai wakisema huwa wanakusanya mayai asubuhi na jioni kwakuwa kuku wa mayai hutaga mara mbili kwa siku.je hii ni kweli?
 
Ni routine tu wamejiwekea..Wanakusanya mara mbili sababu wakiyaacha muda mrefu kuku wanaweza kuyavunja kwa wale kuku wanaofugiwa chini bila cages. Na pia huwezi kukusanya mayai kila muda sababu hujui kuku anataga saaa ngapi kwa hiyo lazima uwe na muda maalumu wa kucheki kama kuna waliotaga.

Unaweza ukacheki mchana na jioni..Wanataga mara moja na si wote. Wengine unaweza kuta hawatagi kabisa.. ukiwa na cages ni rahisi zaidi unaweza fanya mara moja kwa siku na kitu kingine unaweza jua kuku wa kwenye cage ipi hawatagi kila siku.
 
Wanataga mara moja tu ila kila kuku anataga muda tofauti na mwingine .hivyo unapokusanya asubuhi ni yale yaliyotagwa usury. Na unapokusaya jioni ni yaliyotagwa mchana.
 
Nimesikia wafugaji wengi wa kuku wa mayai wakisema huwa wanakusanya mayai asubuhi na jioni kwakuwa kuku wa mayai hutaga mara mbili kwa siku.je hii ni kweli?
Kuku hutaga Mara moja tu kwa siku tena sio kila siku.
na kama haitoshi kwenye iyo Mara moja anayotaga hutaga yai moja tu! japo Mara nyingine Yai laweza kuwa na viini viwili.
 
Inawezekana ikawa si kweli, lakini pia inawezekanaje wafugaji wakusanye mayai mara mbili kwa siku na wakati kuku anataga mara moja?
Kwasababu kuku hawatagi wote kwa pamoja. Kwa mfano una kuku 350. Asubuhi unaweza kupata mayai 100 na jioni 150 labda sio kwamba utaenda asubuhi upate mayai 350 na jioni 350. Haiwezekani

Ukitaka kuhakikisha chukua kuku mmoja mtenge uone kama utapata mayai mawili. Kwa wastani yai hutagwa kila baada ya masaa 27-30
 
Yai moja ukomaa ndan ya Masaa 25 iv mpk kutolewa, hivyo piga mahesabu
 
Kwa sababu kuku hawatagi wakati ule ule Mkuu kwamba ikifika 12 asubuhi kila kuku atataga yai wakati huo huo.

Inawezekana ikawa si kweli, lakini pia inawezekanaje wafugaji wakusanye mayai mara mbili kwa siku na wakati kuku anataga mara moja?
 
Ahsanteni wote kwa majibu yenu nimepata kuelewa machache lakini makubwa kutokana na majibu yenu. Mungu awabariki sana
 
Siku hizi wanaojiita wajasiriamali kwenye ufugaji ni wengi. Wanadanganyana vibaya mno mwishowe mfugaji anategemea very big profit. In reality siyo hivyo. Yangekuwa mayai mawili tungekuwa matajiri wakubwa mno. Yaani hata ukiwapa chakula kila saa. Ni yai moja tu...
 
Ukiwapa chakula kila saa hata hilo moja hupati
 
Inawezekana ikawa si kweli, lakini pia inawezekanaje wafugaji wakusanye mayai mara mbili kwa siku na wakati kuku anataga mara moja?
Co KUKU wote wanataga asubuhi kuna wengine hutaga jion na KUKU kutaga Mara moja ndan ya masaa 24
 
Hiyo sio kweli hakuna kuku anayetaga mara mbili hata apandwe mara mia yai moja kila saa 24 au 26
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom