Ni kweli kamata kamata ya wabunge wa upinzani ni uvunjifu wa sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli kamata kamata ya wabunge wa upinzani ni uvunjifu wa sheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jun 5, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukishindwa kufikirisha kichwa chako unakuwa mjinga, ukishindwa kuchambua mambo yanayokuzunguka unakosa sifa ya kutokuwa mwerevu lakini pengine huwezi kuitwa mjinga lakini unaposhindwa kufikirisha kichwa na ukashindwa kuchanganua mambo huwezi kuepuka kuitwa mpumbavu.

  Tarehe 4 /06/2011 tulipata taarifa kuwa mheshimiwa Mbowe alijisalimisha katika kituo cha kati mikononi mwa jeshi la polisi kufuatia kutafutwa kwake na jeshi hilo ambalo linatekeleza amri halali ya mhimili mmoja wa Jamhuri ya Tanzania. Kama alivorejerea Mbowe mwenyewe kuwa hakuwa na tatizo na jeshi la polisi katika utelezaji wa amri hiyo kwa sababu ni maelekezo halali na mhimili ambao umepata madaraka yake moja kwa moja kutoka katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vinginevyo ni sawa na kukiuka katiba ambayo polisi wenyewe wameapa kuitumikia.

  Wakati nakubaliana na hatua ya jeshi la polisi kutekeleza amri hiyo, napata shida kidogo namna walivyoitekeleza`namna walivyofanya jambo hilo kuwa kubwa ama kwa kutokujua au kwa kujua lakini wafanyaje.

  Tunalazimika kukubalina kutofautiana katika mitizamo na hatua za kuchukuliwa kukabili mitizamo kinzani. Ili kufanikiwa katika hili na kwa manufaa ya kutuwezesha tuanzie sehemu moja ya mjadala niombe kuwakaribisha kwa pamoja tuangalie kamatakamata inayowakabili wabunge wa upinzani kama ni kweli inalengo la kuileza jamii kuwa hakuna aliyejuu ya sheria na wote wanalindwa na kutumikiwa na sheria zao bila ubaguzi au upendeleo. Naanza hivyo kwa sababu hapo ndio kwenye mzizi wa tofauti za mitizamo ambayo mwisho wa siku itatupeleka pabaya kama haitapitia katika mikono iliyotukuka na kujaliwa uungwana wa fikira.

  Tanzania imegawanyika katika mikondo ya kiitikadi za kisiasa na kwa hivyo matukio karibu yote mazuri kwa mabaya yanapitishwa katika litmas ya kisisa na itikadi za kivyama na ndivyo wengi wa wasomaji wa makala hayo watakavyofanya ili waamue kuwa mawazo haya ni sawa au hapana. Kukamatwa kwa wabunge kutoka kambi shindani kisiasa na chama tawala imepitia katika tanuru hilo na sasa kukamatwa kwa Mbowe ndio kunaimarisha zaidi mawazo ya upande huo kuwa kuna utekelezaji wa sheria kwa jicho la kisiasa zaidi katika nchi hii na matokeo yake ni "worst is open for this event, if and only if the state hands tying Mbowe's body and hands, have not used their heart to make judgement on what seem to be the finest moment in the history of this country".

  Tunajua Polisi wametekeleza amri ya mhimili mmojawapo katika nchi, ambao madaraka yake yamegatuliwa moja kwa moja katika katiba ya Jamhuri ya Muungano na kwa hiyo hawakuwa na namna yeyote kufanya vingine isipokuwa kufanya kama amri halali inavyotaka.

  Ambacho leo nataka kujadili nanyi ni kuwa hivi polisi wanatumwa kama watoto? Hivi sheria za nchi hazikuacha fursa ya watumishi wetu wa jeshi la polisi kuanzia kwa kamanda mkuu hadi kwa polisi wa cheo cha chini kufanya maamuzi yanayozingatia kurahisisha utekelezaji wa sheria ya ulinzi na usalama wa raia. Ebu fikiria polisi anaekabiliwa na kazi ya kumkamata jambazi au mharifu mwingine yeyote katika jamii hata kama ni mhaini ambaye amewafanya watu 1,000 kuwa ngao yake na kwamba kwa kuwatumia watu hao ni kama anakaribia kumtoroka polisi na ili amuue au amjeruhi na hatimaye amshike atalazimika kuua watu wengi, je aarishe zoezi la kumshika au aue watu amshike? Sheria iko wazi na inataka muharifu akamatwe lakini mazingira aliyomo ni magumu kidogo lakini pia ili polisi atekeleze amri kikamilifu itabidi kwa haraka ajiulize kama ataua watu wangapi, kumkamata mhalifu anaokoa maisha ya watu wangapi ambao wanatishiwa na muovu huyo, ni kwa kiasi gani atakiwa kuvunja sheria ili atekeleze sheria ingine

  Kwa namna yoyote ile watu wengi wana mtizamo tofauti na kukamatwa wabunge wa vyama shindani na chama tawala na hasa Mbowe. Mhe Mbowe alijisalimisha polishi si kwa sababu alikuwa hana jinsi kwamba alikuwa amezungukwa, alifanya hivyo kwa hiari yake na kwamba polisi wangemuuliza kuwa anapenda kupelekwa kwa njia ipi Arusha, apelekwe na Jeshi la polisi au aende mwenyewe akaripoti kati ya jana na leo, Mbowe kwa vyovyote vile hawezi kutoraka nchi kwa kosa hilo anaweza kuaminiwa na vyombo vya dola akajidhamini na kufika mahali anaoptakiwa bila mgogoro na akapewa karipio la kimahakama kwa kushindwa kutii mamlaka hiyo.

  Hakuna anayeshabikia kuona watu wanavunja sheria lakini kunapokuwa na mtizamo tofauti juu ya tukio moja busara inahitajika ili kuepusha shari kwa pande zote. Ni vigumu kuwashaushi wafuasi wa Mbowe au CHADEMA kuwa kukamatwa kwa viongozi wao hakuna msukumo wa kisiasa unaotekelezwa kwa maelekezo ya watu fulani. Mtizamo huu hauwezi kuondolewa kwa nguvu za kipolisi unaondolewa kwa kuelimishana na majadiliano kwa kila upande kuondoka kwenye msimamo mkali.

  Katika siasa na ufuasi hakuna kitu kinachoitwa ukweli, kwa sababu vitu vyote huangaliwa kwa jicho la kisiasa na kwa matakwa yao wahusika, ni kazi ya sheria kuwatumikia watu katika kundi si kazi ya watu kuitumikia sheria, watu mmoja moja wanaitii sheria, siyo kuwa watumwa wa sheria. Katika kuainisha hili Rais wa 16 wa Marekani Bwana Abrahamu Lincolin aliwahi kusema .......the candid citizen must confess that if the policy of tha government upon vital questions affecting the whole people is to be iirevocably fixed by decisions of the supreme court, the instant they are made in ordinary litigation between parties in personal actions the people will have ceased to be their rulers, having to that extent practically resigned their government into the hands of that eminent tribunal. Nor is there in this view any assault upon the court or judges. It is a duty from which they may not shrink to decide cases properly brought before them, and it is no fault of theirs if others seeck to turn their decisions to political purposes".

  Wasiwasi aliouonyesha rais huyo tarehe 4/03/1861 miaka 150 baadaye inatokea kuwa hivyo Arusha na kwa kumuhusisha kiongozi wa upinzani Bungeni inasikitisha sana.We like it or not this kind of things polalize the country.

  Katika mazingira ya kutumikia sheria badala ya kuangalia mazingira yanahusu sheria hiyo katika wakati huo ilimfanya Waziri mkuu Magreth Thatcher awambie makaburu kuwa kuendelea kumshikilia Mandela kwa misingi ya sheria za nchi ambazo zaidi ya nusu ya watu wa nchi wanazikataa ilikuwa taabu kwa serikali ya makaburu kuliko kumwachia.

  Kwa kifupi iwe kuna ukweli kiasi gani na kwa mamlaka gani kumweka kiongozi wa upinzani kwa zaidi ya masaa 48 hakuwezi kuiweka nchi yetu tukufu katika amani tunayo ienzi kwa sababu ni vigumu kuwashaushi maelfu kwa maelfu ya wananchi wanaomuunga mkono Mbowe kuwa Mbowe ameikosea Mahakama. Tujiulize kwa nini Mbowe ana kesi Arusha, ni kesi ya nini, na kwa nini alihusika? Je Mbowe kama mbunge na kiongozi wa upinzani bungeni analindwa na sheria? Je mtu anapojisalimisha polisi bado ni mhalifu wa kufuingwa na kamba hasa anapokuwa anahadhi ya kijamii kama aliyonayo Mbowe kwa sasa na kwamba unaweza ukamfanyia unavyotaka bila kukabilina na nguvu ya wafuasi wake? Mimi sijui nawaachia welevu wachambue lakini pia nawakaribisha wapumbavu waseme yao katika jicho la kisisa

  Kwa misingi ya ufuasi ndio maana huwezi ukamkamata hata Rais mstaafu kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kwa sababu usipoiandaa jamii na nchi unaweza kuigawa nchi na kusababisha mfarakano mkubwa kuliko kawaida. Tunapotekeleza sheria si lazima tufungue milango ya fujo na kama tunahisi hivyo the law of prudence inatufungilia mlango wa kutokea ili kukwepa kufanya maamuzi yanayoweza kuwasha moto wa malamiko na kuzuwa ghasia

  Polisi si watoto wadogo ambao wakiambiwa piga wanapiga, mtemee mate wanamtemea mtu, mtukane wanamtukana mtu, sheria inawapa fursa ya kutathmini hali inayozunguka tukio kabla ya kuchukua hatua, wanaweza kuiepusha nchi hii katika migogoro ya kisiasa kama wataongozwa katika majukumu yao na kusimamia misingi ya haki kuliko misingi ya sheria (they need to be governed by rule of justice and not rule of law. kwa kusimamia sheria haki inapatikana kiasi gani machoni kwa umma? jawabu la jibu hili litawapa umakini Poli wetu

  Kati ya sasa na kesho mahakama ya Arusha na polisi wanayonafasi ya kutoipeleka nchi hii katika hali isiyotarajiwa, fanyeni hivyo kwa kumkumbuka Mungu wetu kuwa anawaona ndani ya mioyo yenu.

  Mungu ibariki Tanzania
  Mungu ibariki Kazi ya Polisi
  Mungu ibariki mahakama ya Arusha
  Mungu wabariki na kuwaongoza wafuasi wa Mbowe ili waone suala hil;i katika jicho ulitakalo wewe
  Kwa mwanga wako, kwa baraka zako watanzania tutafika katika nchi ya ahadi
   
 2. nzehe

  nzehe Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Ni kweli kuna tatizo,checks and balances na kukiukwa kwa haki za binadamu kwa hali ta kutisha
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mhimili wa mahakama unapata madaraka kutoka katika katiba, lakini hiyo checks and balance haipo kwani mhimili wa mahakama si huru. Kiongozi wa mhimili huu ni jaji mkuu; nani anamteua? na anapomteua nani anaweza kuhoji au kubatilisha uteuzi huo? nani anamwapisha? Kama kiongozi wa mhimili wa serikali anamteua kiongozi wa mhimili wa mahakama na kumwapisha bila kuhojiwa na mtu mwingine au mhimili mwingine, uhuru wake utakuwa wapi?
  Ni katika mazingira ya namna hii watu wanapoweza kuhoji uhalali wa kukamatwa kwa mbowe, ukitilia maanani kuwa kesi ya msingi ni ya kisiasa!
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  TUBNAHITAJI katiba mpya sasa!!!!!
   
Loading...