Ni kweli kamanda Wema Sepetu ndiye Mbadala wa Dr. Slaa ndani ya CHADEMA?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,178
41,995
Wasalaam wana jamvi,

Tangu Dr. Slaa aondoke ndani ya CHADEMA ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa bado hajapatikana mbadala wa Dr Slaa. Lakini hata Dr.Mashiji hajaweza kabisa kuvaa viatu vya Dr. Slaa na ni ukweli ulio wazi CHADEMA imepwaya sana na wana CHADEMA walio wengi hawamtaki Dr. Mashiji hata Sumaye na Lowassa wanamuona Mashiji ni mzigo tuu hana mchango wowote na wengi wanasema Mashiji ni chaguo la Mwenyekiti-Mbowe.

Baada ya ujio wa Kamanda Wema Sepetu CHADEMA wanampango wa kumtumia vilivyo na ikiwezekana kumfanya mashuhuri zaidi na muhimu zaidi kama alivyo kuwa Dr W. Slaa.

Ndio maana Wema jana aliandaliwa Mapokezi ya aina yake na tena akapewa heshima ya pekee ya kupokelewa na Mh Kamanda Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu na maandalizi ya mapokezi yake hakuwai kupewa mtu yeyote yule ndani ya chadema hata Ester Bulaya hakuwai kuandaliwa mapokezi ya aina hii japo pamoja na yote hayo Wema Sepetu hakutokea kabisa na hili limemkera sana Waziri Mkuu mstaafu ameliona kama ni dharau pamoja na wadhifa wake bado Wema hakutokea kwani yeye ndio alikuwa amepanga kumpa kadi ya CHADEMA.

Lakini Kamanda Wema Sepetu ameandaliwa mapokezi nchi nzima na atazunguka kila mkoa na kupokelewa kama mgeni mashuhuri ndani ya chama cha makamanda na huu ni mpango wa kumfanya Kamanda Wema mashuhuri zaidi kwani atakuwa ana andaliwa matamko ili na yeye awe anakamatwa kamatwa ili kumuandalia njia ya kutwaa ukatibu mkuu wa CHADEMA.

N:B Kamanda Wema Sepetu ni asset ndani ya CHADEMA kwani ana followers zaidi ya 1million huko instagram.
 
Kwani dhambi iko wapi? Acheni ubaguzi nyie , tuna hoja za msingi za kujadili kuliko upuuzi huu.
 
Hehe ndiyo chama cha democracy, yaan nimegundua wema sepetu ni noma, mpaka Sasa anawaendesha hata kina BAREGU, NA UPROFESA WAO
hakika Wema ni hatari we fikiri hadi waziri mkuu mstaafu anapewa amri ya kwenda kumpokea hahaha
 
ccm mambo ya kipuuzi kama haya ndio wanapenda sana kujadili. Juzi mwenyekiti wa Chadema Mbowe kawapa changamoto uchumi wa nchi unakufa na wananchi tunazidi kuwa na hali ngumu badala ya kujipanga muisaidie nchi.mmebaki majungu na umbeya. bure kabisa
 
Ee mungu tunakuomba uonde laana uliyoweka kwenye vichwa vya hawa UVCCM.Wao ni kukaa Lumumba na kujadili mambo ya Basha wao CHADEMA.Wape hata tone ya akili wajitambue.
 
ccm mambo ya kipuuzi kama haya ndio wanapenda sana kujadili. Juzi mwenyekiti wa Chadema Mbowe kawapa changamoto uchumi wa nchi unakufa na wananchi tunazidi kuwa na hali ngumu badala ya kujipanga muisaidie nchi.mmebaki majungu na umbeya. bure kabisa
Mkuu unataka kila uzi tujadili uchumi? mbona kuna uzi wa hayo mambo? tafadhali ni jibu swali langu..........
 
Hehe ndiyo chama cha democracy, yaan nimegundua wema sepetu ni noma, mpaka Sasa anawaendesha hata kina BAREGU, NA UPROFESA WAO


Umesahau nyie mnaongozwa na Mwenyekiti ambaye Phd yake ina viulizo vya kutosha.Phd ambayo kila mahali inatoa povu na vitisho,Phd ambayo hata lugha mama ya dunia haipandi?In short Phd hewa.
 
Back
Top Bottom