Ni kweli kabisa, miradi ya tshs 340billion haitapunguza foleni dsm, mtemvu kasema kweli bungeni leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli kabisa, miradi ya tshs 340billion haitapunguza foleni dsm, mtemvu kasema kweli bungeni leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Jun 28, 2012.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Akichangia bungeni mbunge mtemvu ameeleza ni kwa jinsi kulikuwepo na mpango mahsusi wa kuondoa foleni uilobuniwa na mhandisi james nyabakari(tanroads manager dsm wakati huo) yeye alianza kwa kulazimisha pesa za ndani zitumike kuongeza njia ya tatu pale mwenge hadi morroco, pia alibuni mpango wa ring road kama vile chuo kikuu chanhanyikeni goba, chuo kikuu msewe hadi kimara, nk , alikuwa amefauliu kupata 20bn na tenda nyingi zilikuwa floated mwaka jana. what happened?

  alivyoingia maghufulu kwenye hiyo wizara jambo la kwanza ni kumhamishia mhandisi huyu mbeya nje ya dsm(ametajwa sana na mh. zuberi bungeni leo), akamrudisha ndamukana yule alyekuwa kabla ya huyu na ambaye alishindwa kabisa ujenzi wa barabara dsm lakini kipenzi cha maghufuli.

  magufuli huyu anaimba kama kasuku juu ya mradi wa world bank wa ujenzi wa lane 6 toka kimara kwenda kivukoni nk, mradi huu hauwezi kuondoa foleni kwa kuwa foleni ziko kwenye trafic nodes(makutano ya barabara kama ubungo, tazara nk.
  mh zuberi amenifurahisha zaidi kwa jinsi alivyolieleza bunge kuwa kenya sasa foleni ni nhistoria, sisi tunaimbiwa litania za sifa za magufuli akitamka majina ya barabara kama kasuku, wakati kenya kimyaa lakini fly over mji mzima wa nairobi miaka miwili tu iliyopita.

  AMKENIACHENI KUWASILIKILIZA KASUKU
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,238
  Likes Received: 12,949
  Trophy Points: 280
  Nimemsikia the guy went to the point. Dsm ni vigumu sana kumaliza foleni kwani mipango ya maendeleo ni kama story
  inabidi viongozi wanaofanya kazi wawepo kwani wengi waongeaji.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Adui namba wani wa taifa hili ni watu kama akina maghufuli ambao wanataka tuamini kuwa umaskini wa taifa hili unatokana na wadokozi kama wala rushwa wa mizani, na wala si wakupwaji wanaopeleka pesa uswisi.
   
 4. combra

  combra Senior Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hivi huyu mtemvu bado yupo duniani,yaani ktk wilaya zote Tz,temeke ndo wilaya inayoongoza kuwa na wananchi ambayo hawataki mabadiliko,tokea wamchague mtemvu hakuna cha maana alicho kifanya.nawasikitia wana temeke kwa kupoteza mda wao wakwenda kupiga kura.mi kwa akili zangu timamu siwezi mpigia kura yangu,bora ni mpigie mbuzi nitamla nyama.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo la DSM sio Magufuli au Mtemvu, kuna watu wana interest na miradi ya aina wanazotaka wao. Mtu mwenye akili timamu atakuwambia njia rahisi na ya kuaminika itayopunguza kama sio kuondoa foleni dar ni Treni ikifuatiwa na hizo ring-roads. Lakini kuna watu wamekazania mabasi yaendeyo kwa kasi! Tena vibasi vyenyewe ni vya TATA! Hii nchi inauguwa uendawazimu.
   
 6. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tatizo la foleni DSM linasababishwa na mambo matano na watawala wetu ambao wanakusanya kodi wanajua ila wanatafuta majibu mepesi kwa maswala magumu
  1. Makutano ya barabara - mfano Tazara, Chang'ombe, Magomeni/Kawawa, Ubungo, Mwenge, Kinondoni/AH Mwinyi nk. Kunahitajika fly over, hata ukijenga Line 10 bado zitakutana na foleni itakuwepo. Mabadiliko ni badala ya magari mawili kuwa mbele kwenye traffic light watu 5 mtakuwa mbele.
  2. Kukosekana kwa vituo vya daladala vilivyojengwa kwa utalaamu wa kisasa mfano mimi nakipenda sana kituo cha daladala cha Morocco/Kawawa rd, vituo vyote vingekuwa vya namna hii foleni ingepungua karibu na vituo vya daladala.
  3. Magari hasa malori yanayofia njiani. Hatuna sheria ya kuyataka yavutwe badala yake naona yanatengenezwa hapo hapo.
  4. Misafara ya viongozi,- wanazuia magari muda mrefu na naona siku hizi kila mtu akijisikia anapiga simu traffic na kupewa piki piki ya kuongezea msafara.
  5. Ukosefu wa alternative roads, yaani kwenda Kibaha lazima upite Kibamba darajani na sioni kama wanafikiri njia mbadala. Sasa hivi kelele zote ni daraja la Kigamboni lakini maeneo ya Kijichi kuna eneo lingine fupi sana ambapo unaweza kujenga daraja kama la Kibamba na watu na magari yakavuka, wala huihitaji kuinua daraja sana kwa vile watu wanakatiza hapo wakati wa kiangazi.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  alichosema mbunge huyu ni kweli....
   
 8. I

  Isoliwaya Senior Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natamani viongozi wa Tanzania wangekuja hapa kenya waone kitu kinaitwa The Thika Super highway ( The Kibaki Superhighway) waje waone jinsi foleni ilivyomalizwa hapa kenya. Kutoka hapa kahawa wendani ninapoishi mpaka nairobi ni km 25 hivi. sasa hivi tunatumia dk 12 kufika mjini mwakajuzi na mwakajana tulikuwa tunakaa masaa 2 mpaka matatu kutoka hapa Kahawa mpaka Nairobi. Huku wakenya wameweza kumaliza foleni watanzania tunashindwa kwanini? nani alituroga? selikari yetu inafanya nini? kwanini akina kikwete na pinda na wajinga wote wa CCM kwanini waliomba kazi wakati walijua kuwa hawaiwezi? kwanini tunawalipa mishahara? Je safari nyingi za nje zenye matumizi makubwa za raisi kikwete zimeleta tija gani kwa serikali yetu.
   
Loading...