msambaa mwenyewe
Member
- Aug 17, 2016
- 69
- 45
MBUNGE "SUGU" AWAJIBIKE KISIASA
Mwaka 1977 Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Peter Said Sioverwa (kwa sasa ni Marehemu) aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais usalama wa Taifa; bila ya kuwasahau waliokuwa Wakuu wa Mikoa wa Mwanza na Shinyanga Mzee Peter Kisumo na Marco Mabawa (Marehemu) walijiuzulu kutokana na vitendo vya kikatili vilivyofanywa na maafisa wa Serikali waliokuwa chini yao katika operesheni ya kuwasaka wanaodaiwa wauaji na wachawi. Kitendo hicho kinachojulikana kama kuchukua dhamana ya kuwajibika kisiasa.
Leo hii tunaona Dereva wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) aitwaye Gabriel Andrew (43) akimgonga Mtoto kwenye eneo la kivuko cha waenda miguu (Zebra) na hivyo kumsababishia umauti. Damu ya mtoto Recho Lutumo (14) asiye na hatia imemwagika, uhai umepotea.
Kama ilivyotokea kwa Mzee Mwinyi kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kutokana na makosa ya wasaidizi wake, inabidi naye "Sugu" awajibike kisiasa kwa kujiuzulu ubunge wake kutokana na makosa yaliyofanywa na dereva wake Gabriel yaliyopelekea umauti wa Mtoto Recho kutokana na kutokuheshimu sheria za barabarani. Ajipime mwenyewe, naomba kuwasilisha!