NI KWELI INAMPASA SUGU AWAJIBIKE KWA KOSA LA DEREVA WAKE ????

Aug 17, 2016
69
125
MBUNGE "SUGU" AWAJIBIKE KISIASA

Mwaka 1977 Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Peter Said Sioverwa (kwa sasa ni Marehemu) aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais usalama wa Taifa; bila ya kuwasahau waliokuwa Wakuu wa Mikoa wa Mwanza na Shinyanga Mzee Peter Kisumo na Marco Mabawa (Marehemu) walijiuzulu kutokana na vitendo vya kikatili vilivyofanywa na maafisa wa Serikali waliokuwa chini yao katika operesheni ya kuwasaka wanaodaiwa wauaji na wachawi. Kitendo hicho kinachojulikana kama kuchukua dhamana ya kuwajibika kisiasa.

Leo hii tunaona Dereva wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) aitwaye Gabriel Andrew (43) akimgonga Mtoto kwenye eneo la kivuko cha waenda miguu (Zebra) na hivyo kumsababishia umauti. Damu ya mtoto Recho Lutumo (14) asiye na hatia imemwagika, uhai umepotea.

Kama ilivyotokea kwa Mzee Mwinyi kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kutokana na makosa ya wasaidizi wake, inabidi naye "Sugu" awajibike kisiasa kwa kujiuzulu ubunge wake kutokana na makosa yaliyofanywa na dereva wake Gabriel yaliyopelekea umauti wa Mtoto Recho kutokana na kutokuheshimu sheria za barabarani. Ajipime mwenyewe, naomba kuwasilisha!
 
hebu tuijadili hii nimeikuta sehemu
 
kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
3,338
2,000

Sasa atawajibika Vp kwa sababu hata gar lake lilitaka break . hapo ni mambo ya kisheria tu na kulipa fidia bas
 
CCA

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
397
250
Sidhani kama kwa dereva aliehitimu na anaemwendesha mh atashindwa kufuata sheria ikiwemo kuwaheshimu pedestrians labda gari lilikua na hitilafu yakiufundi
 
R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,162
2,000
Mkuu kwa hiyo mifano uliyoitoa kwa hii ajali ya Sugu haiviendani kabisa.

Katika mifano yako inaonekana watu walikaa kwenye kikao na kuwa na maamuzi ya jambo fulani ila wale walitumwa kulitekeleza hawakuwa waadilifu tukirudi kwenye kesi ya dereva wa sugu hakukuwa na mpango wowote uliomuhusisha marehemu na hiyo ajali kabla ya hapo. Kwa maana hawakukaa kikao kusema leo twende tukapate ajali maeneo fulani halafu ije vice versa .

Sioni sababu ya Sugu kuwajibika kisiasa kweny hiyo ajali ila dereva ana kila sababu ya kupelekwa mahakamani angalau kwa maelezo ya Sugu mwenyewe ni kuwa gari ili feli breki. So hatuwezi kuhukumu bila kupata hukumu kutoka mahakani.

Mwisho ninatoa pole kwa wafiwa na Allah awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.
 
Mpira wa kona

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
350
500
Ahaaaa ccm bwana makosa ya kuwajibika yafanywayo Na mawaziri hamsemi hebu tujikumbushe
1.Kumeokotwa maiti saba MTO Ruvu mpaka Leo hakuna taarifa zozote Waziri mwenye dhamana amewajibika?
2. Mauaji ya wakulima Na wafugaji mvomero
3. Faru John Waziri MKUU anahangaika Kwa uzembe au ufisadi wa watu Waziri au mkurugenzi wa wanyamapori kawajibika?
4.Wafanyakazi hewa Waziri mwenye dhamana kawajibika?
Acheni uongo wenu matukio makubwa hamsemi .Ingekuwa Dereva akisababisha ajali mwenye gari anawajibika ingekuwa balaa .Mbona madereva wa
mawaziri wanapata ajali
Mawaziri hawawajibiki?
 
upendodaima

JF-Expert Member
May 23, 2013
4,031

Chenge aliua kabisa lakini yupo wapi na anafanya nini sasa hivi?hawa watu akili zao wanazijua wenyewe.

R.I.P Recho.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom