Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,202
- 42,061
Ni kweli hizi chanjo zilizo letwa wiki tatu zilizopita hazina muda wa kuharibika?
Kati ya mambo ambayo yamewashinda kabisa wizara ya afya kwenye hili chanjo ya COVID ni kuweza kutoa elimu sahihi kwa wanchi kuhusu hii chanjo na katika hili wizara imekuwa ikikimbia maswali ya watu kwa kudhani kila anayeuliza maswali basi anapinga chanjo.
Suala la muda wa kutumika kwa chanjo husika baada ya kuletwa limekuwa likiulizwa sana japo halijawai kupata majibu yake kwani tumekuwa tukiona nchi zingine wakimwaga baadhi ya chanjo baada ya kuisha muda wake wa kutumika.
Hivi ni kweli Johnson & Johnson haina expire date?
Na kama ina expire date au muda wa kuisha matumizi kwanini haiwekwi wazi?
Ni kweli hizi chanjo million moja hata zikikaa hadi mwakani bado zitakuwa ni safi kwa matumizi ya binadamu?