Ni kweli, historia ya Tanzania ni muhimu ikafundishwa

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Naungana na Rais wetu mpendwa kuhusu historia ya nchi yetu kupewa umuhimu unaostahili mashuleni na vyuoni kwani kwa kiasi fulani nadhani itasaidia kuliweka taifa katika mstari hasa katika nyanja sa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Nasema hivyo kwa sababu kizazi cha sasa kinapoteza dira iliyochorwa na historia ya nchi hii katika nyamja hizo.

Kisiasa mathalani, imefika wakati watu wameanza kusahau ni kwa nini tulipigania uhuru na kuondoa ukoloni.

Wamesahau ni kwa nini tuliamua kuingia kwenye demokrasia ya siasa za vyama vingi.

Watu wameanza kusahau hata ya juzi tu kwamba iifika mahala wengi walikuwa wameacha kununua na kuuza nguo za rangi ya kijani, achilia mbali kuzivaa hadharani.

Watu wameanza pia kusahau kuwa bila vuuvugu la siasa za vyama vingi pengine hata Magufuli wetu asingekuwa Rais.Mambo ni mengi ya kukumbuka kwenye historia ya nchi hii kisiasa ila kwa mkutadha wa bandiko hili itoshe kusema tu kwamba, tukifahamu vizuri historia ya nchi hii, pengine tutabadilika na kutengeneza mifumo mizuri zaidi ya namna ya kujitawala na kuendesha siasa safi zitakazotuletea maendeleo ya kweli.

Kiuchumi, watu wamesahau (hata wengine hawafahamu) kwamba kuna kipindi ilikuwa ukikutwa na mche wa sabuni kwenye basi unakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.

Wanasahau kwamba safari ya kutoka Dar mpaka Mtwara kwa basi au gari ilikuwa inamchukua mtu hata wiki akiwa safarini.

Watu wengi hawajui kama zamani tv ilikuwa kwa Mwalimu na Sir George pekee hapa nchini.

Yote hayo na mengine mengi yakifundishwa ndio tutaona umuhimu wa shughuli za ujenzi wa miundombinu tunayoihangaikia sasa.

Pengine watu wameanza kutanguliza maslahi yao na watu wao kwenye nasaba zao za kisiasa na kijamii na kusahau kwamba amani tuliyokuwa nayo inatakiwa iendelee kuwepo mpaka vizazi vijavyo viifaidi.

Watu wanadhani kujilimbikizia mali na madaraka ndio muhimu kuliko kukudumisha amani kwa kufuata katiba na sheria za nchi.

Wanasahau kwamba mali na madaraka havina maana endapo amani itatoweka.

Wanasahau kwamba amani ni zao la haki na uhuru. Pia vurugu ni zao la uonevu na dhuluma.

Pengine historia ikifundishwa mashuleni, kizazi hiki na kijacho kitaona umuhimu wa kuwa na sera nzuri za kiuchumi zinnazolenga kuweka usawa katika kutumia fursa za kiuchumi zilizopo nchini.

Aidha,jamii yetu imefika mahala inaona hata ibada sio muhimu kuliko ushirikina.

Watu wanaona ni bora kupata mkono wa albino kuliko kukosa ubunge!

Ni mengi yanayoanza kuifanya jamii ikengeuke kiasi hiki.

Lakini pengine historia itatuhukumu,hivyo ni muhimu kuijua kabla haijatuhukumu.

Tafakari.
 
Aliyekudanganya kuwa historia ya Tanzania haifundishwi mashuleni/vyuoni ni nani?
 
Mimi nikiwa niliekulia miaka ya Themanini nakuelewa kwa mengi uloyataja,lakini tukumbuke tu zama zimebadirika sana.Namaanisha kuwa muono(perspective) ya wengi imebadirika,hii imebadirisha jinsi tunavyochangia siasa,tunavyowasiliana,utamaduni na mengi mengineyo.

Miaka ya zamani ukiambiwa kaa unakaa,ukiambiwa yule mhujumu uchumi basi unamchukia,kwa sasa watu wanauliza kwa nini,au wanataka ushahid.Hiyo siasa unayotaka ifundishwe pia kuna baadhi ya watu wanaona ina matobo,maana yake inakosa uhalisia.Swali langu wakifundisha siasa wako tayari kuulizwa maswali magumu au kukosolewa?

Kama nimekusoma vizuri,unamaanisha watu wakijua history ya tulipotoka wata ridhiswa au kuunga mkono tulipofikia,lakini pia kuna wanaofikiri tumecheleweshwa na tungefika mbali je mpo tayari kwa mtazamo wao?.

Mi si wa zamani sana lakini nakumbuka maduka ya ushirika,chipukizi,sabuni za mche nk na nimeona mji kama wa Dar es salaam nilipozaliwa na kukulia ukibadirika,vitu kama flyover havini 'impress'sana ikiwa umaskini umezidi.

Nimeshuhudia wasemaji wa upinzani kama Tindulissu,Lema,Mbowe,Zitto kabwe ambao ingawa sina chama,na niliamini magufuri angeshinda,hawa watu wakipotezwa kutoka ukumbi wa siasa.Kutokuwepo kwao kutaifanya nchi kutoskia mawazo mbadala ingawa vyama vipo lkini kusema bungeni kuna uzito tofauti.Wapo tayari upande huu wa history kuandikwa?

Kuna mengi yatafukuliwa ukitaka history ifundishwe na kwa mwenendo wa sasa,sidhani kama uzalendo utapatikana kwa kuandika mazuri ya upande mmoja wakati kuna mamilioni ya watanzania wanajua uzuri wa upande mwengine pia.
 
Back
Top Bottom