Ni kweli haya yapo tutawaeleza nini watoto wetu miaka ijayo

Brodre

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,351
1,372
Tutazungumza watasema ni upepo tu na utapita.

1. Wanakaa kwenye ma estate na ma mansion, wanafikia five stars hotels watafamu lini kuwa kuna maisha ya watu wa chini wanaolala kwenye nyumba za tope?

2. Barabara za rami zipo hadi chooni, 24/7 wapo angani lini watafahamu kuna barabara ya vumbi?

3. watoto wao wanasoma UK,Canada, USA lini watafahamu kuna St. Kayumba schools hazina madawati wala waalimu?

4. wana umeme majumbani kwao muda wote eti wanakaa kwenye special lines ambazo ni marachache umeme kukatika pia wanastandby generators lini watajua kuwa kuna mgao wa umeme?

5. Wana maccounts uswizi ya kuwalisha wao na watoto wwao na vijukuu vyao miaka nenda rudi lini watafahamu kuna watanzania wanakosa hata 200 ya unga?

6.watoto wao wanatembelea gari za Anasa wengine za serikali lini watafahamu kuwa Kuna wasiojiweza wanaohitaji hata baiskeli za gurudumu tatu?

7. Wanatibiwa India na UK lini watafahamu kuwa kuna hospital hazina wauguzi?

8. Magari yanassimamishwa wakiwa wanapita kwa raha zao lini watajua kwamba kuna foleni za gari waongeze barabara au watafute njia mbadala?

TUSIDANGANYANE: Hao viongozi wataishia kupiga kelele tutawajengea barabara,mara mgao wa umeme utaisha, ohh tutainua mfumo wa elimu mara hii mara lile lakini kutokana na sababu ya kwamba hawa experience tunayo experience sisi watu wa hali ya chini hata siku moja hawawezi leta maendeleo zaidi wataishia kuendelea kutunyonya na kuimagine kuwa tunaishi kama wao yani kwa kifupi wanaconclude kwamba wote tunaishi kama wao wanavoishi na hakuna haja ya maendeleo.

We ushawahi ona wapi mtu anakua kiongozi miaka 40, lini ataonja shida ndio maana wakiingia huko hawataki kutoka kwa sababu wanajua nini kiko juu huko. tubadilishane nao hata kwa muda wa saa 3 waje huku twende huko uone kama wakirudi hawatabadilisha maisha ya watu.

sio siri kuna vitu vinakera sana ila hata tukisema tuliowapa dhamana ya kututetea nao washajisahau wakifika huko wanakuwa na kale ka usemi "For God and for my Stomach" Badala ya "For God and for my people"

Vizazi vijavyo mtatusamehe kwa haya yafuatayo;

  • kushindwa kuwaandalia Tanzania ambayo mtaishi kwa raha.
  • Kushindwa kuzuia vitendo vya rushwa
  • Kushindwa kukemea maovu yanayofanyanywa na viongozi.
  • Kushindwa kuzuia unyonyaji wanaofanya wawekezaji
​
Mtusamehe tu walisema maisha bora kwa kila Mtanzania, tukawapa kura lakini matokeo yake yakawa maisha duni kwa kila Mtanzania.

As long as hayo hapo juu yapo tutaendelea kuwa masikini daima
Vizazi vijavyo mtatusamehe kwa kushindwa kuwa
 
Natamani niyachukue hayo maneno niyatengenezee bango kubwa halafu niliweke sehenu ya wazi kila mtanzania ayasome.....ndio CCM hiyo, tukisema sana wanatuambia tuna wivu wa kike.
 
Natamani niyachukue hayo maneno niyatengenezee bango kubwa halafu niliweke sehenu ya wazi kila mtanzania ayasome.....ndio CCM hiyo, tukisema sana wanatuambia tuna wivu wa kike.

Inaumiza sana basi tu
 
Mkuu, wenzetu hawawazi shida, dhiki na matatizo mbali mbali yanayotuandama kila uchao maana wao na vizazi vyao hayawahusu wala kuwagusa hata kidogo. Wewe, mimi, watoto wetu ndio tunaonja karaha za foleni, miundombinu mibovu, huduma mbovu mahospitalini, bora elimu na sio elimu bora na mengine meeeeeeeeeeeeengi.

Wenzako kwa sasa wako kwenye mikakati ya kuhakikisha wanashinda tena ubunge (ili waje wawe waziri), au kijiandaa kugombea kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais. Matatizo ya watanzania sio agenda muhimu kwao.
Kazi ni kwetu kuhakikisha hatuwapi nafasi yakuendelea kutukandamiza na kudunisha maisha yetu na ya watoto wetu.
It can be done..., play your part.

kweli mkuu ni sisi wananchi ndo tutaandaa taifa tunalolihitaji si viongozi
 
Well spoken, ...kwa miaka 20 - 40 uyo ni mtawala na si kiongozi, na hapo ndipo mambo huanza kufanywa kwa "UZOEFU"(tena uzoefu mbaya) yaani ni kama routine vile.
 
sheria itungwe sasa ya kuanza kudhibiti muda wa kukaa madarakani ili yasijetokea kama ya Misri na Libya sababu lini tutapata mambo mapya kama wale waliokuapi zamani hawataki kuachia vijana wabadilishe nchi wataendelea kuendesha nchi kizamani sababu hawajui kama dunia inabadilika sijui hizo safari zao za nje wanafataga nini kama hat huko hawajifunzi
 
Nakubaliana nawe mkuu lakini napenda kutoa angalizo kuhusu kuwaachia vijana. Nionavyo mimi sasa hivi hawa jamaa wameshasoma upepo wanachokifanya sasa hivi ni kurithisha watoto wao madaraka unaweza kuona hatari iliyopo kwa nchi kumilikiwa kiuongozi na familia moja mfn familia kuanzia baba, mama na mtoto wako ngazi za maamuzi kutoka ngazi ya serikali hadi chama. Watanzania inabidi tuwe makini na hira hizi maana tutakuwa na tabaka la watawala na watawaliwa na hivyo kitu kinachoitwa maendeleo itakuwa ni ndoto kwetu.
 
Mkuu Dreson3 umesema kweli na naunga mkono hoja yako. Na kw asasa elewa kuwa hatuna viongozi ila tuna watawala ambao kutwa wanapambana kuhakikisha wao na familia zao wanapata nini kw aajili ya maisha yao na ya baadae ya familia zao na sio wale wanaowatawala watafaidika nini kwenye utawala wao.
 
Last edited by a moderator:
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom