Ni kweli Hamad Rashid Kapangwa Kuivuruga CUF? Muulize sasa LIVE ON Star TV

nimechelewa ila nilitamani kumuuliza maswali huyo msalitiwa Upinzani, wameshaanza kulipwa hapa hapa
 
muulize ni kwanini alikuwa mpinzani ndani ya upinzani? anawezaje kutushawishi kuwa yeye si mtu anayetumiwa na ccm kuua upinzani bungeni? mfano ni mchango wake anapokua bungeni dhidi ya chadema
 
Muulize Hamad Rashid ni kweli Jimboni kwake ameshindwa kuanzisha shule ya sekondari hata moja zilizopo ni zile tangu mkoloni?

Pili kwanini hakai jimboni kwake maisha yake yapo Dar? je , haoni kwamba hawatendei haki wapiga kura wake?

Tatu ni kweli alikuwa ameshashindwa kura za maoni za jimboni kwake Seif ndiye aliyemuokoa? Nne Hanatashawishi vipi kusema democrasia haijatumika na wakati kati ya wajumbe 25 wa bara 23 walihafiki kufukuzwa kwake naye anadai Bara wanampenda?

Mwisho ni kweli kwamba kuendelea kuwa katika uongozi wa CUF kwa muda mrefu Seif alijitahidi kuwashawishi wanachama wakukubali wakati wengi walikuwa hawana imani nawe kwa vile mke wako ni Afisa wa usalama wa taifa?

Masuala mujarabu kabisaa.

Na kwa kuongezea baada ya swala ya ijumaa watu kule WAWI leo wanakula halua kushangilia kufukuzwa kwake.

 
Hayo ndo maswali ya waandishi wa tz. Yaani hivi vyuo ni vya kuchomwa moto vyote. Utakuta mpiga desa ndo anabaki kuwa lecturer. Ivi swali la heading yako(japo sijasoma ulichoandika ndani) ukimuuliza HR, unategemea atakujibu nini? Jana pia saa 3 usiku TBC1,nilikereka na kile kipindi maalumu ya wanajeshi kupandisha mwenge K/njaro, yani mtu anauliza maswali ya kiuoga ambayo, hata mtoto wa darasa la 2c anajibu.

Wewe ulitaka waulize maswali watakayoshindwa kujibu?
 
Maswali mengi mliouliza hata kama ni kweli yanayosemwa sidhani hata kama kichaa hawezi kusema ndiyo natumika na ccm ama pinda anahusika na tunawajua wanasiasa walivyo waongo na wanafiki kwahiyo hata iweje msifikiri mtapata majibu sahihi hata kidogo
 
Yayha

huyu bwana si mala ya kwanza kufukuzwa ktk vyama.hii ni mala ya pili kama sikosei akitokea ccm na akawa mwanzilishi wa Cuf,

je haoni kuwa yeye ndiye mwenye matatizo kwani hii si mala yake ya kwanza kufukuzwa?

na kama alikuwa ana nia ya kugombea huo ukatibu mkuu kwanini hakutaka kufuata taratibu za kichama kama zilivyo ktk katiba yao ya cuf na yeye kuamua kujitangaza bila hata kuwa na mawasiliano na chama chake?
 
Yahya

Kwanini huyu bwana alichukuwa jukumu la kukidanganya chama chake pale alipo pewa nafasi ya kukusanya michango kwa wabunge wa cuf walio bungeni dodoma na badala yake akadai kuwa mshahara wanaopata wabunge ni mdogo na hawawezi kuchangia?

Na kwanini anakuwa hana imani na katibu wake,kwani mala nyingi amesikika akisema kuwa kwa kuwa hamadi ni makamu wa raisi zanzibar anatakiwa mambo ya chama awaachie wengine haoni kuwa kumwondoa ktk hiyo nafasi hamadi ni kumwondoa pia ktk hiyo nafasi ya umakamu wa raisi zanzibar?

safi sana,kweli jf ni chanzo kizuri sana cha habari
 
Back
Top Bottom