Ni kweli Hamad Rashid Kapangwa Kuivuruga CUF? Muulize sasa LIVE ON Star TV

Yahaya!
muulize HR, anajiskiaje sasa mbele ya Chadema baada ya yeye na wenzake akiwamo Kafulila kuvunja kanuni ya bunge ya kuitambua kambi rasmi ya upinzani wakishirikiana na wabunge wa CCM na spika?
 
1)muulize yeye ana msimamo gani kuhusu muungano wa sasa?
2)kwanini CUF inahusishwa na uzanzibar na udini km ilivyo CDM inavyohusishwa na ukristo na ubara? Je anaamini kwamba hizo ni propaganda za CCM?
3)ana msimamo gani kuhusu rais wa 2015? anashauri atoke upande upi wa tanzania (bara na kisiwani) na awe na sifa zipi za kuongoza nchi yetu.
 
Tumerejea hewani tulipata tatizo la Umeme kutokana na kulipuka ghafla kwa transforma ya Eneo la Ilemela ambalo liliathiri saketi yetu ya automated generator, replacement has made quickly with deligent technical crew. We are onair
 
Mtatiro keshanukuliwa na magazeti kuwa "Kuanzia sasa Hamad Rashid si mwakilishi wa wananchi wa Wawi kupitia CUF, akitaka kuendelea kuwa Mbunge anapaswa kuwa mwakilishi kupitia mahakamani"

So HR anajua yeye ni mbunge tu kupitia mahakama, kwani hata CUF nao wanajua wamekiuka kumfukuza wakati kuna zuio la mahakama.
 
namuunga mkono HR. Ana uungwaji mkono na watu wwenye nguvu ya hoja. Nawahakikishieni kuwa cuf watajutia hili kwa ubinafsi wao. Iko wapi ile dhana ya mizani kwenye bendera ya cuf?
 
Paul Mabuga unachakachua maswali yetu. Unavyoyasoma hayaeleweki, hayawezi kujibiwa, last time Yahya alikuwa anayasoma kama yalivyo na tukapata majibu yake.
 
HR anasema kwamba kikao kilichomfukuza hakikuwa halali kwa sababu kulikua na zuio (Injunction) ni kwanini alikwenda kujitetea ilihali akijua ni batili ab initio?
 
Hamad anasema Maalim na Jussa walienda kufanya muafaka bila baraka za chama cha Cuf.
 
Paul Mabuga unachakachua maswali yetu. Unavyoyasoma hayaeleweki, hayawezi kujibiwa, last time Yahya alikuwa anayasoma kama yalivyo na tukapata majibu yake.

aisee hata mimi nimeona jinsi anavyochakachua maswali, halafu anayasoma km kalazimishwa vile, loh! huyu nilimtoa thamani siku ile alivyokuwa anamuuliza maswali Dr.slaa na upande wa pili kukiwa na msomali, aisee...
 
"The mkerewe" wewe ni Julius Mtatiro? Maana hoja ulizochangia ndizo ulizoongea Channel Ten. Pia inaonyesha wazi kuna maandalizi yamefanyika kuhusu watu wa kupiga simu n.k.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa Maalim Seif anawezaje kuwa Makamu wa Rais na wakati huohuo Katibu Mkuu wa Chama. Huo ni uroho wa madaraka na ubinafsi uliopitiliza. Aidha hakuna demekrasia katika vyama vingi vya upinzani ambavyo ndio watanzania walivitegemea.

Nampongeza Mh. Hamad Rashid kwa Uthubutu wa kujaribu kukinusuru chama. Lakini nimkumbusha Mh Hamad Rashid kuwa kwa sasa CUF ni CCM - B,
 
Anasema kuna milion 500 hazijulikani zimepotelea wapi,na Mtatiro kala milion 128..
 
HR ni mnafiki huyu nakumbuka waloyafanya wakiwa na Kafulila lakn Mungu mwema amewazabua hapahapa na watoto wenu wakiona
 
Suala dogo tu la kumuuliza. Kwanini baada ya msukosuko wa kutimuliwa chama kwanini usiende kwa wapiga kura wako WAWI kupata nasaha na barka zao unakuwa unakimbilia bara na kuwakimbia wapiga kura wako?
 
HR anasema kwamba kikao kilichomfukuza hakikuwa halali kwa sababu kulikua na zuio (Injunction) ni kwanini alikwenda kujitetea ilihali akijua ni batili ab initio?

Hapo ndipo alipojichanganya.

Na zuio hilo la mahakama alilichukulia kwenye mahakama kuu ya Tanzania na sio ile ya Zanzibar. Alishindwa elewa kuwa Zanzibar na Tz wameungana katika mahakama ya Rufaa na sio mahakama za chini ya hapo.

Ili injuction yake ifanikiwe na kuweza kutumika Zanzibar alitakiwa aende kuisajili katika mahakama kuu ya Zanzibar ndio ingeweza kutumika.

Hakika wanasharia wake wamemwingiza choo cha kike

 
Swali: Kama alijua kikao kile hakikuwa halali kwani kilikuwa kinakiuka amri ya mahakama, mbona alihudhuria?
 
Muulize Hamad Rashid ni kweli Jimboni kwake ameshindwa kuanzisha shule ya sekondari hata moja zilizopo ni zile tangu mkoloni?

Pili kwanini hakai jimboni kwake maisha yake yapo Dar? je , haoni kwamba hawatendei haki wapiga kura wake?

Tatu ni kweli alikuwa ameshashindwa kura za maoni za jimboni kwake Seif ndiye aliyemuokoa? Nne Hanatashawishi vipi kusema democrasia haijatumika na wakati kati ya wajumbe 25 wa bara 23 walihafiki kufukuzwa kwake naye anadai Bara wanampenda?

Mwisho ni kweli kwamba kuendelea kuwa katika uongozi wa CUF kwa muda mrefu Seif alijitahidi kuwashawishi wanachama wakukubali wakati wengi walikuwa hawana imani nawe kwa vile mke wako ni Afisa wa usalama wa taifa?
 
Journalism is so broad inawezekana unafahamu kijieneo tu Mkuu take time usome vema , Tazama Kipindi... ya TBC wapelekee TBC hatuwezi kuwasemea
Tatizo watu humu ndani wanajidai wanajua kila kitu! Ni bora ukauliza kama hujaelewa heading kuliko kuanza kuropoka!
 
Back
Top Bottom