Ni kweli Hamad Rashid Kapangwa Kuivuruga CUF? Muulize sasa LIVE ON Star TV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Hamad Rashid Kapangwa Kuivuruga CUF? Muulize sasa LIVE ON Star TV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Jan 6, 2012.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mjadala juu ya hali tete ya sintofahamu ndani ya Chama cha Wananchi CUF unachukua sura mpya. Mtatiro yupo TV nyingine na version ya upande mmoja wa Sarafu na soon HAMAD Rashid atakuwa Star TV.

  Nipo Online kumoderate maoni na maswali ya wanaJF

  Karibuni katika mjadala
   
 2. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Atakuja kujuta
   
 3. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pole sana bwana Hamad kwani hiyo ndiyo misukosuko ya kisiasa.Ningependa kujua baada ya Bwana Hamad kuvuliwa uanachama,je ana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa au ataanzisha chama chake kama ilivyokwishasikika hapo awali?
   
 4. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ASANTE MKUU
  SWALI

  • Anajisikiaje kufukuzwa CUF
  • kwanini anasema yeye bado ni CUF ili hali ana mpango kuanzisha chama chake
  • je, mahakama ikiamuru aendelee /mwanachama kuwa mbunge atafayaje
   
 5. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Hayo ndo maswali ya waandishi wa tz. Yaani hivi vyuo ni vya kuchomwa moto vyote. Utakuta mpiga desa ndo anabaki kuwa lecturer. Ivi swali la heading yako(japo sijasoma ulichoandika ndani) ukimuuliza HR, unategemea atakujibu nini? Jana pia saa 3 usiku TBC1,nilikereka na kile kipindi maalumu ya wanajeshi kupandisha mwenge K/njaro, yani mtu anauliza maswali ya kiuoga ambayo, hata mtoto wa darasa la 2c anajibu.
   
 6. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  HR amehusishwa sana na Mizengo Pinda ktk kukiua chama! Je, nini ni kauli yake ktk hili... lakin Jussa amemuhusisha na ugomvi wa kukataa kukomkopea bilion kadhaa kwa Rostam Aziz. Je, haya ya ukweli au ni kumchafua?

  Mtatiro katika maongezi yake amesema HR n Mbunge wa MAHAKAMA YA JMT na si CUF, Msimamo wa HR ni nin?Mwsho,je ana mpango wa kukutana na Maalim Seif na kuomba radhi?

  Asante
   
 7. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Journalism is so broad inawezekana unafahamu kijieneo tu Mkuu take time usome vema , Tazama Kipindi... ya TBC wapelekee TBC hatuwezi kuwasemea
   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Swali tunajua kuanzisha chama inawezekana lakini kuna vikwazo vingi tumeona ccj/cck kushindwa kusajiliwa sasa je kama ikishindikana kuanzisha chama atafanya nini? anatarajia kujiunga na chama gani? Na kwann anafikiria kujiunga chama hicho?
   
 9. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nini kilimsukuma kimtetea Maalim Seif pale alipotihumiwa Mwigulu Nchemba kuwa Maalim alisababisha waandamanaji Z'bar kufa baada ya kupata Madaraka na kawaacha na sasa ananawiri na Kukata Ndevu, kipi kilimsukuma kuipinga Kauli hiyo na baadae amekuwa yeye (Hamad Rashid )arudia kauli kama hizo dhidi ya Seif, ni muda upi alikuwa mwongo, sasa au Zamani?
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hi Yahya,

  Hamad Rashid anazungumziaje tuhuma za kwamba alidanganya mapato ya wabunge wa CUF ili watoe michango kidogo kwenye chama baada ya wabunge hao kutakiwa kuchangia asilimia fulani ya mapato yao kwenye chama?
   
 11. Y

  Yassin Madiwa Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je ni nini hatima yako ya kisiasa bwana HR? Je unaonaje ukajiunga na CHADEMA na kuwa mpinzani wa kweli na hata kuleta mageuzi ya Kiasiasa Zanzibar badala ya kua CCM B. Na kama mpango wako ni kuanzisha chama kingine huoni itakuchukua muda na punde tu baada ya jimbo lako la uchaguzi kuitangazwa wazi utakosa fulsa ya kugombea tena?

  Ahsante Yassin Madiwa Lushoto Tanga
   
 12. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Namuuliza HR, kwanini amekuwa kwenye migogoro ya kiuongozi kwa muda sasa? Mkumbushie jinsi alivyoli present issue ya kambi rasmi ya upinzani, na sasa ndani ya chama chake. Je hivyo si viasharia vya tamaa ya madaraka iliyovuka mipaka?
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Yahya:
  Kwa nini Mh Hamad Rashid alishiriki kupitisha sheria ya uundwaji wa tume ya katiba mpya akijua wazi sheria hiyo ina mapungufu? haoni kwamba sheria hiyo itapelekea kuundwa kwa katiba mbovu ambayo itaendelea kuruhusu vyama kuwa na nguvu ya kuvua watu uanachama kadiri wanavyotaka na hivyo kuwaondolea haki ya kuongoza na kuongozwa/ kuchagua na kuchaguliwa?
   
 14. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Anasemaje kuhusu huu umangimeza uliopo kwenye vyama ambao unavifanya kuwa mali ya watu binafsi! Kwamba mnapotofautiana hoja suluhisho ni kutimuana
   
 15. Y

  Yassin Madiwa Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini uende mahakamani kupigangal kufukuzwa usijipange kwenda kugombea jimbo lako kwa tiketi ya CDM na ukatetea kiti chako cha ubunge ukichukulia kwamba wapiga kura wako wakuhitaji uwawakilishe bungeni?
   
 16. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yahaya muulize Hamadai Rashidi hivi:

  Jana amenukuliwa na vyombo vya habari akisema yeye ni mwanachama hai wa CUF na bado ni mbunge wa Wawi; swali kama kweli yeye ni mwanachama mwenye nia njema na chama chake kwa nini anaendeleza vitendo vya hujuma, vya kuboma chama chake? Mfano, kukusanya kadi za wanachama wengeni anaodai wanataka kuhama nae? Pili, kuzungumzia kuhama chama au kuanzisha chama kingine wakati ni mwanachama wa CUF?

  PILI: Hiyo strategy yake, ya kutumia vyombo vya habari, ambavyo vingine tunavijua kamwe haviandiki mazuri yeyote ya CUF, inasaidiaje kukijenga chama?
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Yahya ninafuatilia mjadala huu wa Star tv nikiwa Lindi. Kusema ukweli Hamad na Jabir kuna kitu wanakifahamu lakini hawataki kukisema. Anaewahoji ajikite kwenye maswali ya kichokonozi zaidi ili tunaofuatilia sakata hili tuje tuelewe msingi mkuu wa huu mgogoro
   
 18. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swali kwa hamad rashid

  1.Akiwa kiongozi wa upinzani bungeni 2005-2010 haoni kama alishindwa kuchagiza wabunge wa CUF wawe na hoja za maana na kuifanya CUF iliyokuwa na wabunge wengi relative to CDM ionekane haina makali??????????

  2.Kifo/kufifia kwa CUF bara kumechangiwa pamoja na mambo mengine tabia ya CUF kutokuwa/kutokusimamia hoja za kitaifa HR akiwa kiongozi wa hao wabunge kivipi asilaumiwe na wana CUF kwa hili.

  3.Ni kivipi HR ameweza mswaada wa KATIBA ambao wazanzibar wengi wanaonekana kutoutaka huu mswaada na hasa kipengele cha muungano.

  4.Kama HR alikuwa kiongozi wa upinzani kwa miaka mitano na bado alishindwa kuwa na mvuto/kuwa mwana harakati anayekubalika bara na au visiwani leo hii akianzisha chama anategemea kipate wafuasi (wafuasi wenye uelewa mzuri na sio wafuasi waliojaa chuki na Seif AMBAO WITH TIME WATAYEYUKA KWA KUZIDIWA HOJA?)
   
 19. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sasa mbona mmekata matangazo kwa sie tunaotumia ving'amuzi vya strong?
   
 20. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  vipi mbona star tv mmetoweka hewani ghafla'au ccm wanawafanyia?
   
Loading...