Ni Kweli Hakuna Mwenye Ushahidi Kuhusu Tuhuma Za Ufisadi Kwa Kuwa Walishamaliza Mwaka Toka 2008

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
NI KWELI HAKUNA MWENYE USHAHIDI KUHUSU UFISADI KWA KUWA WALISHAMALIZA MWAKA 2008

HAKI NA MADARAKA YA BUNGE.

Kwa mujibu wa lbara ya 100(1) ya Katiba ya Nchi na kwa mujibu wa Kifungu cha 5 Cha Sheria ya Kinga,Haki na Madaraka ya Bunge,uamuzi wa Bunge hauwezi kuhojiwa mahakamani. Ibara ya A100(1) na ya 63(2) na kifungu hicho cha Sheria ya Kinga ,Haki na Madaraka ya Bunge, vinazuia kufunguliwa kwa mashauri ya madai au ya jinai kupinga uamuzi wa Bunge.

Nimenza na maelezo hayo ikiwa ni kutaka kushare na Watanzania wenzangu ambao ni maamuma wa sheria na tusio kuwa na ufahamu wa ndani kabisa kihusu mgawawanyo wa nguvu za uendeshaji wa Nchi. Kuna maombi yalitolewa na Mh Lowasa kuwa "MWENYE USHAHIDI KUHUSU UFISADI WAKE ALETE". Mfano Kupitia gazeti la Mwananchi ya tarehe 2/07/2015 NA 5455 linasema kwa maandishi makubwa kuwa LOWASA:"NIMECHOKA KUITWA FISADI".

Ni kweli Mzee huyo KACHOKA nami NAMI NAKILI KACHOKA KWELI TENA SIO MCHEZO NI ZAIDI..YA TUNAVYOMUONA. Ombi langu kama Mkewe Mama Regina yeye bado ajachoka amshauri Mzee kupumzika kulea wajukuu zake biashara ya IKULU ILISHAFUNGWA SIKU ZILE KWENYE TAMKO LAKE KUWA "MIMI NAONA HAPA TATIZO NI UWAZIRI MKUU"

Anachokiomba hakiwezi kutolewa ama kutetewa na yeyote yule isipokuwa BUNGENI.Anapotuomba ushahidi wakati wenzie walipokuwa wansoma ripoti maarufu kwa jina Richmond yeye aliambiwa APIME NAE AKAPIMA KUACHIA UTAWALA..KUMBE NDIO ALIKUWA ANA AGANA NA URAIS. Kama kuna sehemu anaona alionewa basi haki hiyo hawezi ipata nje ya chombo chochote kile zaidi ya kule AMBAKO ALIAMBIWA APIME nae kwa upeo wake akaona KUPIMA NI KUJIUZURU [RESIGN] NA KUONDOKA SERIKALINI.

Kama ni kosa lilifanyika siku ile ya KUJIUZURU hivyo kusababisha AKOSE haki zake binafsi na za msingi.Na ukilejea kauli zake Mwenyewe, inaonekana dhahiri kuwa UKIONDOA MKEWE HAKUNA MTANZANIA YEYOTE ALIYEJUA UAMUZI WAKE HUO WA KUACHIA NGAZI MPAKA PALE ALIPOKUWA ANATUTANGAZIA WATANZANIA. Kama ndio hivyo basi ukweli ni huu WAHENGA WALISHASEMA HASIRA HASARA.Maamuzi yoyote yanayoegemea ama tegemea hali ya kuwa una HASIRA basi yana madhara makubwa sana na hasara kubwa sana, hasira daima uacha hasara kubwa sana nyuma,kama ambayo yeye anapitia hasara hiyo kwa sasa.Kwa sie Waswahili tunasema ''Hasira ya mkizi furaha ya mvuvi''..yani udhaifu wa yeye kutokuimilki hasira yake kwa upande mwingine imekuwa advantage huko kwingine kunakoitwa tatizo ni Uwaziri Mkuu.

Sasa kupitia Magazeti,Radio na Televisioni ambazo amekuwa akijaribu kuomba watu walete ushahidi UKULASA HUO WA USHAHIDI ULIFUNGWA MWAKA 2008 pale DODOMA NA YEYE KUAMUA KUKAA KIMYA MUDA WOTE NA BAADAE KUIBUKA KWA RACE YA URAIS KWA KASIYA AJABU MIAKA MIWLI ILIYOPITA. NA KAMA KUOMBA USHAHIDI BASI AKIWA BUNGENI HUMO HUMO, TOKA SIKU ZA NYUMA ANGETOA HOJA BINAFSI KWA KUOMBA YEYE MWENYEWE AMA ANGEMTUMIA MBUNGE YOYOTE YULE NDANI YA BUNGE KUJA NA HOJA BINAFSI.KWA KUIBUA HOJA BINAFSI YA KUOMBA ''USHAHIDI'' LABDA SWALA LA TUHUMA ZAKE LEO HII ZINGEKUWA ZIMEFUTWA HUKO HUKO NA KWA MISINGI ILE ILE YA MAJADILIANO YALIOPELEKEA KUTENGENEZA TUME YA MWAKYEMBE...UENDA LEO MZEE WETU HUYO ANGEKUWA WA MWANAKINDAKINDAKI WA UCHAGUZI 2015 YEYE PEKEE BILA UFISADI.

KWA MUJIBU WA KATIBA YA JMT KAMA NILIVYO ONYESHA PALE JUU HAKUNA MTANZANIA AU KIKUNDI CHA WATANZANIA AMA CHOMBO IWE NI MAGAZETI, RADIO AU TELEVISION KINACHOWEZA KUMWONDOA KWENYE TATIZO ZAIDI YA CHOMBO KILE KILE AMBACHO MAAMUZI YAKE HAYAHOJIWI NA CHOMBO KINGINE CHOCHOTE KILE AMBACHO NI BUNGE LA WATANZANIA.SI MAHAKAMA [JUDICIAL ] WALA SI WATENDAJI [EXECUTIVE] WALA VIKUNDI VYETU AU CHAMA CHAKE KINACHOWEZA KUMNASUA NA HIYO KADHIA AMBAYO AMEKILI MWENYEWE AMECHOKA NAO HUO MZIGO MZITO.

MUDA USHAKWISHA SASA, SIJUI KAMA MAMA MAKINDA ANA UWEZO WA KUPOKEA HATI YA DHALULA IKIWA TU SERIKALI YENYEWE IMEKULA ZA USO KWA HATI YA DHALULA KWENYE SEKTA YA GASI.OOhh my God with all that!!!Imekuwa kazi bureeee, si mbaya kukaza moyo na kuludi kulea Wajukuu Maisha yaendelee ''IT END BEFORE IT START!!''
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom