Ni kweli hakuna iphone 13 original nchini Tanzania?

Unajuaje? Ndo wanaeka android humo ndani ?
Ukitaka kununua kifaa cha apple nenda mtandao wao na wata kurejesha kwa dealer wao ambaye kwa hapa Tanzania ni Elite na wao watakujibu kwa email na whatsapp na sidhani kama atafanya ujinga wa kuuza feki kuharibu biashara yake
 
Nina maana ya fake kama fake zile zinazotoka China na zinauzwa kwenye baadhi ya maduka ya simu. Refurbished nazielewa vizuri, ukienda kwenye maduka ya Europe ikiwa unayo iphone ya zamani na unataka kununua mpya ya version ya juu, basi huwa wanaichukuwa na kukufanyia refund ya fedha. La muhimu ni kwamba isiwe imevunjika au ina michubuko yo yote.

Simu fake ya iPhone haitumii iOS unakuta ina muonekano Clone wa iPhone na ukiiwasha ndani ni Android yenye theme kama iOS hyo unaijua ni fake sababu kama una iCloud haiwezi kuingia na huwezi access huduma yoyote ya Apple kama iTunes ,Apple music , iMessages hata wala FaceTime huwa ni android kila kitu

So hizo ni rahisi kuzijua wanaotumia ni mtu anaweza kua mshamba sana na nilizionaga mwanza tu na Kariakoo sijawah ona sehemu rasmi zinauzwa

Simu zote za iPhone 90% zinakua assembled in china maana apple wana factory china kwa ajili hyo sababu huko kuna urahisi wa ku produce vitu ( cheap labor ) unaweza soma YouTube more kwa nn makampuni mengi duniani wana viwanda china kwa ajili ya production

Bongo kwetu hapa watu wengi wanatumia refurbished iPhone tena models old zile iphone 6 mpaka 8 na zinawasumbua sababu unakuta parts nyingi ni old zinakufa kufa lakini huwa ni pure iPhone

Hakuna Apple store bongo ndio maana wauzaji wengi wana agiza kutoka kwa international resales store ingawa yapo maduka kama 3 hapa nchini yanayotambulika na apple kama Trusted resale shops in Tanzania , kuan Elite Computers branch mbili na iStore ya mlimani city

Kitu kingine naona kinawachanganya watu ni Softwares updates za Apple iphone 6 inaishia iOS 12 na apple walitangaza hilo walipo release iOS 13 sasa mtu unakuta ana compare features za iphone 6 na X hizi zina software mbili tofauti inagwa hata kama una old softare unaweza access huduma zote za 

Kitu kingine ni design ya simu kutokana na policy ya nchi husika sio simu tu hata vitu kama magari na electronics eqp zingine kila nchi ina policy yake iphone za japan , Uingereza , German ziko tofauti vitu vidogo vidogo mfano simu za US ni lazima uweke symbol ya recycling kama hiyo item ni recyclable or not simu za japan ni lazima iwe na shuttle sound ukipiga picha lazima itoe sauti nk..

So hizi design mbali mbali za nchi pia watu huwa hawazielewi wanahisi design flani ndo original zingine sio which is not true
 
uyu kazoea kuropoka hakuna anachojua, labda iyo feki yake inamaanisha nn?og sio lazima ununue aple store kuna zile ambazo zinapata shida kipind bado cha warranty zinarudishwa na kuingizwa tena kwenye production,ndo hizo zimejaa tz ambazo siofeki,zina kila kitu ambacho unapata kwenye hizo yy anazosema og kutoka apple store
Jibu hoja zake, ukikimbilia kusema anaropoka wewe na Mange mropokaji ni nani hasa? Anakwambia US IPhone 13 zimeisha mbishie kwa hoja...
 
Bongo zikija hata iPhone 13 Mia tano zitaonekana nyingi maana hamna wanunuzi.
ila huyo dada hamjamsoma Tu yeye anataka mmtumie Hela awatumie iPhone
Kwa hiyo watanzania milioni 60 hakuna watu 500 wenye uwezo wa kununua iPhone 13 kwa milioni nne? Hoja ya Mange ni kwamba alitaka kununua hiyo simu lakini maduka yote maajenti wa IPhone huko US hakuna simu zimeisha, sasa inakuwaje bongo zipo tele??
 
Sikuwahi kujua kama Mange ni mjinga kiasi hiki..

Anasema USA stock za iPhone 13 pro zimeisha na zinapatikana kwa shida na anashangaa inakuwaje bongo zipo..anasahau kuwa mtu akileta hata iPhone 13 pc 1000 mpaka zijekuisha kwa hapa bongo ni mziki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo huyo mleta hizo iPhone 1000 huku akijua hazitaisha leo si atakuwa ndezi huyo? Yaani ui hold pesa yako kwa biashara isiyotoka? Kwa nini asilete pisi 200?
 
Kwa hiyo watanzania milioni 60 hakuna watu 500 wenye uwezo wa kununua iPhone 13 kwa milioni nne? Hoja ya Mange ni kwamba alitaka kununua hiyo simu lakini maduka yote maajenti wa IPhone huko US hakuna simu zimeisha, sasa inakuwaje bongo zipo tele??
Kwa hiyo huyo mleta hizo iPhone 1000 huku akijua hazitaisha leo si atakuwa ndezi huyo? Yaani ui hold pesa yako kwa biashara isiyotoka? Kwa nini asilete pisi 200?
Naona mange umekuja kujitetea JF
 
Ukweli ni kwamba, nina zaidi ya miaka 15 sijawahi kununua simu TZ kwa sababu hapo maduka mengi siyaamini! Hata hivyo, kusema eti iPhone 13 Pro zote ni fake ni habari ya kipuuzi!!

Mange anasahau au hafahamu kitu kimoja!! Kwenye baadhi ya nchi za wenzetu... kule walikopatia maisha, tech enthusiast and iPhone Die Hard Fans huwa wanasubiria matoleo mapya kama watu wa Mbagala wanavyosubiri daladala za Ferry!!

Matokeo yake, first day ya mauzo, watu huwa wanasubiri maduka kufunguliwa kama Wateja wa NMB wanavyosubiri tawi la benki kufunguliwa au kama US wanavyokaa standby for Black Friday Shopping! Matokeo yake, maduka yakifunguliwa tu, within a day unakuta iPhone zimekauka!!

Tanzania ni kinyume! Hata ule simu 25 TU, lazima zitakaa sana kwa sababu 10/1 ndio wenye uwezo wa kukimbilia hizo simu! Hata wale tech enthusiasts and iPhone Die Hard Fans, majority wanasubiri miezi ipite ili wanunue za mikononi!!
 
Fact! iPhone fake rahisi sana kuitambua kwa macho tu na hata ndani tofauti na brands zingine kama Samsung.

acheni kuzungumza msichokijua,ndio maana hata mange anawazingua maana hamzijui vyema bidhaa zenu.umeshawahi kukutana na iphone 7 plus fake wewe,12 max fake je!!mpaka ios skin inapigwa ndani huko,na mbaya zaidi inagongwa mpaka animation ya apple logo.kama ni mgeni mjini tayari maumivu.

mtu yeyote ambaye ametumia samsunga hata s2 anajua note 20 fake kabla hata hajaishika.na siri kubwa ni super amoled display,inaongea hata ukiwa km moja mbele.

uliza kkoo blaza uletewe copy ya apple,utajua hujui.hii hapa chini copy ya 11.View attachment 1987125
View attachment 1987126
 
uyu kazoea kuropoka hakuna anachojua, labda iyo feki yake inamaanisha nn?og sio lazima ununue aple store kuna zile ambazo zinapata shida kipind bado cha warranty zinarudishwa na kuingizwa tena kwenye production,ndo hizo zimejaa tz ambazo siofeki,zina kila kitu ambacho unapata kwenye hizo yy anazosema og kutoka apple store
kwa hiyo kwa kipindi kifupi hiki iPhone nyingi zimepata matatizo na kua refurbished na kuletwa soko la bongo kiasi cha kua ziko nyingi mnooo
si juzi Tu zimekua launched au mi sijui.
 
Labda kwa faida ya wachache tu, wenye iPhone na wasionazo hasa kwa wale wenye ku-afford used au second hand iPhones ni kwamba:

1. Kama model number ya iPhone yako inaanza na “M” au “P” basi your iPhone was purchased Brand New. (Hiyo Inayooanza na “P” ni zile Personalized iPhones with engraving ambazo ziko customized kwa michoro/maandishi etc vile impendezavyo mteja kwenye cover lake)

2. If the first letter is “N” your iPhone is an Apple replacement phone was replaced likely due to a service request (ama kudevelop problem/kuwa na fault) & by the way these ones are refurbished by Apple themselves

3. If it starts with “F” your iPhone was refurbished by a carrier or a third-party vendor.

4. And the one starts with “4” that’s a demo version of iPhone.

Pia Hapo hapo kwenye model number ya iPhone Kuna vingine pia vya kutambua kuhusu iPhone yako including zile herufi mbili za mwisho kabla ya slash (/) ambazo-zinaspecify country of origin kwa mfano iPhone yenye model number MKR32LL/A hizo LL represents US n.k. na hiyo M ya kwanza kama nilivyoeleza kule juu.

So, ni hayo tu kwa uchache hasa kwa hizi used unakuta ilishabadilishwa cover kwa fundi ukiicheki kwenye data base kwa kutumia IMEI/Serial number au Model number ya iPhone unakuta rangi tofauti thou details za chassis ni zile zile.

IMG_7136.jpg

Kitu kama haitambua iOS kimbia sana
 
Labda kama hujawahi kabisa kutumia iphone au hata android ndio utapigwa na hayo mafamba

Utayajua sababu
Yanatumia Android na hayana service yoyote ya Apple

Hata yakiwekea theme ya ios kwa kiwango gani lakini ukianza tu kuitumia hata kama ulikua unamiliki itel utajua tu hapa bado ni Android

Hii wanapigwa wasio na ufahamu mzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom