Ni kweli Dullah Planet anastahili kuitwa rais wa Bongo Flavour?

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Mambo vipi mabibi na mabwana? Natumaini uko poa na unaendelea na mitikasi ya maisha vile ambavyo umejaliwa.

Ebana siku ya Jumapili ya tarehe 12 mwezi Julai 2020 ilikuwa ni siku kubwa sana kwenye tasnia ya burudani na michezo. Nisingependa kuongelea kwenye michezo maana hayo yamepita na kilichotokea ndicho hicho unachokijua.

Katika tasnia ya burudani kulikuwa na kampeni moja iliyokuwa ikiendeshwa kwenye kituo cha radio cha East Africa Radio iliyojulikana kama "Simama na mimi". Naweza kusema kuwa kampeni hii ilikuwa ni kubwa sana ambayo ilifanyika pale makao makuu ya IPP Mikocheni jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na watu kibao wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, watangazaji wa East Africa Radio na wadau wa media wao hujiita Team Media.

Hafla hiyo ilikuwa kubwa sana kwa mtangazaji Khamis Abdalah Ambua (Dullah Planet) ambaye alipewa zawadi ya gari aina ya Benz. Hii ilitokana na mchango wake kwenye radio na uvumilivu wake kwenye radio tangu alipopokea kijiti kutoka kwa mwanadada mkongwe Salama Jabir.

Ikumbukwe kuwa East Africa Radio imekuwa radio kubwa na yenye ushindani sana kwenye tasnia ya habari na mambo yawahusuyo vijana. Pamoja na hayo yote bado kumekuwa na lindi kubwa la watangazaji kuhama kutoka hapo kwenda radio zingine mfano; George Bantu, Mamy Baby, Irine Tilya, Scola Kisanga, David Rweganyira na wengine wengi.

Kwa Dullah amekuwa ni mmoja kati ya watangazaji kutoka East Africa Radio kupitia kipindi chake cha Planet Bongo ambaye amekuwa na ushawishi sana huku akivumilia mengi aliyokutana nayo hapo ambayo mengine ni siri yake. Huwezi kubisha kuwa Planet Bongo ni mpinzani mkubwa sana wa XXL ya CMG na Dullah ndiye kama icon ya PB.

Pamoja na yote hayo bado Dullah Planet alipewa heshima ya kuitwa rais wa Bongo Flavor, sasa hapa naomba maoni yako kuhusiana na hili yaani ni kweli anafaa kuitwa rais wa Bongo Flavor au hafai? Nitakuja na mtazamo wangu baadaye.

Kwenu wataalamu.
 
ni swala la kujikubali tu,yani hapa duniani wakati mwingine tunapaswa kujikubali na kujipa vyeo vikubwa.
 
Ungetumabia kwanza kams, kabla ya hapo kulishawahi kuwa na hicho cheo(rais wa bongo flava) na nani alikua rais hapo kabla na vigezo gani vilitumika ndio tujue huyo bwana dula qnastahilia au na si tupate nafasi ya kuchangia
 
Inakuwa nje ya uwezo wangu labda ufuatie
 
Mambo vipi mabibi na mabwana? Natumaini uko poa na unaendelea na mitikasi ya maisha vile ambavyo umejaliwa.

Ebana siku ya Jumapili ya tarehe 12 mwezi Julai 2020 ilikuwa ni siku kubwa sana kwenye tasnia ya burudani na michezo. Nisingependa kuongelea kwenye michezo maana hayo yamepita na kilichotokea ndicho hicho unachokijua.

Katika tasnia ya burudani kulikuwa na kampeni moja iliyokuwa ikiendeshwa kwenye kituo cha radio cha East Africa Radio iliyojulikana kama "Simama na mimi". Naweza kusema kuwa kampeni hii ilikuwa ni kubwa sana ambayo ilifanyika pale makao makuu ya IPP Mikocheni jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na watu kibao wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, watangazaji wa East Africa Radio na wadau wa media wao hujiita Team Media.

Hafla hiyo ilikuwa kubwa sana kwa mtangazaji Khamis Abdalah Ambua (Dullah Planet) ambaye alipewa zawadi ya gari aina ya Benz. Hii ilitokana na mchango wake kwenye radio na uvumilivu wake kwenye radio tangu alipopokea kijiti kutoka kwa mwanadada mkongwe Salama Jabir.

Ikumbukwe kuwa East Africa Radio imekuwa radio kubwa na yenye ushindani sana kwenye tasnia ya habari na mambo yawahusuyo vijana. Pamoja na hayo yote bado kumekuwa na lindi kubwa la watangazaji kuhama kutoka hapo kwenda radio zingine mfano; George Bantu, Mamy Baby, Irine Tilya, Scola Kisanga, David Rweganyira na wengine wengi.

Kwa Dullah amekuwa ni mmoja kati ya watangazaji kutoka East Africa Radio kupitia kipindi chake cha Planet Bongo ambaye amekuwa na ushawishi sana huku akivumilia mengi aliyokutana nayo hapo ambayo mengine ni siri yake. Huwezi kubisha kuwa Planet Bongo ni mpinzani mkubwa sana wa XXL ya CMG na Dullah ndiye kama icon ya PB.

Pamoja na yote hayo bado Dullah Planet alipewa heshima ya kuitwa rais wa Bongo Flavor, sasa hapa naomba maoni yako kuhusiana na hili yaani ni kweli anafaa kuitwa rais wa Bongo Flavor au hafai? Nitakuja na mtazamo wangu baadaye.

Kwenu wataalamu.
Amekuwa Rais kupitia chama kipi ?
 
Kwa pale ndani ya EA RADIO kwa mchango wa kuibeba bongo fleva jamaa hana mpinzani wake. Na amedumu kwa muda mrefu bila kutetemeshwa na beba beba ya media nyengine.

Jamaa wameamua kutambua mchango wake.
 
Umesomeka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom