Ni kweli CORONA ni hatari tena hatari sana tuunganeni na Amiri jeshi mkuu wetu kwenye hii Vita kila mmoja wetu awe chachu ya Mabadiliko be the change

Ni kweli tangu nijitambue hapa Duniani kwa kuwa na ufahamu sijawahi kuona hofu kama hii inapamba moto Duniani, inaitisha DUNIA kiasi hiki kweli hofu imetawala lakini lazima tuishinde

Nawaombeni vijana wa kitanzania huu si wakati wa kuimba nyimbo za vyama, dini, hadhi au kabila huyu mdudu ni adui yetu hana utani, amedhamiria kutumaliza tusikubali lazima tupambane kumshinda lazima tushinde kwa kuchukua tahadhari

Kila mmoja wetu awe mwanamabadiliko tuwahimize wasioelewa waelewe umuhimu wa kufuata kanuni na Taratibu za afya

Viobgozi wa Dini huu ndio mda wa kuwahubiri waumini wenu njia za kuchukua hatari tusikubali huyu mdudu atuangamize anatisha

Huyu ni ibilisi mtoa roho amekuja kwa mtindo wa Virus tupambaneni kumuondosha

Tuunganeni na Rais wetu kutii sheria kanuni na matumizi ya njia za kitaalamu

Watanzania wenzangu nawaombeni kila mmoja achukue tahadhari Vita bado ni kubwa tupambaneni tena bila kuchoka adui ana nguvu za kutisha tuunganeni kumuangamiza

Hivi kila kitu lazima mumchomeke huyo rais wenu? Sisi ni watu wazima tunaweza kujilinda bila kumtegemea huyo rais wenu. Kila kitu rais wetu rais wetu. Yeye atakeleze nafasi yake kutokana na mshahara anaolipwa, na sisi tutatekeleza wajibu wetu, sio mambo ya kutuletea habari za rais wenu.
 
Back
Top Bottom