kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,469
- 4,903
Siku chache zilizopita mkuu wa Kaya alitoa kauli ambayo ilipokelewa kwa hisia tofauti tofauti na wadau wa siasa, ni pale aliposema kuwa CCM itatawala milele.
Anaweza akawa hayupo sahihi kwani mambo yanabadilika na watu wanabadilika lakini kitu ambacho Kiko wazi kabisa ni kwamba CCM itaendelea kuitawala nchi hii hadi pale tutakapopata vyama vya siasa.
Ukweli mchungu ni kuwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hatujawahi kuwa na vyama vya siasa kwa upande wa upinzani, bali tumekuwa tuna watu binafsi ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakija na kuondoka. Ni bahati mbaya utamadumi wa nchi yetu, wananchi na mfumo( decision makers) unaonekana kutokubaliana na aina hii ya siasa za upinzani na kwa hili hata Kama hayo yote uanayosemwa kuwa mazingira magumu kwa vyama vya upinzani yakirekebishwa bado upinzani uliopo sasa hauwezi kushinda uchaguzi.
Tanzania ni taifa lililokamilika ni tofauti na Kenya, Uganda karuwanda au Kaburundi ambapo mtu mmoja mwenye nguvu au umaarufu ni rahisi watu na mfumo kumkubali unahitaji zaidi ya umaarufu na nguvu za kisiasa kuwa Rais wa Nchi hii na hapa Swala la Chama Chenye uimara kuanzia kimuundo na kimdumo bila kusahau aina na idadi ya wanachama ni mhimu.
Mrema alikataliwa, Silla alijitahidi Lowassa alikataliwa, Lissu atakataliwa, Zitto atakataliwa na hata angeletwa bwana Yesu hapa nawaapia atakataliwa tu.
Huu ndo ukweli mchungu, hivi ndivyo Taifa hili lilivyo ndivyo lilivyodizainiwa na ile ufanikiwe lazima ukubaliane na hali hii, lazima uje na muundo unaokubalika na kwa maana hiyo lazima the so called vyama vya siasa vilione hili waachane na kasumba ya kujenga watu maarufu bali watengeneze vyama vyenye mifumo na miundo imara na inayoeleweka bila kusahau watu Imara na wanaoaminika.
Watanzania, utamduni na mfumo wa nchi hii haitaki akina Kabwe, Akina Lissu au akina Lowassa, Wanataka ACT, CHADEMA, NCCR na CUF zilizo imara ndio maana Lowassa Leo Ikulu anaiskia hewani huku Anko akiwa anapunga upepo mle ndani, kabla ya July 2015 inawezekana ilikuwa hata siyo rahisi kwa Anko kupata nafasi ya kusalimiana na Lowassa, walikuwa ni mbingu na Nchi, lakini utamaduni, watanzania na mfumo vilimkataa mzee wa Monduli kwakuwa tu tu hakuwa ndani ya Chama, Hii ni Nchii, huwezi kupewa tu tuma unavopewa gari au shamba.
Kitu kimoja ambacho lazima tutambue, Watanzania na mfumo ndo watu wenye dhamana ya kuamua nani awe Rais na Wala si wanaCCM na sio kwamba watanzania au mfumo wanakipendelea Chama Cha Mapinduzi ukweli ni kwamba Chama Cha Mapinduzi ndo Chama pekee kinachokizi matakwa ya utamaduni, matakwa ya watanzania na mfumo.
Mwenyekiti Mbowe alijitahidi Sana kukijenga Chama Cha Democrasia na Maendeleo ili kukidhi mahitaji haya, bahati mbaya akaingiwa na tamaa, akaanza kugombana na vijana wake na hitimisho lilikuwa mwaka 2015, CHADEMA ya mwaka 2005-2010, Kama ingeendelea kulelewa vizuri pengine 2025 kwa Mara ya kwanza tungekuwa na vyama viwili vya siasa na hivyo kuwapatia uwanja mpana Watanzania na Mfumo
kuamua nani wa kumpa Dora bahati mbaya safari hii ya matumaini iliyoanza mwaka 2003-2004 imeishia ukingoni mnamo mwaka 2015 na hakuna jitihada zozote zinaonekana kujaribu tene kujenga Chama katika namna ambayo inakidhi matakwa ya utamaduni wa Nchi hii, wanatanzania wenyewe na mfumo, wanarukaruka tu.
Narudia na huu ni ukweli Mchungu hadi tutakapopata vyama vya upinzani ndipo utawala wa CCM utakapokoma, Zitto, Lissu, sijui Lowassa hawawezi kushindana na CCM halafu wategemee kupewa Nchi, Watanzania si wajinga, hii si Nchi inayoweza kuongozwa Kama Kashamba tuu ka mtu, hv Leo Zitto, Lissu au Mbowe akipewa Nchi na hutu tu vyama twao nani atawafung speed gavornor, kwa sababu Rais ni kiongozi mkubwa na ambaye maamuzi yake Yana athari kubwa kwa taifa hili, hivyo lazima atokane na Chama kinachoelelweka, chenye mifumo na taasisi Imara na chenye watu Imara wanaoaminika na kufahamika vyema na amabao wanaweza hata kumkemea hata Rais mwenyewe, ka ACT au KaCHADEMA ambapo hakawezi kumkemea au kumkosoa Zitto au Mbowe Leo kanawezaje kesho akiwa Rais.
Mwisho kabisa acheni kuwalaumu Watanzania na mfumo, jengeni vyama vyenu vikizi matakwa mtapewa Nchi, CCM hawana hati miliki ya Nchi hii Bali ndo Chama pekee kinachokizi vigezo kwa sasa.