Ni kweli CHADEMA itanufaika na msaada wa mafisadi 2020?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Kumekuwa ni shangwe miongoni mwa wanachadema wengi wakiamini kuwa hatua za serikali na CCM kuwaondosha mafisadi kuwa watakuwa na msaada mkubwa kukiwezesha chama hicho kuwa na ushawishi kwa wapiga kura na hatimaye kushika dola.

Ikumbukwe uwepo wa mafisadi kwa miaka takribani kumi ulipelekea CCM kushuka umaarufu kwa wananchi ambao kimsingi waliitaka CCM iwaondoe ili kurudisha imani.

Je ni kweli sasa wananchi wamewasahau watu hawa waliopewa jina la ''magamba'' na CCM?..ikumbukwe si kila maovu ya kisiasa hupelekwa mahakamani bali mara nyingi mahakama ya mafisadi ni wananchi kupitia sanduku la kura.

Nawatakia CHADEMA kila laheri katika mpango wao wa kuwatumia wahalifu,wezi na mafisadi katika ujenzi wa chama imara kitakacholeta ushindani nchini.

Tujibizane kwa hoja na si majibu ya vijembe,hasira,jazba,matusi..nk.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom