Ni kweli CHADEMA imewatosa watu wake?

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
724
242
Kuna mtu aliwahi kuweka uzi humu akidai kuwa CHADEMA haiwasaidii wanachama wake wenye kesi za uchaguzi (wabunge na madiwani). Nilitaka kuamini kuwa uzi ule haukuwa sahihi.

Leo nimeshtuka kusikia kuwa Joseph Fuime aliyemshtaki Leonidas Gama (Songea) kupinga matokeo ya ubunge akilalamika kuwa Chama hakikuwahi kumsaidia (kwa hali na mali) katika kipindi chote cha kesi. Na sasa baada ya kushindwa kesi Fuime anatakiwa kulipa 12m ambazo kwake ni mtihani. Anasikitisha.

Bila shaka ndiyo maana inaonekana kuwa sehemu nyingi CHADEMA walipokata rufaa za ubunge na udiwani wamepoteza rufaa hizo. Hata ukimwangalia Waitara wa Ukonga licha ya kumshinda Silaa jana mahakamani inaonekana kama hana furaha sana kwani Chama kilimuacha. Tusipuuzie hali hii…
 
Back
Top Bottom