Ni kweli Bustani ya Eden ipo Tanzania?

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,025
Source: Radio France Internatinale.

Juzi wakati nasikiliza hii radio, kulikuwa na mama mmoja anahojiwa. Huyu mama anaitwa Chaiba Kombo ni Mwandishi wa Vitabu na Mdau mkubwa wa Sanaa za hapa Tanzania. Kwa hapa Tz sio maarufu sana ila nje ya mipaka kachukua tuzo nyingi za uandishi wa vitabu vya kijadi.

Sasa wakati anahojiwa alieleza kwamba research zake alizozifanya licha tu ya kuonyesha kwamba mifupa ya kale imegunduliwa hapa tanzania(Olduvai Gorge), ni kwamba wale watu wa zamani waliokufa kwenye gharika la Nuhu(kizazi kile kiliteketea kwa maji), mifupa yao watu hao ipo hapa tanzania na ana ushahidi huo.

Akaenda mbali zaidi akasema Bustani ya Eden walipokaa wazazi wa mwanzo Adam na Eva pia ilikuwapo hapa Tanzania. Research yake kajaribu kuipeleka Chuo kikuu cha Dar UDSM, lakini mawazo yake waliyapuuza na hawakumpa ushirikiano. Kwahiyo anafanya kazi na wattu wa Mataifa sasahivi.

Vp wadau kuna details zozote kwa mwenye kulijua hili?
 
Mkuu nadhani nna DVD ya hiyo documentary, nikumbushe wikiendi ntaiweka hapa!
 
Kwa Mujibu wa Wataalamu wa Mambo ya Kale, Eden ilikuwa nchin Iraq, Katika ya Mito miwili mikubwa , Mto Tigris na Mto Euphrates, ile ardhi ya katikati ndipo ilipokuwa Bustani ya Eden. Hiyo kusema ipo Bongo ni uzushi.
 
Vp kuhusu watu wa Nuhu nao ni uzushi ama?
 
na hizi ndio simulizi halisi za kusadikika,..............mimi kwa uchunguzi wangu nimekuja kugundua bustani ile ilikua marekani na ufaransa....ahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,..joke
 
Back
Top Bottom