Ni kweli bilioni 10 zimejenga flat 20? Au tuna woga kuhoji gharama halisi?

kwa maisha ya wakazi wa mgomeni kota mtu umweke gorofa ya tisa mbona mtihani, maji yakikatika house girl kazi anayo, haya magunia ya mkaa yatafikaje huko? wasasambuaji nao balaa utaona chupi nyekundu imeanikwa gorofa ya nane inapepea kama bendera ya simba, niliwa enda pale kambi ya farasi kilwa, unakuta mtu anaishi gorofa ya nne anataka apikie kuni! huku nako usishangae unapita chini kwa mguu mara pyaata rambo yenye mzigo imerushwa.
 
Mmezoea kupiga dili this time is over hakuna cha dili huo mradi ni 10 Bilioni if you like or not.
 
Kuna taasisi nyingi tu zimefanya kazi kwa kujitolea (nilisikia kwa mfano SUMA JKT wamejenga fence na kutoa ulinzi kwa kipindi chote cha mradi). Kwa hivyo ni wazi tu thamani (gharama?) ya hayo majengo ni zaidi ya hivyo inayotajwa kama kazi zote zikithaminishwa (hata kama hakukuwa na cash payments). Ni sawa kwa mfano mtu anunue cement na mchanga halafu afyatue matofali mwenyewe na kujenga ajenge mwenyewe akishirikiana na mkewe na watoto. Ni kweli pesa (cash) watakayotoa itakuwa ndogo lakini itakuwa sahihi kuchukua kiasi hicho cha cash waliyotoa kama thamani halisi ya nyumba yao? Wakimpa mtu mwingine kiasi hicho hicho ataweza kujenga nyumba kama yao kama akilipia cash materials na nguvu kazi yote inayotumika?

Lakini ndugu zangu tusisahau pia mambo haya yana siasa "mingi" sana ndani yake. Mmeona mtukufu rais ameacha hata kwenda msibani tena msiba wa mashujaa! Kwa hivyo muangalie mambo haya kwa jicho la kisiasa zaidi. Ukiangalia kitaaluma utavuruga Pasaka yako bure tu.

Karibuni pilau jamani!:)
 
kwahiyo milioni 125 haijengi floor moja waungwana? ok anyway tufanye wamejenga majengo yote kwa Tsh elfu 80, au trillion mia au billion 10, so what?????????
Majibu yote ya mleta mada na vibaraka wake yote yako hapa...
Kutumia nguvu nyingi kuhoji na kujadili vitu visivyo na ulazima kwako nayo ni K.
 
Sifa moja kuu ya tawala za kidikteta popote Ulimwenguni ni kudanganya na kupika data...namba ndogo huongezewa sifuri mbele iwe kubwa na kubwa hupunguziwa sifuri ili iwe ndogo...it is the case with Russia, Uganda, Rwanda nk. na sasa Tanzania...kama unafanya research katika nchi hizo inabidi uchanganye akili za kuambiwa na za kwako maana information is frightfully not reliable!
Well noted. However provide proof siyo maneno matupu ....!! Mwaga data tulinganishe ....
 
Tunafurahia kupata hostel mpya za kulala wanafunzi pale Udsm. Ni sawa. Tumefahamishwa kuwa kuna flat 20 zenye floor 4 kila moja.

Mimi sio mtaalamu wa majengo. Lakini wataalamu wa majengo wanaweza kweli kututhibitishia kuwa hizi bilioni kumi ndio halisia? Ukiangalia kwa ukaribu unapata shaka. Naamini kuna hela imezidi Ila kwa vile mkuu alishatamka hicho kiasi basi TBA wamelazimika kuendelea kukariri bilioni kumi.

Jé wasimamizi wa mradi huo walikuwa hawalipwi? Bodi ya ukadiriaji majenzi ina standard zake katika kujenga Jengo lolote. Nina amini ipo siku tutapata uhalisia wa gharama hizo.

Kuna athari kubwa ya kutokuwa wakweli katika mradi huo. Athari yake ni kuwa kila jengo litakalojengwa nchini kama litapita gharama hizo basi wataambiwa wameweka chá juu. Tuliona hili kule Simiyu. Rais alikataa Jengo lenye kukadiriwa hela nyingi. Akatoa mfano wa bilioni kumi katika mradi huu wa mabweni ya udsm. Wataalamu watakuwa na woga kuleta gharama halisi zá majengo kwa hofu ya kuambiwa wameweka chá juu.

Tunahitaji kupata majengo haya kwa gharama nafuu lakini isiwe chini ya nafuu. Natoa wito wakadiriaji majenzi waje hapa kutupa standard zao zikoje kwa majengo kama haya. Wasiogope kusema ukweli.

Flat 20 ina maana kila flat iligharimu shilingi milioni 500. Jé flat moja lenye floor 4 gharama yake ni milioni 500? Na hapo hapo wakajenga na uzio. Sitaki kufurahia tu kupata majengo haya lakini lazima gharama halisi zionekane.
Nadhani wewe ulizoea kupiga dili au baba yako alikuwa kazoea kupiga dili. Safari hii mtanyooka tu, hivi sasa wewe umegeukia mitandaoni ili uungwe mikono kuwa gharama ni ndogo ili uruhusiwe wewe na baba yako mpige dili. Kamwe haitawezekana.
 
Chadema hamuamin hamin. Magu ni chuma. 500 milion kama una ardhi flat yenye floor nne inatoka na chenchi kubaki.
Huo ndo ukweli. Me nimeshasimamia ujenzi wa nyuma sana tu.
Kama ardhi ni flat, cement unachukulia kiwandani na vifaa vingine unachukua kwa oda kiwandani, hapo kumbuka serikali inaweza kutoa hata kodi kwa wauzaji wa vifaa ili ikajengee majengo m.f kama hizo hostel...
Mimi naamini hapo kuna ufisadi umefanyika ... Tumepigwa chenji ya kutosha...
Hapo kila jengo tumepigwa milioni 60 mpaka 40 kwa wastani.
Ajabu watu badala ya kuleta mada ya jinsi tulivyoibiwa kwenye hizi hostel wako busy kusema hiyo bajeti ya 10b haiwezi kutosha kujenga hayo majengo !!!
Sijui Magu katumia dawa gani kuwaroga hawa wapinzani wa Tanzania???? Dah ama kweli maisha yako speed sana yamebadilika mno.
 
Nadhani wewe ulizoea kupiga dili au baba yako alikuwa kazoea kupiga dili. Safari hii mtanyooka tu, hivi sasa wewe umegeukia mitandaoni ili uungwe mikono kuwa gharama ni ndogo ili uruhusiwe wewe na baba yako mpige dili. Kamwe haitawezekana.
Ungemsaidia sana Rais wako kama ungejibu hoja. Sasa shida yako ni kuishia lá pili B. Hoja yangu itaonekana na maana kubwa kwa kushindwa kwako kujibu na unatanguliza matusi ukidhani mimi nitashtuka.
 
Unaposema mafundi walikuwa wanavaa boxer kazini sijakuelewa hebu tuwekee picha tujiridhishe, kuhusu gharama sijakuelewa kama diamond kanunua nyumba ya gorofa moja tena uzunguni kwa mil 300, kinachokufanya ushindwe kuamini hizo gharama ni nini? nimekuwekea picha za mafundi walivyokuwa kazini.

6-1.jpg

mkuu umeniwekea picha siku ya ukaguzi ambayo amekuja rais, siku hiyo wote walikua wana shine na reflectors, japo sio matraffic au watu ambao reflector ni muhimu sana kwao. mavazi ya site sio reflector mkuu. japo zinaweza kuwepo ila ni makoti, mabuti, kofia zenye utambulisho, kamba za kujifunga ukiwa juu, ma ovaroli nk. site safety measures ikiwemo njia za kupita watu materials nk. naamini at OSHA hawakupita pale, maana mradi ungefungwa kwa viwango vile vya safety
-nimekuwekea picha, angalia nani ana reflector, kofia, kila mmoja kajivalia tshirt, mmoja kushoto amevaa ndala. ningeweka zaidi ila si unajua "u have the freedom but not to that extent"
-diamond kununua nyumba kwa mil 300, ilo hatuwezi jiridhisha na sijaelewa inahusika vp. hua wenye taaluma za ujenzi hatulinganishi kiivo.
-hoja yangu kubwa ni kwamba, kuna mambo ambayo hayajafanywa na ndo maana wametumia kias kidogo cha pesa na kutumia muda mdogo, kiasi gani haswa basi wanajua wenyewe waliohusika moja kwa moja. inawezekana ilikua bil 8. ila kama huku notice kwenye ufunguzi hakuna aliekazia kwamba bei ikikua kiasi gani sbb sio bil 10 kiukweli!

680fe43cb7bde41d1780c4e0fb7750a4.jpg
 
You are absolutely right. We need to criticize to get the real cost. There is a big effect ahead on hiding this issue. I think there were some additional costs not disclosed tô public. It seems surveyors and contractors plus engineers were exaggerating the expense. Magufuli will always refer to this cost. Let us wait for.

ita very disappointing but the best thing with buildings is that. time always tells the truth! he has already refered to that cost in his speech to the magereza coming project and some 56Bn hospital
 
Lakini yamejengwa,ingekuwa hayajajengwa mm naona ndiyo ulikuwa na haki ya kuhoji. Pengine kwa mtazamo wangu wewe na kikundi chako mmezoea kupiga dili ambazo zinatuohopesha sisi hata kujenga kajumba ka kisasa tuishie kwenye matembe.Hongera Mh. Raisi kutufungua macho nasi tutatafuta kandarasi wa bei poa tujenge shule , zahanati, nyumba za wauguzi na walimu kwa bei safi kabisa. Heri ya Paska ndugu zangu Hosteli ndiyo hizo tayari
Hata hivyo sidhani kama kulikuwa na haja ya kusema kiasi cha fedha kilichotumika kama hakuwa tayari kusema ukweli. Ukiamua kuwa msemakweli mpenzi wa Mungu uuseme ukweli.

Sikuona sababu ya msingi ya kutaja thamani ya majengo. Idadi ya wanafunzi watakao ishi humo ilitosha kabisa.
 
Nyumba tu,standard ya kawaida inakimbilia milioni 100,sasa ghorofa ina zege ya msingi,nguzo,nondo, kokoto,

Halafu weka miundombinu ya ghorofa ya kwanza,zege la kutosha,mondo,kokoto,


Halafu weka miundombinu ya ghorofa ya pili,zege,kokoto,mchanga,simenti,nguzo.....


Endelea hovyo mpaka ghorofa ya NNE

Haya,finishing,vigae,rangi,umeme,fenicha,

Lipa maji,vibarua


Ngumu sana kutumia milioni 500 tu
Labda izo 10B za mkubwa zingine wamejazia wafadhili ziko nyuma ya pazia
 
vijijini kule kuna jamaa wanajenga nyumba asubuh na jion anahamia ukimuuliza imemla bei gan haizidi elf 12,, huku mjini kuna watu wanalipwa take home ya m 16 kwa mwez, walinzi wanapewa 120k kwa mwezi ila wote hawafi njaa na wote mishahara ya mwezi huu haikuti akaunti zao zikiwa na masalia ya mshahara wa mwezi ulopita! sayansi ya pesa ni ngum sana na always me naamini pesa yoyote inatosha na ukiamua pia pesa yoyote haitoshi
 
Watanzania ni wagumu sana kuelewa, rais kwa kauli yake amesema kila Flat ni 10 billion na hivyo jumla ni 200 billion

Acheni Ubashite basi

Kama Kuna mtu bado anaamimi yale majengo yote ni 10B huyo na mjinga, zwazwa, poyoyo, zezeta, mburura, kiazi, kilaza, mpumbavu, mpuuzi na lofa
 
Aliyejenga ndiyo anajua gharama halisi.Kuna bwana mmoja aliwahi kusema kuwa serikali ya Tanzania ina uwezo wa kumjengea nyumba baba mwenye familia!Wanjanja wakasema haiwezekani!Nchi za wenzetu serikali inajenga raia wanapanga.Nyumba thamani yake inatofautiana na nyumba nyingine kwa vitu vilivyotumika kujengea ikiwa ni pamoja na makadirio ya nyumba hiyo itadumu kwa muda gani?Kwa hiyo waweza kujenga kwa tofali 40 za inchi tano au sita na mwingine akatengeneza tofali 20 kwa mfuko.Uimara wa nyumba hizo utaonekana katika umri wake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom