Ni kweli bilioni 10 zimejenga flat 20? Au tuna woga kuhoji gharama halisi?

Yani hapo tumewapiga wapinzania!!njoni na hoja nyingine!!!2020 lazima tuzike upinzania ichara!!! Na mkileta lowasa tena ndo mumekwisha!!tunawachezesha ngoma msiyoijua!!pumbaaaaaf!!!
 
Mimi si civil engineer. Lakini nina hakika hiyo figure ni cooked ili tu kumridhisha mfalme. Isipokuwa imeandikwa "UKWELI UTATHIBITIKA DAIMA, ISIPOKUWA UONGO NI WA KITAMBO TU"! Muda utasema....!
 
Unaposema mafundi walikuwa wanavaa boxer kazini sijakuelewa hebu tuwekee picha tujiridhishe, kuhusu gharama sijakuelewa kama diamond kanunua nyumba ya gorofa moja tena uzunguni kwa mil 300, kinachokufanya ushindwe kuamini hizo gharama ni nini? nimekuwekea picha za mafundi walivyokuwa kazini.

6-1.jpg
Hawa walikuwa hawalipwi? Au gharama za Ujenzi zina exclude gharama zá mjengaji?
 
Mi naomba raia turuhusiwe kuwakodisha flat moja kwa 550 serikali ile 50 raia tusiwe tunapigwa cha juu
 
kuna watu wanapenda kuhojihoji kuhusu ujenzi wa hotel za udsm lakini kumhoji mbowe kuhusu matumizi ya pesa za chadema wanaogopa!!!!
Sio kila anayehoji ni mwanachama wa Chadema. Kama fikra zako zipo hivyo basi hao chadema ni great thinkers katika nchi hii. Hujajua effect yake ya kuficha hizo gharama halisi.
 
Tunafurahia kupata hostel mpya za kulala wanafunzi pale Udsm. Ni sawa. Tumefahamishwa kuwa kuna flat 20 zenye floor 4 kila moja.

Mimi sio mtaalamu wa majengo. Lakini wataalamu wa majengo wanaweza kweli kututhibitishia kuwa hizi bilioni kumi ndio halisia? Ukiangalia kwa ukaribu unapata shaka. Naamini kuna hela imezidi Ila kwa vile mkuu alishatamka hicho kiasi basi TBA wamelazimika kuendelea kukariri bilioni kumi.

Jé wasimamizi wa mradi huo walikuwa hawalipwi? Bodi ya ukadiriaji majenzi ina standard zake katika kujenga Jengo lolote. Nina amini ipo siku tutapata uhalisia wa gharama hizo.

Kuna athari kubwa ya kutokuwa wakweli katika mradi huo. Athari yake ni kuwa kila jengo litakalojengwa nchini kama litapita gharama hizo basi wataambiwa wameweka chá juu. Tuliona hili kule Simiyu. Rais alikataa Jengo lenye kukadiriwa hela nyingi. Akatoa mfano wa bilioni kumi katika mradi huu wa mabweni ya udsm. Wataalamu watakuwa na woga kuleta gharama halisi zá majengo kwa hofu ya kuambiwa wameweka chá juu.

Tunahitaji kupata majengo haya kwa gharama nafuu lakini isiwe chini ya nafuu. Natoa wito wakadiriaji majenzi waje hapa kutupa standard zao zikoje kwa majengo kama haya. Wasiogope kusema ukweli.

Flat 20 ina maana kila flat iligharimu shilingi milioni 500. Jé flat moja lenye floor 4 gharama yake ni milioni 500? Na hapo hapo wakajenga na uzio. Sitaki kufurahia tu kupata majengo haya lakini lazima gharama halisi zionekane.
Ungepewa tenda wewe ungeongeza za kwako ngapi?
 
namna walivyo weza kupunguza gharama na kutumia muda mfupi.
-kutofwata au kupindisha taratibu za kawaida za ujenzi.
-health and safety ya site (unamkuta fundi yuko kwenye scaffolds floor ya tatu amevaa ki boxer cha jeans vest na yebo yebo)
-professional fees (hakuna msimamizi wa kusimamia quality ile)
-inawezekana walipata exemptions in tax, authorities mbali mbali (manispaa, fire, registration boards, insurance, bonds nk)
-ku procure materials karibu zote zilizokua available locally kwenye stock za watu (bila kujali ubora wake, mfano madirisha)
-mjenzi kutopata faida (ceo wa tba si analipwa mshahara na serikali sijui kama anahitaji faida yoyote zaidi ya kupewa heshima na shukrani)
-kutotumia vifaa vya kisasa na methods za kisasa (ndo maana nguzo, slabs, plaster nk karibia vyote vimepinda pinda tena kwa kipicho cha macho, mambo ya mirunda na tape measure)
-kuruka heirachy ya wataalamu. manake kuna msimamazi probably engineer na casual labour labda na fundi wachache sana, manake hakuna technicians, experienced surveyors nk.
-kutoruhusu second opinion. (kazi achore, ajenge asimamie mtu huyo huyo ni muujiza kua na ubora)

nimechoka kuandika ila generally
wamejenga at a low cost at the expence of quality. hata ivo i still doubt if its as low as 10bn.

hofu yangu
-ule mradi kutumika kama mfano wa ubora, gharama nafuu na muda mchache wa ujenzi.
na zaidi mfano kua ma contractor ni wezi, wataalamu huweka gharama za uongo, na kutokua na sababu ya wasimamizi.
-kukimbia initial cost na kukubali mzigo wa maintanance cost. (kwa mabweni litakua under maximum use or over utilized)
-usalama wa yale majengo (kwa macho lile eneo ni water logged na fence ya huo mradi mpya ilibomoka juzi tu kama mita 30 wakaujenga upya kwa mvua ya siku moja)
-ata tusiongelee issues za fire fighting systems, usalama wa vitu floor za chini kwa madirisha yale nk.

Nia ni nzuri ila sasa methods, inasikitisha sana!
You are absolutely right. We need to criticize to get the real cost. There is a big effect ahead on hiding this issue. I think there were some additional costs not disclosed tô public. It seems surveyors and contractors plus engineers were exaggerating the expense. Magufuli will always refer to this cost. Let us wait for.
 
Sisi Watanzania hatujui iwapo kama zimetumika bilion 10 au la! Kwakuwa watoaji ni haohao, walaji ni haohao. Watanzania hatukuhusishwa kuzihesabu hizo bilioni wakati wa malipo. Asanteni!!
Sema baadhi ya watanzania kama wewe na si wote, nyinyi mnaeleweka, shida yenu kubwa ni pilau, tshirt, kapelo na kanga wakati wa kampeni. Mkipewa hivyo tu basi hamna shida tena.
 
Tunafurahia kupata hostel mpya za kulala wanafunzi pale Udsm. Ni sawa. Tumefahamishwa kuwa kuna flat 20 zenye floor 4 kila moja.

Mimi sio mtaalamu wa majengo. Lakini wataalamu wa majengo wanaweza kweli kututhibitishia kuwa hizi bilioni kumi ndio halisia? Ukiangalia kwa ukaribu unapata shaka. Naamini kuna hela imezidi Ila kwa vile mkuu alishatamka hicho kiasi basi TBA wamelazimika kuendelea kukariri bilioni kumi.

Jé wasimamizi wa mradi huo walikuwa hawalipwi? Bodi ya ukadiriaji majenzi ina standard zake katika kujenga Jengo lolote. Nina amini ipo siku tutapata uhalisia wa gharama hizo.

Kuna athari kubwa ya kutokuwa wakweli katika mradi huo. Athari yake ni kuwa kila jengo litakalojengwa nchini kama litapita gharama hizo basi wataambiwa wameweka chá juu. Tuliona hili kule Simiyu. Rais alikataa Jengo lenye kukadiriwa hela nyingi. Akatoa mfano wa bilioni kumi katika mradi huu wa mabweni ya udsm. Wataalamu watakuwa na woga kuleta gharama halisi zá majengo kwa hofu ya kuambiwa wameweka chá juu.

Tunahitaji kupata majengo haya kwa gharama nafuu lakini isiwe chini ya nafuu. Natoa wito wakadiriaji majenzi waje hapa kutupa standard zao zikoje kwa majengo kama haya. Wasiogope kusema ukweli.

Flat 20 ina maana kila flat iligharimu shilingi milioni 500. Jé flat moja lenye floor 4 gharama yake ni milioni 500? Na hapo hapo wakajenga na uzio. Sitaki kufurahia tu kupata majengo haya lakini lazima gharama halisi zionekane.
Jibu ni kupata takwimu za mkataba uliosainiwa vinginevyo ni kuogelewa kwenye tope
 
You are absolutely right. We need to criticize to get the real cost. There is a big effect ahead on hiding this issue. I think there were some additional costs not disclosed tô public. It seems surveyors and contractors plus engineers were exaggerating the expense. Magufuli will always refer to this cost. Let us wait for.
yes, the price of land is not inclusive and 10%'s were excluded,
 
Naombeni mnijuze namna ya kuwapata hao wakandarasi, na mnijuze kama wanajenga na nyumba za watu binafsi.
Maana ninakiwanja changu kikubwa na nina hizo ml 500
Nataka wanijengee na mimi flat kama hizo nipangishe.
Maana hadi kauzio nitapata kwa hiyo pesa.
Wakuu nijuzeni fasta na mimi nimiliki flat hapa mjini
 
hapana kaka hii ni idara ya serikali, ila wazo zuri kama wataamua kujiendesha kibiashara sio mbaya.
 
Back
Top Bottom