Ni kweli bilioni 10 zimejenga flat 20? Au tuna woga kuhoji gharama halisi? | Page 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli bilioni 10 zimejenga flat 20? Au tuna woga kuhoji gharama halisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikivembu, Apr 15, 2017.

 1. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2017
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,912
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Tunafurahia kupata hostel mpya za kulala wanafunzi pale Udsm. Ni sawa. Tumefahamishwa kuwa kuna flat 20 zenye floor 4 kila moja.

  Mimi sio mtaalamu wa majengo. Lakini wataalamu wa majengo wanaweza kweli kututhibitishia kuwa hizi bilioni kumi ndio halisia? Ukiangalia kwa ukaribu unapata shaka. Naamini kuna hela imezidi Ila kwa vile mkuu alishatamka hicho kiasi basi TBA wamelazimika kuendelea kukariri bilioni kumi.

  Jé wasimamizi wa mradi huo walikuwa hawalipwi? Bodi ya ukadiriaji majenzi ina standard zake katika kujenga Jengo lolote. Nina amini ipo siku tutapata uhalisia wa gharama hizo.

  Kuna athari kubwa ya kutokuwa wakweli katika mradi huo. Athari yake ni kuwa kila jengo litakalojengwa nchini kama litapita gharama hizo basi wataambiwa wameweka chá juu. Tuliona hili kule Simiyu. Rais alikataa Jengo lenye kukadiriwa hela nyingi. Akatoa mfano wa bilioni kumi katika mradi huu wa mabweni ya udsm. Wataalamu watakuwa na woga kuleta gharama halisi zá majengo kwa hofu ya kuambiwa wameweka chá juu.

  Tunahitaji kupata majengo haya kwa gharama nafuu lakini isiwe chini ya nafuu. Natoa wito wakadiriaji majenzi waje hapa kutupa standard zao zikoje kwa majengo kama haya. Wasiogope kusema ukweli.

  Flat 20 ina maana kila flat iligharimu shilingi milioni 500. Jé flat moja lenye floor 4 gharama yake ni milioni 500? Na hapo hapo wakajenga na uzio. Sitaki kufurahia tu kupata majengo haya lakini lazima gharama halisi zionekane.
   
 2. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #221
  Apr 18, 2017
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,912
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Wewe mwenyewe hujanipuuza ndio maana ukajibu
   
 3. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #222
  Apr 18, 2017
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,912
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Utaburuzwa sana. Kama kila rangi wewe kwako ni njano basi pole sana
   
 4. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #223
  Apr 18, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,583
  Trophy Points: 280
  Hizo flats inawezekana zikawa na bei mara tatu ya zilivyoainishwa,ila wanaogopa kutumbuliwa.Ukweli huo unatabia ya kufunuka siku moja utafunuka tu na tutajua mbichi na mbivu
   
 5. T

  Tino100 Senior Member

  #224
  Apr 18, 2017
  Joined: Mar 13, 2014
  Messages: 197
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Ni kweli ni nchi ya ujamaa hata pia katiba ya CCM inawaambia hivyo wanachama wao. Mimi binafsi naamin katika ujamaa asilimia nyingi sana, Japo ubepari ni ngumu kuukwepa. Kuhusu maswala ya ujenzi kungekua na kampuni moja kubwa ya Ujenzi ya taifa ili project zote kubwa zijengwe na sisi wenyewe. Kampuni kutoka nje ziwe ni kwa ajili ya miradi mikubwa sana ambayo hatuna uzoefu nayo, na zikija zifanye kazi mara moja na kamwe kazi ya namna hiyo isirudiwe tena kufanywa na kampuni na kampuni kutoka nje. Wao wakija tujifunze kutoka kwao. Ni aibu kubwa sana baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru lakini bado eti barabara na maghorofa yanajengwa na wachina. Inauma sana unakuta ma-engineer wanapigika lakin mchina kapanda ndege kutoka kwao anakuja eti kujenga barabara Tanzania. Tuombe Mungu tupate Kiongozi mkuu wa nchi mzuri, kila kitu kitanyooka. Tanzania sio ya kuwa hivi ilivyo sasa.
   
 6. edu88

  edu88 JF-Expert Member

  #225
  Apr 20, 2017
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 707
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 180
  Aisee hicho kitu kinauma sana. Nashangaa sana. Ilibidi TANROADS waweke vipengele vya kuwalazimisha foreign contractors kushirikiana na local contractors kwenye ujenzi wa barabara kubwa na kuwepo na mikakati madhubuti kabisa ya kuhakikisha local contractors wanajifunza kutoka kwa washirika wao. Tanzania yetu sote. Point yako ya shirika la kujenga miundombinu hasa ya umma ni nzuri sana, nadhani TBA ndo taasisi husika. Hawa majamaa wangejenga apartments nyingi katika sehemu strategic kama Kino, Sinza, Magomeni, Masaki, Oysterbay na downtown, wangesaidia sana kuleta unafuu kwa wafanyakazi maana hali ilivyo sasa, tunalipishwa bei za ajabu sana na hawa landlords mtaani. Mchechu namsifu kwa kufufua shirika ila aliegemea zaidi kutengeneza faida hivyo matokeo yake hakujali wenye kipato cha kati kweli kweli. Nyumba za milioni 120 na kuendelea, wangapi wanaweza nunua? hata kama wakinunua, je ni thamani yake kweli? Mbaya zaidi hawakuwekeza kwenye nyumba za kupanga kwa young professionals, bachelors au wale wenye small families. Yaani focus ipo kwenye 2-3 bedroom apartments ikiwa na high-end finishing na furniture ndani, who needs all that? Bachelor anahitaji one bedroom yake safi, simple finishing na minimum cost. Yaani uzembe serikali ya awamu iliyopita ya kushindwa kusimamia real estate ilileta mzigo mkubwa sana kwa watanzania. Mzigo ambao hadi sasa tunaubeba. Natumai Mheshimiwa Raisi atasikia kilio hiki na kuweka sera ya kujenga nyumba za bei nafuu za kupanga na kuuza. TBA anajenga, NHC anasimamia tu maana kama nafasi NHC alishapewa na alishaonyesha yeye bei yake ni ya kichaa.
   
 7. k

  kabombe JF-Expert Member

  #226
  Apr 20, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 16,972
  Likes Received: 9,779
  Trophy Points: 280
  Lete gharama zako badala ya kulia lia kama mtoto mdogo,huweleweki kama hutaki hostel zijengwe kwa kiasi kidogo au huamini kama hostel zinaweza kwa kiasi kidogo namana hiyo.
  Ukishazoea vya kunyonga,vya kuchinja lazima iwe tabu
   
 8. e

  erick lionel Member

  #227
  Apr 20, 2017
  Joined: Feb 14, 2017
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Ni uongo wa mchana kujenga hizo block kwa 10 bilion
   
 9. G

  Getstart JF-Expert Member

  #228
  Apr 20, 2017
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 6,078
  Likes Received: 658
  Trophy Points: 280
  Subiri CAG atatoa kweli mwaka kesho
   
 10. Rayban/p

  Rayban/p JF-Expert Member

  #229
  Apr 20, 2017
  Joined: Jun 30, 2015
  Messages: 1,111
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  CAG aibukee kwa ruhusa yanani? Hata akiibuka akakuta madudu atathubutu kusemea wap? Skuhizi nikufunika kombee sijui nani apite) usimtaftie matatizo cag wawatu
   
 11. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #230
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 5,168
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280

  Umeongea tena cha maana, hata vi studio studio bro, room moja kubwa ikijitosheleza kila kitu humo, pa kakiti, choo, kajiko na pakulala, sio lazima target yako kila wakati iwe wenye familia, sasa hawa wa studio wakipata family watahamia zile kubwa, and the cycle continues...
  Kuna jamaa mmoja nilitaja bei za mikopo humu, hasa za benki na NHC, ktk mahesabu yangu kwa kweli yalikaribia (mark-up 2.55)! That is too high kwa wale vijana wetu wa vyuo n.k.! Ila yeye alibisha kabisa na kudiriki kusema huwa nakopa kwa ma (Loan Sharks)! Wakati kiukweli wao hawapiga jumla ya hesabu yote ya deni siku ukidaiwa, kuna zile "small prints" watu wa mikopo hawapendagi kuwaelimisha watu, basi kumbe ndipo tunapoumia pale..
  Itabidi hii sekta ya real estate, mortgage na house-loans iangaliwe aise, the price is to high...
   
 12. dolevaby

  dolevaby JF-Expert Member

  #231
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 25, 2013
  Messages: 8,269
  Likes Received: 3,399
  Trophy Points: 280
  Usikariri hakuna majengo ya 10bl pale Pesa nyingi tu imetumika acheni kuamini porojo
   
 13. dolevaby

  dolevaby JF-Expert Member

  #232
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 25, 2013
  Messages: 8,269
  Likes Received: 3,399
  Trophy Points: 280
  ...shida yenu wabongo kuamini kila mnachoambiwa na watawala....
  ngejua kiasi gani Management ya TBA ilivyotaabika na ule mradi kwa ..kupeleka Bajeti ya siasa wala msingeandika haya mambo...
   
 14. dolevaby

  dolevaby JF-Expert Member

  #233
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 25, 2013
  Messages: 8,269
  Likes Received: 3,399
  Trophy Points: 280
  ...sio kufanyakazi bure tu na madeni juu....
  watu wanateremsha Povu humu...sababu wamezoea kumezeshwa Maneno na watawala
   
 15. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #234
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,401
  Likes Received: 1,940
  Trophy Points: 280
  Kazi imekamilika. Mgt ya TBA ilitaabika kuhakikisha kazi ziliainishwa kwenye mradi zinafanyk na mrdi unakamilika ndani ya muda na bajeti; ni sawa. Mental and physical fatigue (kutaabika) ndio kazi yenyewe na dhana ya kulipwa ujira. Wahenga walisema kazi si lelemama.
   
 16. k

  kiatu kipya JF-Expert Member

  #235
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 4, 2016
  Messages: 3,296
  Likes Received: 1,917
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo unataka kutoa watoto wetu kafara kwaajili ya mauchaguzi yenu ya 2020 ati hebu tuambie vizuri
   
 17. Omar Mzungwe

  Omar Mzungwe Senior Member

  #236
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 4, 2017
  Messages: 183
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mkuu ameshasema sasa mi nifanyeje nangoja zamu yangu ifike nilale katika flat la bilion 10
   
 18. u

  umulitho JF-Expert Member

  #237
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 18, 2012
  Messages: 418
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Mmezoea kuibiwa mananga nyie ndio maana mnahoji kuwa kwanini hamjaibiwa tena kwenye ujenzi wa hostel.!!!
   
 19. Itzmusacmb

  Itzmusacmb JF-Expert Member

  #238
  Apr 21, 2017
  Joined: Jun 22, 2016
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1,029
  Trophy Points: 280
  Kwahyo ni bilion 2 na hzo 8 wamekula c ndyo ?
  Mpumbavu ww
   
 20. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #239
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,876
  Likes Received: 1,024
  Trophy Points: 280
  Msubiri Lowasa atoe hiyo kafara.
   
 21. edu88

  edu88 JF-Expert Member

  #240
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 707
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 180
  Very very good point mkuu. Real estate sector iliachwa kujiendesha yenyewe utadhani serikali haipo, unacceptable kabisa. Yaani investors wengi wako kujenga nyumba za bei mbaya tu. Chunguza hata sasa. Zile za bei nafuu kwa kweli ni chache na most zinakuwa kwenye hali mbaya sana conditionally. Ndio maana serikali inabidi iiwezeshe TBA kujenga affordable houses mijini kwa ajili ya rika zote - mabachelor na wenye familia. Hii itasaidia sana kupooza bei za nyumba mitaani na kusaidia sana watumishi kuweza kuwa na mahali safi pakuishi bila kutoboa mifuko. Kingine, wabongo wengi elimu ya mikopo ni ndogo na hata ya matumizi pindi tupatapo pia ni issue hivyo tunaishia kupoteza.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...