Ni kweli Bia ni tamu kama inavyodaiwa?

Sisi wa k vant na MO ya bariiidi tunakomenti wapi?.mkuu haupigi bia aisee utofauti wako na pisi kali ni upi sasa
 
Nimeshachapa walevi wengi sana hapa mtaani hata uwe mbabe mi nakusubiri ukilewa tu unletee ungese nakuburuza hadharani
Bia inafanya watu wazims wawe wendawazim
 
Hebu nunua kamboga kazuuuuri mwambie shem akapike vizuriii ule na kaugali ka dona mixer na makopa !!! Kisha tafuta tubia kwako tuwili kisha washa sigara embass !!!! Acha aiseee maisha matamu bwana!!! Ila bia tamu!!!
NB ila uwe umemaliza ada za watot

Hebu nunua kamboga kazuuuuri mwambie shem akapike vizuriii ule na kaugali ka dona mixer na makopa !!! Kisha tafuta tubia kwako tuwili kisha washa sigara embass !!!! Acha aiseee maisha matamu bwana!!! Ila bia tamu!!!
NB ila uwe umemaliza ada za watoto
Makopa ni Nini?yaani juice embe ni kila kitu,nakushauri uache pombe na sigara jamaa yangu
 
Natumai muwakheli wa afya,,,,

Nijikite moja kwa moja kwenye mada husika, mimi sio mnywaji wa bia ila napenda kufahamu kupitia watumiaji wa kimiminika hicho.

Je ni kweli Bia ni tamu kama inavyodaiwa?

Nakumbuka siku moja nikiwa na rafiki zangu tulitoka mahali pa kupata vinywaji na chakula (Hotel), ilikuwa weekend wao wakaaagiza vinywaji aina ya serengeti light me nikaagiza juice ya embe kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo walizidi kuongeza vinjwaji wakati huo me bado nahangaika na juice yangu.

Nikajiuliza inaa maana aina hii ya kinywa haina kikomo mbona toka tumeanza wamesha maliza zaidi ya chupa 9 wakati me niko na kopo langu ni kuwa kuna radha tofauta lakini pia inawezaje kuishia tumboni bila tumbo kujaa alihali mtu akiagiza soda hawezi maliza hatachupa 3,!!

Na hii nimekuwa nikiiona sehemu nyingi za starehe kukuta meza imejaa vilevi kuliko juice au soda.

Sikuwa na majibu lakini pia sikuweza hata kuuliza kwani nilikua nimekaribishwa.
Kulitipia kibao hiki cha Mario kinachotikisa kwa sasa Bia tamu. Bila shaka watumiaji mpo hemu jimwayeni hapa tupate fahamu mengi zaidi juu ya utam wa bia....

Nawasilisha.
Neno 'tamu' ama 'mautamu' ni neno la kihisia zaidi kuliko uhalisia.

Hutumiwa na watu kuonesha kupenda ama kuridhishwa na kitu hicho alichotumia ama tendo fulani aliloridhishwa nalo.

Ninadhani hapa umeuliza kutaka kujua bia ni tamu kama embe dodo?

Jibu ni hapana, utamu unaotajwa hapo ni wa hisia maridhawa aipatayo mtumiaji na kuujua utamu wake hadi ujiingize kichwa kichwa na si kwa kusimuliwa, maana kila mmoja kabeba kinywa chake.

Yaani ni sawa na kusema penzi tamu ama desh desh tamu, je utamu huo unaweza kuuelewa kwa kusimuliwa?

Nadhani umeelewa kijana.
 
Back
Top Bottom