Ni kweli BARAA hili linainyemelea Tanzania?

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
5,044
11,690
Baraa hili ambalo tayari limeshapitia nchi kadhaa zinazoizunguka Tanzania baadhi ya watu wanasema sasa ni zamu ya Tanzania kukumbwa nalo.

Janga hili lilianzia miaka kadhaa huko nyuma kwa kukikumba chama cha UPC (Uganda people's congress) na kukisababishia kifo ambacho hakikutarajiwa. Baada ya kupumua kwa muda, baraa hili liliwavamia majirani wa Tanzania wanaoishi kuzini magharibi Zambia na huko likakiteketeza chama cha UNIP (United national independent party) Baada ya kusababisha mazara hayo huko Zambia na kusababisha baadhi ya viongozi wake kusota kwa muda mbele ya Nondo mpaka Mwl Nyerere akawaombea msamaha, baraa hilo lilihamia Kenya.

Hapo Kenya bila Huruma lilikifumuafumua chama cha KANU (Kenya African national Union) mpaka sasa wote mnajua mazishi yake yalivyofanyika.

Kwa sasa baadhi ya watabili wanasema Wazi kuwa ni Zamu ya Tanzania kukumbwa na zahama hiyo, na baadhi ( wengi wakiwa watanzania) wanatamka wazi kuwa mwaka 2015 baraa hilo haliepukiki Tanzania. Je utabili huu ni kweli utatimia baada ya Tanzania kuzungukwa tayari na baraa hili?
 
Ungeeleza na vyanzo vya majanga hayo ungesaidiwa lakini unaonekana kama unabashiri bashiri tu.
 
Ole wao watakaokutwa ndani ya nyumba hiyo (ccm) "baraa" litakapotua rasmi, wenzao weshajenga safina (Chadema)
wasije kutulaumu kana kwamba hatukuwaambia.
 
Ungeeleza na vyanzo vya majanga hayo ungesaidiwa lakini unaonekana kama unabashiri bashiri tu.

mkuu, hili baraa limewapata hawa kwa uamuzi wa wananchi tofauti na vyama vilivyopotea kwa nguvu za kijeshi kama Chama Cha Patric Lumumba kilikufa baada ya yeye kuuawa hiki ndicho chama kilicholeta Uhuru DRC , VYAMA VILIVYIJIFUTA baada ya mapinduzi ya kijeshi Rwanda na Burundi, Ila nilikuwa nimesahau chama kingine kilichokufa kilikuwa kinaongozwa na KAMUZU BANDA Rais wa maisha wa Malawi. Naye baada ya kufa nacho kikafa. Nchi zote zinazozunguka Tanzania Tayari Je sasa ni zamu ya nani?
 
bilaa hilo kuwakuta viongozi wa chadema wanao kula ruzuku wao na familia zao tena balaa hilo kuwakuta mapema sana
 
bilaa hilo kuwakuta viongozi wa chadema wanao kula ruzuku wao na familia zao tena balaa hilo kuwakuta mapema sana

Mkuu kwingine kote lilikopita limelenga vyama tawala, sijui kama safari hii litabadilisha mwelekeo.
 
BaRaa; utabiLi... BaRaa ni neno la kiarabu maanake TANGAZO/kupiga mbiu. utabiLi em tuekee hapa maana yake. vinginevyo hariri uzi wako uondoe huo ukakasi mkuu
 
BaRaa; utabiLi... BaRaa ni neno la kiarabu maanake TANGAZO/kupiga mbiu. utabiLi em tuekee hapa maana yake. vinginevyo hariri uzi wako uondoe huo ukakasi mkuu

Mkuu hili neno zuri ni baraa au majanga kwani angako lolote la chama lina athari kubwa kwa viongozi ,wanachama na mali za chama. Mambo hayo yanaweza kupelekea baadhi yao wajae ndani ya nondo imara na pia kufirisi baadhi ya watu na kutaifishwa baadhi ya mali za chama , viongozi na hata wanachama.Hili kama si baraa au majanga ni nini?
 
Ningeamini kama kungekua na chama M-Badala,, kwasasa TZ hakuna waliopo wote ni Wababishaji kama hao waliopo au afadhali au hao waliopo
 
Hebu usituchanganye hapa ukaharibu lugha yetu kajifunze L na R then na ww uanzishe mada yko
 
Ningeamini kama kungekua na chama M-Badala,, kwasasa TZ hakuna waliopo wote ni Wababishaji kama hao waliopo au afadhali au hao waliopo

mkuu kuna unafuu gani kwa waliopo !!!!??? kutufanya masikini zaidi!!!!?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom