Ni kweli baadhi ya vitambulisho vya NIDA havitambuliki?

kyarluta

Member
Oct 28, 2019
24
12
Ni muda umepita kidogo tangu niende kupokea mzigo wangu kwa huduma ya EMS pale Bukoba. Ofisa niliyemkuta zamu alishtuka alipoona kitambulisho changu cha NIDA.

Cha kwangu ni kati ya vitambulisho vya mwanzo kabisa ambavyo saini yake haionekani. Kwa mujibu wa ofisa huyo, ofisi yao ina waraka unaozuia kupokea vitambulisho hivyo ambavyo havina saini.

Swali langu ni je, ni kweli waraka huo upo ama ofisa aliteleza? Na kama ni kweli naomba kuelimishwa utaratibu unaotumika ili kuvibadili.
 
Naamini ofisa huyo yupo sahihi kwa kujibu wa ofisi yake,hayo mengine tusubiri wajuzi waje tupate elimu pamoja mkuu.
 
Haya Malalamiko yako nakushauri yaweke pending kwanza ndugu yangu kwani kwa sasa mkazo Wetu ni Uchaguzi Mkuu ujao na Kuiba mno Kura.
 
Back
Top Bottom