Ni kwasababu alikuwa na Akili sana, siyo Mnafiki, Msomaji mzuri, hakuogopa Kukosolewa, alijiamini na hakuwa Muongo kama wengine

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Mkapa alikuwa haogopi mijadala ya kimataifa- Rais
@SuluhuSamia

Chanzo: EastAfricaTV

Ninachojua tu GENTAMYCINE ni kwamba Siku zote ukiwa na Akili sana, Unajiamini, Msomi na Msomaji mzuri wa Vitabu, una 'Exposure' ya Kutosha, siyo Mnafiki wala Muoga, Mcha Mungu hasa na siyo Mchanganya Mungu na Majini ya Baharini, Mshamba na Mbinafsi hata Watu wa Kimataifa nao Watakuheshimu mno tu.

RIP sana Rais wangu Bora kabisa wa Pili kuwahi kutokea nchini Tanzania Hayati Benjamin William Mkapa 'Makuwa Genius' ukitanguliwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 'Zanaki Genius' na Kiukweli si tu huwa nawakumbuka bali nawalilia zaidi kwani mliifanya Tanzania iheshimike si tu Afrika bali hata duniani kote.
 
Mtu akifa anazidishiwa sifa..
Mkapa alifungia magazeti..
Bunge halikuwa live..
Mauaji ya mwembechai..
Kuuza NBC bei ya bure.
Kuwapa wabunge mishahara hii ya sasa
Imagine toka enzi ya Mkapa mishahara ya
Wabunge ndo hii hii na bado hadi leo tunalia ipunguzwe..

Kutokulipa Kodi kwa Rais Hadi wabunge Hadi ma DC...yote haya ya Mkapa.

Watoto wa juzi mmeanza tena kusifia watu kwa kupewa mazuri yao tu bila ku balance mapungufu Yao makubwa..ndo maana hata wengine mnataka wajengea masanamu
 
Mkapa alikua na ngeli nzuri .

Alifanya vizuri sana kwenye uchumi.

Ila sera ya ubinafsishaji haikwenda vizuri.

Viwanda vilichukuliwa na wahusika hawakuviendeleza.
Ukiniambia nisahihishe Tawala zote za Tanzania Kitaaluma haya ndiyo Matokeo yangu na naomba yaheshimiwe tafadhali....

Nyerere 95%

Mwinyi 40%

Mkapa 90%

Kikwete 25%

Magufuli 75%

Samia 5% mpaka sasa

Ukichukia jikaangie tu Sumu unywe Ufe.
 
Ni kweli unawashukuru pia kwa mchango wao kwa ndugu yako Kagame kuipigania Rwanda na kuituliza hadi leo!au sio??
Nyerere na Mkapa hadi Magufuli hawakuwa na Uadui na Chuki na Rwanda kama 'Wanafiki' wengine na ndiyo maana Rwanda ina Heshima Kubwa na ya Kutukuka kabisa kwa Nyerere na Mkapa.

Na hata Wanyarwanda ( ambao mnawachukia kila Uchao ) wameifanyia Makubwa sana Tanzania yenu hii ( hasa Kipindi cha Nyerere na Mkapa ) na hata kidogo Kipindi cha Magufuli, ila kutokana na Upofu wa Akili kwa baadhi yenu hamuwezi Kutambua.

Nawapenda hakuna mfano Nyerere, Mkapa na Magufuli na ningetamani na wengineo wakitaka Kuongoza vyema Tanzania na mpaka akina GENTAMYCINE tuwakubali basi wawaige hawa 'Geniuses' wangu Watatu tajwa hapa tafadhali.
 
Mtu akifa anazidishiwa sifa..
Mkapa alifungia magazeti..
Bunge halikuwa live..
Mauaji ya mwembechai...
Sikushangai kama ambavyo Mimi nimekuwa nikiambiwa nina Chuki Binafsi na Kikwete na Mimi leo kutokana na kila nikianzisha Uzi wa Kumsifia Mkapa ni lazima tu utakuja na huu Upuuzi wako dhidi yake.

Halafu acha Kuniita Mtoto wa Juzi na usinilazimishe nikaanza Kukuvunjia Heshima ya muda mrefu niliyokuwa nayo dhidi yako sawa? Na ni nani aliyekuambia kuwa ukiwa Mtoto wa Juzi au Jana huwezi kuyajua mambo, kuyachakata na kuyachambua vyema kuliko Wakongwe nyie wenye Akili za Kuku wa Mdondo?
 
Mkapa ndio aliweka ile sheria ya Rais hata akishinda kwa tofauti ya kura moja atangazwe mshindi, wakaondoa ushindi wa asilimia uliyokuwepo awali.

Ubinafsishaji pia ulianza enzi zake na kwa kiwango kikubwa haukwenda vizuri mpaka Nyerere akakasirika akasema mtakuja kubinafsisha hadi magereza.

Uzuri wake nakumbuka palikuwepo na ile sera ya ukweli na uwazi, hii ilitoa uhuru kwa watu kutoa maoni yao kwenye masuala mbalimbali hapakuwepo na kuwindana.
 
5℅ 😀😀😀 uhuru wa kuandika ni fursa ya wasomi pekee
Tena hata hiyo 5% nimempa basi tu na kwa ninavyoona katika Darubini yangu anavyoenda sasa huenda ikifika 2025 akaishia tu kuwa na 7% kwani kuna maeneo ya Msingi kama Matatu hivi ( ambayo sitoyataja ) naona anaupiga mwingi sana kwa Kuyakosea / Kukosea na yatamgharimu kuliko awazavyo au anavyodanganywa na 'Mswahili' Mmoja anayemuamini mno wakati 'Legacy' yake pekee aliyotuachia ni Uharibifu wa Maadili na Utaratibu wa Taifa hili la Tanzania.
 
Mkapa alikua na ngeli nzuri .

Alifanya vizuri sana kwenye uchumi.

Ila sera ya ubinafsishaji haikwenda vizuri.

Viwanda vilichukuliwa na wahusika hawakuviendeleza.
Alilijutia kosa hilo.

Mkapa alikuwa kiongozi mzuri, pamoja na unazi wake mwingi juu ya chama chake cha CCM.

Hakukibadilisha sana chama chake, lakini tayari uozo ndani ya chama ulikuwa umekwishaanza kuota mizizi. Hili hakujishughulisha sana nalo kuhakikisha kwamba anakiacha chama imara.
 
Alilijutia kosa hilo.

Mkapa alikuwa kiongozi mzuri, pamoja na unazi wake mwingi juu ya chama chake cha CCM.

Hakukibadilisha sana chama chake, lakini tayari uozo ndani ya chama ulikuwa umekwishaanza kuota mizizi. Hili hakujishughulisha sana nalo kuhakikisha kwamba anakiacha chama imara.
Huwa napenda mno Comments za Watu 'very Brainy' and 'analytical' kama Wewe Mkuu. Heko ( Kongole ) sana na ukiona Mtu anamchukia Hayati Rais Mstaafu Mkapa 'Makuwa Genius' jua Kichwani mwake kumejaa 'Tope Chafu' tupu tu.
 
Back
Top Bottom