Ni kwanini watanganyika wengi wanaoishi zanzibar wanakiunga mkono chama cha mapinduzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kwanini watanganyika wengi wanaoishi zanzibar wanakiunga mkono chama cha mapinduzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lengeri, Oct 7, 2010.

 1. Lengeri

  Lengeri Senior Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Source Mzalendo.net

  Mwanzoni wa kuingia vyama vingi Tanzania, kulikuwa na upotoshaji mkubwa unaliofanywa na Vyama vingine zidi ya CUF, ikiwemo kuambiwa kuwa:
  1.CUF Wakipata madaraka watarudisha Waarabu.
  2.Watarudisha mashamba ya Eka kwa wenyewe (Waarabu waliopokonywa).
  3. CUF nia yao kuvunja Muungano kwa hiyo Watanganyika wote watafukuzwa warudi kwao.
  Na mengineo mengi ambayo yaliyowafanya watu wasio na upeo mkubwa kuyaamini kuwa kweli wanaweza kufanya.
  Watanganyika wengi walioko Zanzibar wameamini na bado mpaka sasa wanaendelea kuamini kuwa CUF ikiingia madarakani wao watakua wako hatarini, na Zanzibar ni nchi nzuri kwao kuliko Tanganyika walikotoka, hapa wamefaidika na mengi kwa sababu wenyewe wamelala sana na kwa kuwa Wanzazibar wenyewe wanabaguana. Na kwa kuwa Wanzanzibar wenyewe hawaajiriwi kwenye makampuni mengi kwa sababu moja ama nyengine ikiwemo lile la uvivu pamoja ile tabia yao ya kila wakati kuaga kazini leo kafiwa na mjomba, kesho ana harusi ya mdogo wake na baada ya wiki anamsafirisha mama yake mdogo kwenda nje na mengineo mengi.
  Kutokana na sababu hizi basi Watanganyika wengi wamekuwa wakidanganywa na wao wakakubli kudanganyika na wakakubali kutumiwa kuingia katika jambo kuvunja katiba ya Zanziabar inayowakataza kushiriki katika kupiga kura kuwachagua Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na hata Rais Wa Zanzibar. Na hiyo basi ikawa inawaongezea wao ugomvi na Wanzanzibar kuanza kuwachukia kwa kuwa wamekuja Zanzibar wamemaliza ajira zote, na pia wanatuingilia katika chaguzi zetu kutuchagulia vioongozi tusiowataka na wasio na maslah na Zanzibar.
  Wengi unapozungumza au kulaumu Muungano khasara zake watauliza mbona Wazanzibar wako wengi kule Bara na hawabuguziwi?
  Jibu la suala hilo ni kwamba Wanzanzibar wengi walioko bara na si T/Bara peke yake ni Dunia nzima wao mara nyingi wanajishughulisha na lile walilolindea tu ambalo mara nyingi ni biashara. Wakiwa ugenini wanakuwa hawana na nafasi ya siasa na hata kama watajishughulisha na siasa ya ya huko T/bara basi wako sawa tu kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawaruhusu wao kuchagua popote pale wakiwa Zanzibar au wakiwa Tanganyika ni tafauti na ile katiba ya Zanzibar inawaokataza Watanganyika kujishughulisha na chaguzi za Wanzibari.
  Sasa sisi Wanzibar tunawaasa na kuomba Watanganyika wailoko Zanzibar sisi ni ndugu zenu na nyinyi ni ndugu zetu sote tumeshafanya maingiliano baina yetu. Lakini tunatatizo kubwa la kimaisha hapa kwetu kwa hiyo tunaomba muache kudanganywa kama watoto wadogo mukaitilia CCM kura zenu. CUF haina nia ya kumfukuza mtu hapa Cuf nia yeke ni kubainisha Haki ni ipi na batili ni ipi kuwatambua Wanzibar ni wepi na wageni ni wepi. Kama nilivyoeleza mwanzo kuwa Wanzibar wenyewe hawapendi kufanya kazi, neeme ikija tutapata sote na kwa kuwa Wanzibar ni kidogo hizo kazi zitakurudieni tena nyie nyie.
  Wapemba wamesema “RIZIKI HAIWANWI” KAMA NI HAKI YAKO UTAIPATA KWA KUWA MTOWA RIZIKI HANA UPENDELEO.
  Shime shime Watanganyika tuchague CUF ingie madarakani tufaidike sote.


  My take: Kweli huu Muungano kazi ipo
   
 2. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni zaidi ya kuwepo kazi
   
Loading...