Ni kwanini wanandoa hufikia uamuzi wa kuvunja ndoa?

Chrismoris

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
13,550
16,631
Amani iwe kwenu nyote Wanajopo wa jf mlio ndani ya ndoa na wale ambao katika sehemu ya maisha yao walipata wasaa wa kufunga ndoa na kuishi kwenye ndoa kabla ya kuachana, tunaomba mtumegee siri ya kambi.

Nahitaji kufahamu ni kwa nini wawili hawa walioamua kuoana,
1. wakaandaa kadi za michango ya harusi
2. wakafanya vikao vya kamati ya sherehe,
3. wakaandaa na kusambaza kadi za mwaliko wa sherehe,
4. wakapokea wadau ukumbini kwenda kuwasherekea na kuwa spoil kwa zawadi za kila aina, uamua kuachana bila kujali hatua walizopitia hadi kufikia hatua ya kuitwa wanandoa.

Maswali:
1. Ni kwanini wanandoa (baadhi) huamua kuachana baadae ?


"Why do people get married to divorce later?"

2. Nini kifanyike ili watu hawa wasifikie maamuzi ya kuachana?

Mshiriki maalumu ni "stone" mwenyewe.
 
Sijaoa lakini Naweza Kuchangia Busara yangu Japo Kidogo!

Maisha ya ndoa ni kama jua, Yanakuwa Matamu sana mwanzoni kama lile jua la asubuhi, ila itafika mahali haya maisha yanakuwa machungu na hayavumiliki kama jua la Mchana, Na hapa wengi huachana.. Wachache watakaovumilia ndio watakaopata ile ladha ya mwanzo yaani sawa na jua la Jioni, ule utamu wa Jua la asubuhi Hujirudia!

Ndugu Mtoa Post, Kama tunavyoachana katika Mahusiano ya kawaida kwa sababu ya Kuchokana na kwenye Maisha ya Ndoa vivyo hivyo!

Your Elder Bro!

Divine Santana
 
Ukiona watu wameachana jua hawakuendana, walilazimisha tu labda kwa kutofatiliana zaidi kujuana mazuri na mabaya/ndani na nje. Ila wengi sasa hivi hatuna uvumilivu wa kuvumiliana mapungufu. ukichanganya na dunia hii ya digitali ndio basi "waja leo waondoka leo"
 
Kila mtu anapooa na kuolewa anakuwa na sababu zake za msingi na matakwa yake ila kwa bahati mbaya wengi wanajificha kwenye kichaka cha upendo.

Anapokuwa ndani ya ndoa Yale malengo yake na matakwa yasipotimia ndipo mtihani unaanzia hapo. Watu wanavumilia ndoa endapo maslahi yake ya ndoa aliyoyakusudia toka mwanzo yanatimia .
 
Back
Top Bottom