Ni kwanini wanamageuzi wa kisiasa wengi dar wanatokea manzese,buguruni,mbagala na temeke.

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Kwa wale ambao tuliowahi kuishi dar tangu mwaka 1995 hadi leo hii ni lazima mtakubaliana nami tunapozungumza historia ya mageuzi ya kisiasa na harakati za kisiasa hapa dar bila kuzungumzia siasa na harakati za mageuzi hapa dar bila kuzungumzia maeneo ya manzese, buguruni, mbagala na temeke basi wewe utakuwa mgeni wa jiji.

Utafiti niliofanya katika maeneo haya ndio yanayoongoza kwa mijadala ya kisiasa na harakati za kisiasa na harakati za kisiasa lakini kuwa vijiwe vingi vya kisiasa mitaani.

2.Pili unapokuja katika swala la maandamano au unaposikia maandamano dar asilimia kubwa ya vijana wanaoshiriki wengi wanatokea buguruni, manzese, temeke na mbagala ndio maana hata wakati lowassa akipeleka fomu ya uraisi mwaka 2015 alianzia buguruni.

3.Tatu katika haya maeneo hata ukijaribu kutembea ni lazima katika kila hatua tano utakutana tawi la chama cha siasa, nakumbuka katika maeneo haya kuliwahi kujitokeza matawi kama kossovo pale manzese, osama lilikuwa pale midizini, ukanda wa gaza kule temeke, buguruni kulikuwa na tawi kama waasi, tawi kama palestina lilikuwaga buguruni haya matawi kuna kipindi kuna waziri aliyapinga sana.

Lakini swali langu jee ni kwanini ni wana mageuzi wengi wanatokea maeneo haya kuliko sehemu nyingine jee ni kweli kwa hapa dar wapinzani wa kweli wanatokea maeneo haya......, ni kwanini maeneo mengine unakuta harakati kama hizi hazipo kwa wingi kama buguruni, manzese, temeke na mbagala

Note: Yapo maeneo mengine sijayataja lakini haya ndo maeneo yanaongoza kwa harakati lakini haya niliyotaja ndo yanayoongoza kwa harakati .
 
Ndo maana Magufuli anataka watu wakafanye kazi, hivyo vijiwe vyenu ni sababu ya kutokufanya kazi.
 
Ndo maana Magufuli anataka watu wakafanye kazi, hivyo vijiwe vyenu ni sababu ya kutokufanya
kazi.
Sasa kama watu hawana ajira , hela ya kula inawapiga chenga , maisha magumu unafikiri bila kukaa vijiweni wataishijee
 
WANA WA NCHI YA TANZANIA NDIO MAENEO YAO HAYO, WENGI HAWAKUPATA BAHATI YA KUPITIA SHULE, WALIOPITIA SHULE HAWANA WATU WA KUWAANDIKIA VIMEMO HIVYO HAWANA KAZI, WENYE VIBARUA BASI MSHAHARA HAUTOSHI HATA NAULI YA BASI! MASHUJAA WA KWELI NA KWA KIASI KIKUBWA WATU WENYE HOFU YA MUNGU
 
Back
Top Bottom