Ni kwanini walimu wa kujitolea wananyanyaswa mno na walimu wajiriwa hasa kwenye shule za serikali?

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Japo sio shule zote ila shule nyingi hakuna mwalimu anayedhalauliwa na kunyanyasika kama mwalimu wa kujitolea sio na walimu hata wanafunzi pia baadhi ya wanafunzi wakijua mwalimu wa kujitolea huwa wanamdharau.

Tukianzia swala la malipo unakuta wazazi wanachanga buku buku kwa ajiri ya walimu wa kujitolea lakini lakini katika lile fungu mkuu wa shule,makamu wa shule, mkuu wa idara, katibu wa wazazi wanagawana zile hela alafu walimu wa kujitolea wanapewa elfu 30 au 20 kwa mwezi kama posho ya kazi.

Mwalimu wa kujitolea akiwa na program zake za kufundisha masomo ya ziada walimu waajiriwa wanamwingilia na kucuruga program zake Kisha wao kuichukua hiyo program.

Walimu waajiriwa wengine hufika hatua ya kuwaponda walimu wa kujitolea mbele ya wanafunzi kwamba wao sio lolote ndo maana wanafunzi wanawadharau hata akitaka kumwadhibu mwanafunzi anamgomea.

Haya mambo imefika hatua kumekuwa na makundi ya walimu wanajitolea na walimu waajiriwa Hawa waajiriwa wanajiona super classic kuliko wanajitolea.

Ni mengi ya kusema acha niishie hapa.
 
Mkuu, hiyo Ni hulka ya binadamu. Yaani wale walio na kitu cha ziada hujiona bora kuliko wengine na hutumia uziada huo kuwadhoofisha au kuwanyong'onyeza wale wasio nacho.

Mfano, Registered Engineer vs Graduate Engineer - utakuta yule aliyesajiliwa katika maongezi yake na watu wengine anamshusha sana yule ambaye hajasajiliwa, labda watu wakasifia kazi aliyefanya yule graduate, jamaa atachomekea,"lakini hajasajiliwa yule"

Mawakili vs wanasheria - hawa huwafanya vijakazi wale wasiosajiliwa. Huwaambiwa wawabebee briefcase zao nk. Na wakiwa mbele ya watu huwaita hao wengine 'vijana wao' nk, kitu ambacho hakina umaana wowote, kingeweza kuwa kati yao tu.

Lakini mara nyingi haya hufanyika ikiwa huyo asiye na sifa za ziada akiwa anajituma kazini na anaonesha weledi katika kazi kiasi cha webye sifa za ziada kuona kama ni tishio kwao. Komaa usiyumbishwe na maneno na usikate tamaa. Focus kwenye malengo yako
 
Japo sio shule zote ila shule nyingi hakuna mwalimu anayedhalauliwa na kunyanyasika kama mwalimu wa kujitolea sio na walimu hata wanafunzi pia baadhi ya wanafunzi wakijua mwalimu wa kujitolea huwa wanamdharau.

Tukianzia swala la malipo unakuta wazazi wanachanga buku buku kwa ajiri ya walimu wa kujitolea lakini lakini katika lile fungu mkuu wa shule,makamu wa shule, mkuu wa idara, katibu wa wazazi wanagawana zile hela alafu walimu wa kujitolea wanapewa elfu 30 au 20 kwa mwezi kama posho ya kazi.

Mwalimu wa kujitolea akiwa na program zake za kufundisha masomo ya ziada walimu waajiriwa wanamwingilia na kucuruga program zake Kisha wao kuichukua hiyo program.

Walimu waajiriwa wengine hufika hatua ya kuwaponda walimu wa kujitolea mbele ya wanafunzi kwamba wao sio lolote ndo maana wanafunzi wanawadharau hata akitaka kumwadhibu mwanafunzi anamgomea.

Haya mambo imefika hatua kumekuwa na makundi ya walimu wanajitolea na walimu waajiriwa Hawa waajiriwa wanajiona super classic kuliko wanajitolea.

Ni mengi ya kusema acha niishie hapa.
Mimi nafanya hio kazi walimu wananijali na wananitegemea japo wazazi wanalipa kiugumu lakini walimu wale wamenilea kama mtoto wao "sababu ni mdogo kwao" na mara zote kazi nyingi na maswali Mengi wanayoshindwa nawasaidia au mada wanazoshindwa kufundisha vizuri naclear na mwaka Jana shule imepandisha ufaulu wanatamani hata waniweke kwenye system ila inashindikana sababu sjasomea ualimu inategemea na kituo na hao walimu jishushe na ishi maisha Yako kumbuka upo kwenye kipindi Cha transition kudharauliwa ni kawaida tu katika utafutaji pambana we mkubwa we ni binadamu
 
Back
Top Bottom