Ni kwanini Viongozi wa sasa Barani Afrika hawapendi kukosolewa na ni wazuri sana kwa vitisho na visasi?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Hapa nchini Afrika ya Kati (CAR) yalipo Makazi yangu Kikazi (japo Tanzania huko ni Nyumbani) kuna Mauzauza mengi kutoka kwa Rais wa hapa.

Kwanza japo ni Katili na ana Chuki kwa Watesi (Critics) wake ila pia ana Sifa kubwa ya Uwoga na Uwoga wake zaidi unazidi katika ugonjwa huu wa Tauni uliopo huku kwa sasa.

Natamani mno huyu Rais Wetu hapa CAR na wengine waige tabia njema na nzuri za Rais wa kule Kwetu Nyumbani Tanzania Dk. Magufuli ambaye anapendwa na Watanzania wote, anawasaidia vyema Wagonjwa mfano wa Corona na anakubali Kukosolewa, hana Visasi wala Kashfa ya Kuhatarisha Maisha ya Mtu.

Natamani Rais wa Afrika nzima angekuwa Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli na si huyu wa hapa nilipo nchini CAR ambaye pia muda wowote anaenda Kuzima Mitandao ya Kijamii kwani hapendi Watu Watwiti, Waritwiti au Walaiki Michango (Mitazamo) ya Watu wenye Akili Kubwa kumzidi yeye.
 
“Magufuli kwanini hapendi kukosolewa na ni mzuri kwenye vitisho na visasi”

Mfano!! Tundu lissu , Nape, January etc

Tutaishi kwa uongo mpaka Lini!!
 
Nani amekwambia hawapendi kosolewa? namna inayotumika kuwakosoa ndo hawaipendi.

Hata baba nyumbani kuna namna akikosolewa huwa anarudi nyuma na kujitathimini.
 
Tamaduni za kiafrica sio sahihi kumkosoa mtu je wewe apo unaweza kumkosoa baba yako.au mama yako.waafrica ni makosa kumkosoa mkubwa wako ata akikosea ndo tamaduni.zetu...ndo maana viongozi waafrica wengi ukiwakosoa wanachukua maamuzi magumu.maana waafrica kukosoana sio jadi yetu....atujazoea.ayo.
 
Back
Top Bottom