NI KWANINI VIJANA WENGI SIKU HIZI NI OMBAOMBA

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
miaka ya zamani kuanzia ya 80 ukisikia omba omba asilimia 90 ni watanzania wasiojiweza na wenye ulemavuuu.

miaka ya karibuni tuhuma za kuomba omba zilikuwa upande wa kina dada lakini siku hizi mambo yamebadilika sio wanaume sio wanawake vijana wamekuwa omba omba......

kwa mfano vijana wengi wa kiume unakuta asilimia karibia 80 wanashinda vijiweni wakisubili apite mtu anaemfahamu akuombe hela either ya sigara, kula,bangi, kiroba na n.k.

sio huko tuu siku hizi hata ukienda bar kujipumzisha utashangaa kuna kijana flani flani kisa mnajuana atakupiga mzinga wa bia au hela umnunulie mbaya zaidi mwingine hajui mfukoni bajeti yako ni shillingi ngapi.

sio uko hata kwenye kumbi za starehe,mitaani, n.k hii tabia ya kuomba omba imekuwa kero sana halafu mbaya zaidi .

kuna kijana mwingine unamkuta ana nguvu za kufanya kazi lakini hataki kazi yeye muda mwingi kijiweni kuzungumza mpira, maisha ya watu akikuona tuu anakupiga mzinga.

sasa kuna mwingine unakutana nae hata ile aibu hana kila siku akikuona unatoka zako kwenye mishe mishe yeye kazi yake ni kutangaza shidaa umsaidiee yaani hata ile aibu ya kusema leo nimkaushie nisimpige kibomu lakini wapi kila akikaa kibomu.

najiuliza hivi haya maisha ni kwanini yapo hivi kila siku watu hawabadilikiii na wamekuwa omba omba tatizo hivi ni nini
 
Back
Top Bottom