Ni kwanini unajenga nyumba ya ghorofa?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Wazungu walijenga nyumba za ghorofa kutokana na uhaba wa ardhi kwao. Nimekutana na Wafrika Magharibi pia mawazo yao ni ya kujenga ma ghorofa. Nikipowauliza sababu waliniambia kwao ardhi ni ghali sana. Kupata kiwanja cha kujenga nyumba inakulazimu uwe na kuanzia milioni 20 kwa pesa ya Tanzania. Wanasema ukijenga ghorofa hukosi mpangaji na wewe unapata na sehemu yako ya kuishi kwa amani.

Wengine wanasema wanajenga ghorofa kuyaona matunda ya mafanikio yake kwa macho. Sasa ninajiuliza sisi ardhi tunayo kubwa sana. Mpaka sasa bei ya kiwanja ni wastaniwa milioni tano mijini. Ni kwanini unawaza kujenga ghorofa kama una wazo hilo au ni kwanini ulijenga ghorofa?

1609109999598.jpeg
 
Ili kutia heshima!
Kuna kijana kule Tanga alikua baharia. Alirudi na pesa yake na kununua nyumba ya udongo mtaani enzi hizo. Alisema ninakwenda tena nikirudi ninajenga ghorofa niwe nina wasanifu wanaokwenda chooni na makopo ya maji nikiwa chumbani kwangu.

Mauti yalimkuta kabla hajaanza kuwasanifu wanaokwenda chooni.
 
Aisee
 
Namnukuu binti nimeongea nae hapa sasa hivi:

"Wengine ni lifetime dream zetu tu. Hivyo yani. Unaamka unashuka ngazi toka chumbani kuja down stairs. "

"Halafu pia the idea ya kuseparate downstairs where the place greets every Tom, Dick and Harry, na upstairs ambapo ni more personal and private"
 
Kuna kijana kule Tanga alikua baharia. Alirudi na pesa yake na kununua nyumba ya udongo mtaani enzi hizo. Alisema ninakwenda tena nikirudi ninajenga ghorofa niwe nina wasanifu wanaokwenda chooni na makopo ya maji nikiwa chumbani kwangu.

Mauti yalimkuta kabla hajaanza kuwasanifu wanaokwenda chooni.
Tanga siyo sehemu ya kujidai kabsa, ndio maana imedumaa kimaendeleo
 
View ya bahari.

Mfano mzuri Pemba Mnazi saa hizi ni kama Mbweni mpya. Watu wenye beach Front wana ghorofa kwa hiyo ukisogea nyuma kidogo na ukajenga ghorofa moja unaiona bahari ingawa kiwanja siyo beach front.

Hata Salasala hivyohivyo.

Ukitoka balcony unaiona bahari, au ukiwa bedroom.
 
Back
Top Bottom