Ni kwanini tusiangalie tunapokwenda kuliko kuangalia tulipotoka?

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,002
2,000
Baada nyuzi nyingi jf tangu enzi za watu wanatumbuliwa majipu, vyeti feki hadi kufikia issue ya mchanga mpaka madini....

Ni mambo mengi yamezungumziwa humu JF hadi inafikia hatua watu wanasema baadhi ya viongozi wakamatwe, mara wafilisiwe wengine wafugwe na mengine mengi ....

Mimi naona ni kwanini tusiangalie mbele kuliko kuangalia ni wapi tulipojikwaa na wapi tulipokosea .

MPAKA TUNAVYOZUNGUMZA HIVI SASA KATIKA NCHINI YETU KUNA

1.Kuna vijana hawana ajira .

2.Maisha mtaani yamekuwa magumu watu hawana mbele wala nyuma katika maisha.

3.Njaa imekuwa kali mtaani

4.Watu wana taabika na maisha mpaka inafika hatua wengine wanajiua kwa ugumu wa maisha

5.Kuna vijana wapo nyumbani kwa kukosa ada ya kusoma chuo au shuleni.

6.Kuna vijana wadogo hawana baba na wala mama wanaishi katika mazingira magumu.

7.Huko ma hospitalini huduma mbovu kila kitu kigumuu tuu

Na mengine mengi hivi ni kwanini tusiangalie mbele ni jinsi gani tutaboresha maisha kuliko kuangalia tulipotokaa mimi sidhani hayo mambo mnayaongea yatasaidia.

Huu ni ushauri tuu kwa rais wangu.
 

toto zuli

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
257
500
Ulichozungumza uko sahihi kabisa unachokizungumza

Maisha saivi yamekuwa tight sana na usiombe uwe na majukumu
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,099
2,000
C programming
Ni makosa makubwa kutojifunza kutokana na makosa.

Huwezi kwenda mbele kama hujui umejikwaa wapi, ni likely utajikwaa tena na kudhani ni vema kuendelea na safari

Haya ya madini si jambo jipya. Tumefumba macho miaka mingi, kuendelea kufumba macho ni kutoa nafasi ya uharibifu. Wahusika wawekwe hadharani, mikataba iwekwe hadharani kisha tujifunze kutoka hapo ili twende mbele

Wenzetu nchi zilizoendelea, linapotokea tukio hawaendi mbele tu, wanatafuta maswali na majibu

Fani ya Engineer ina misem(kama sitjakosea) katika kutafuta majibu ' How,when,where, why and what'

Tujiulize kwa kauli hizo; Imetokeaje, lini, wapi, kwanini na nini kifanyike
 

MSELA WA MANZESE

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,603
2,000
Mkuu ni muhimu kuangalia ulipojikwaa kuliko kuangalia ulipoangukia, vinginevyo unaweza kujikwaa tena palepale.
Ni kweli ulichokizungumza mimi ndo maana mambo mengine ya kisiasa huwa sipendi kuyashabikia

Kwa sababu hao ninaowashabikia mwisho wa mwezi wanakula mshahaara na malupulupu kibao mimi naendelea kula msoto mtaani halafu nikiomba ajira niwe kama wao na ninambiwa nijiajiri ajira hakuna wakati sina mtaji
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,737
2,000
Kujitathmini ni muhimu, ulikuwa wapi, uko wapi na unataka kwenda wapi. Kwa kuangalia nyuma na kujifunza wapi ulifanya vizuri au ulikosea, uendako utaboredha yale mazuri na kutorudia makosa.
 

MSELA WA MANZESE

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,603
2,000
Kujitathmini ni muhimu, ulikuwa wapi, uko wapi na unataka kwenda wapi. Kwa kuangalia nyuma na kujifunza wapi ulifanya vizuri au ulikosea, uendako utaboredha yale mazuri na kutorudia makosa.
Mimi hapa nilipo hata sijielewi
Hali ya maisha imekuwa ngumu sana jamani hebu tusaidiane jinsi ya kupata michongo kuliko kutuma siasa
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,150
2,000
DAIMA KUJIPANGA KWA YAJAYO NI NJEMA ZAIDI,PAST HAS GONE TUNAJIPANGA KWA FUTURE IWE NJEMA
 

MSELA WA MANZESE

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,603
2,000
DAIMA KUJIPANGA KWA YAJAYO NI NJEMA ZAIDI,PAST HAS GONE TUNAJIPANGA KWA FUTURE IWE NJEMA
TUNAJIPANGA VIPI MKUU HEBU TUSAIDIANE KWA MAANA KAMA

1.KAMA KUTAFUTA AJIRA TUMESHATAFUTA HADI TUMECHOKA.

2.KAMA KUVUMILIA UGUMU WA MAISHA TUMESHAVUMILIA HADI TUMECHOKA.

3.KAMA KUJIAJIRI TUTAJIAJIRI VIPI WAKATI HATUNA MITAJI

4.KAMA KULALA NJAA TUMESHALALA NA NJAA HADI TUMECHOKA HEBU TUSAIDIEN

WEWE MWENZETU UNAFANYA NINI
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,150
2,000
TUNAJIPANGA VIPI MKUU HEBU TUSAIDIANE KWA MAANA KAMA

1.KAMA KUTAFUTA AJIRA TUMESHATAFUTA HADI TUMECHOKA.

2.KAMA KUVUMILIA UGUMU WA MAISHA TUMESHAVUMILIA HADI TUMECHOKA.

3.KAMA KUJIAJIRI TUTAJIAJIRI VIPI WAKATI HATUNA MITAJI

4.KAMA KULALA NJAA TUMESHALALA NA NJAA HADI TUMECHOKA HEBU TUSAIDIEN

WEWE MWENZETU UNAFANYA NINI
MKUU HAPA KILICHOPO NI TUJARIBU TUWEKEZE KATIKA KILIMO,TATIZO LINAKUWA MITAJI NA MASOKO HUSIKA.MKUU TUHAME NCHI AU
 

RReigns

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
16,334
2,000
Ukijikwaa ni muhimu uangalie ulipojikwaa urekebishe ndo uendelee na safari, vinginevyo kesho ukijikwaa tena pale pale utakua ni uzembe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom