Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Tume ya uchaguzi ya Tanzania (NEC) ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutangaza muda wa kuanza kampeni kwa vyama vyote vya sasa, kwa nafasi zote za zinazogombewa katika uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Tume hiyo ya uchaguzi bado haijatowa ratiba hiyo na hivyo kuonya kwa yeyote atakayefanya kampeni kabla ya muda, wa kutoka chama chochote cha siasa, ajue kuwa anavunja sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kutokana na hali hiyo TAKUKURU imepewa jukumu la kuwachukulia hatua watu wote watakaofanya kampeni kabla ya muda kutangazwa.
Tumejionea namna TAKUKURU walivyokuwa wakali kwa jambo hilo, walipomtia mbaroni, Ismail Aden Rage, aliyekuwa mbunge wa Tabora mjini, kwa tiketi ya CCM, ambaye inasemekana amekuwa katika kampeni, kabla Tume ya uchaguzi ya Taifa, haijapuliza kipenga, cha kuanza rasmi kampeni.
Hata hivyo wananchi tumeshuhudia, namna mwanachama wa Chadema, Dkt Mayrose Majige, akiutangazia Umma wa watanzania kuwa ana nia ya kugombea Urais, kwa tiketi ya CHADEMA , katika uchaguzi wa mwaka huu.
Swali ninalouliza je ni kwanini TAKUKURU hawamtii mbaroni Dkt Mayrose Majige kwa kuanza kampeni mapema kabla ya muda?
Vile vile ninafahamu pia kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, ni lazima mgombea yeyote adhaminiwe na apitishwe na chama chake, ndipo kimtangaze kuwa ni mgombea.
Je chama cha Chadema, ni lini kimemtangaza Dkt. Mayrose Majige kuwa kimempitisha kuwa mgombea wao kwa nafasi hiyo ya Urais?
Ni kwanini TAKUKURU itumike kisiasa katika kutimiza majukumu yake kwa kutumia "double standards" kwa kuelekezwa na mabosi wao watawala wa awamu ya tano wa CCM, ni nani wanapaswa kumkamata na kumhoji na nani hapaswi kukamatwa na kuhojiwa?
Ni dhahiri kuwa hao jamaa wa TAKUKURU wamepewa "maelekezo maalum" na mabosi wao watawala wa CCM kuwa wasithubutu kumkamata mwanamama huyo Dkt Mayrose Majige, kwa kuwa amepewa maelekezo maalum na CCM, atangaze nia ya kugombea nafasi hiyo ya Urais, kwa nia ya kuivuruga CHADEMA !
Kwa kuwa haiingii akilini ni kwa vipi wao TAKUKURU wafanye "double standard" kwa kosa la aina moja la kuvunja sheria ya uchaguzi, iliyotungwa na serikali yao katika kushughulikia wale wanaoanza kampeni mapema, kwa kumng'ang'ania mgombea wa CCM, Ismail Aden Rage na kumwacha huyu mwanamama, aliyetangaza hadharani kuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chadema
Tunachojua sisi wananchi ni kuwa huyo mwanamama Dkt Mayrose Majige, ni "mtu wao" hao CCM na ametangaza nia ya kugombea Urais, kwa maelekezo yao na ndiyo sababu TAKUKURU inashikwa na "kigugumizi"_cha kumtia mbaroni na kumhoji ni kwanini ameanza kampeni kabla ya muda