Ni kwanini sindano za chanjo zinatolewa kupitia begani na sio kwenye makalio?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,233
2,000
Wataalamu naombeni majibu,

Kwanini chanjo nyingi hata hii ya Covid 19 zinatolewa kwa kuchomwa begani na sio sehemu nyingine kama makalio au mapajani au kuingizwa kwenye mshipa wa damu moja kwa moja?

Nimeuliza hili swali baada ya raisi mtata wa Phillipines Rodrigo Duterte kutangaza kwamba yeye atachanjwa chanjo ya Covid 19 kwenye makalio na sio begani, huu uamuzi wake ulileta maoni mchanganyiko kutoka kwa wataalamu nguli wa chanjo kutoka nchi mbalimbali.

Na mimi nikaona niulize,Je haiwezekani kuchomwa chanjo sehemu nyingine za mwili?

Ahsante
 
Nature

Senior Member
Nov 5, 2014
177
1,000
Pia kuchoma begani inasaidia kuhamasisha watu wengi kukubali kuchanjwa katika mazingira rafiki bila hofu wala aibu.., bila kujali wala kuhofu kuhusu jinsia ya anayekuchoma chanjo....

Hebu fikiri chanjo ingekuwa inachomwa kwenye makalio akina Joe biden na Kamala Harris wangekubali kuchomwa hadharani mbele ya camera???
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
362
500
Suala ni eneo lenye misuli zaidi kuliko mafutamafuta. Mafuta yana blood supply kidogo, hivyo uwezo wa dawa kuchukuliwa toka eneo hilo ni mdogo.

Pia hutegemea kama dawa husika inayeyuka vizuri kwenye kimiminika cha majimaji au mafutamafuta. Hivyo, kuweka kwenye misuli kuwa eneo pendwa kulingana na asili ya dawa.
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,233
2,000
Pia kuchoma begani inasaidia kuhamasisha watu wengi kukubali kuchanjwa katika mazingira rafiki bila hofu wala aibu.., bila kujali wala kuhofu kuhusu jinsia ya anayekuchoma chanjo....

Hebu fikiri chanjo ingekuwa inachomwa kwenye makalio akina Joe biden na Kamala Harris wangekubali kuchomwa hadharani mbele ya camera???
Sawa hii inaweza kuwa sababu ya kijamii zaidi,tunahitaji na ya kitabibu
 
Tall Guy fam

JF-Expert Member
Jan 16, 2017
858
1,000
Utangulizi
Chanjo (antigen) nyingi huchomwa kwenye misuli kwa sababu kwenye misuli kuna immune cells ( Seli zinazohusika na kuulinda mwili dhidi ya vijidudu mfano virusi na bakteria). Baada ya immune cells kutambua hizi antigen inazichukua na kuzipeleka kwenye Lymph nodes, sehemu ambayo mwili huanza kutengeneza Antibody au kinga dhidi ya ugonjwa husika.

Kwa nini Chanjo inachomwa zaidi kwenye bega kuliko kwenye misuli mingine?
1. Kwenye kwapa kuna lymph nodes nyingi. Ili kuweza kuongeza ufanisi, chanjo inachomwa sehemu iliyo karibu ambayo ni bega.
2. Kwenye bega hakuna mafuta na pia kuna mzunguko mzuri wa damu ukilinganisha na kwenye sehemu nyingine mfano Matako hivyo kufanya chanjo inyonywe na kusafirishwa haraka na immune cells.
3. Size ya msuli. Watu wazima na watoto miaka 3 na kuendelea wanachomwa kwenye bega kwa sababu msuli tayari umeshajengeka. Wakati watoto wadogo chini ya miaka 3 huweza kuchomwa kwenye paja kwa sababu bega bado ni dogo.
4. Urahisi pamoja na staha. Kupandisha mkono wa shati juu ili uchome sindano ni rahisi zaidi kuliko kushusha chini suruali au gauni. Hii husaidia mtoa huduma wa jinsia moja kuweza kuhudumia jinsia zote na kwa uharaka zaidi.

Ziada
Lymph nodes zipo maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo around sehemu za siri. Sindano ya chanjo huchomwa kwenye paja kwa sababu kwenye makalio kwa kawaida kuna mafuta mengi.
Update: Kwenye mafuta (fat cells) hakuna mzunguko wa damu, hivyo endapo chanjo itachomwa eneo hilo haitaweza kufanya kazi vizuri.
Wataalamu naombeni majibu,
Kwanini chanjo nyingi hata hii ya Covid 19 zinatolewa kwa kuchomwa begani na sio sehemu nyingine kama makalio au mapajani au kuingizwa kwenye mshipa wa damu moja kwa moja?

Nimeuliza hili swali baada ya raisi mtata wa Phillipines Rodrigo Duterte kutangaza kwamba yeye atachanjwa chanjo ya Covid 19 kwenye makalio na sio begani,huu uamuzi wake ulileta maoni mchanganyiko kutoka kwa wataalamu nguli wa chanjo kutoka nchi mbalimbali.

Na mimi nikaona niulize,Je haiwezekani kuchomwa chanjo sehemu nyingine za mwili?

Ahsante
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,233
2,000
Utangulizi
Chanjo (antigen) nyingi huchomwa kwenye misuli kwa sababu kwenye misuli kuna immune cells ( Seli zinazohusika na kuulinda mwili dhidi ya vijidudu mfano virusi na bakteria). Baada ya immune cells kutambua hizi antigen inazichukua na kuzipeleka kwenye Lymph nodes, sehemu ambayo mwili huanza kutengeneza Antibody au kinga dhidi ya ugonjwa husika.

Kwa nini Chanjo inachomwa zaidi kwenye bega kuliko kwenye misuli mingine?
1. Kwenye kwapa kuna lymph nodes nyingi. Ili kuweza kuongeza ufanisi, chanjo inachomwa sehemu iliyo karibu na lymph nodes ambayo ni bega.
2. Kwenye bega hakuna mafuta na pia kuna mzunguko mzuri wa damu ukilinganisha na kwenye sehemu nyingine mfano Matako hivyo kufanya chanjo inyonywe na kusafirishwa haraka na immune cells.
3. Size ya msuli. Watu wazima na watoto miaka 3 na kuendelea wanachomwa kwenye bega kwa sababu msuli tayari umeshajengeka. Wakati watoto wadodo chini ya miaka 3 huweza kuchomwa kwenye paja kwa sababu bega bado ni dogo.
4. Urahisi pamoja na staha. Kupandisha mkono wa shati juu ili uchome sindano ni rahisi zaidi kuliko kushusha chini suruali au gauni. Hii husaidia mtoa huduma wa jinsia moja kuweza kuhudumia jinsia zote na kwa uharaka zaidi.

Ziada
Lymph nodes zipo maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo around sehemu za siri. Sindano ya chanjo huchomwa kwenye paja kwa sababu kwenye makalio kwa kawaida kuna mafuta mengi.
Asante mkuu maelezo yako mazuri yaliyoshiba vizuri,nimekuelewa

Kwahio pamoja na hivyo hata kwenye makalio unaweza kuchomwa tu kama huyo raisi alivyotaka? Au mpaka wafanye tathmini kujua kama chanjo itakuwa na ufanisi?
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,955
2,000
Mi nilikua nawaza, hivi hao waliopata chanjo ya corona wanatu postia picha zao mitandaoni kuonesha mabega yao kuwa encourage watu je wangedungwa za makalio wangetuoneshea nini?
 
Tall Guy fam

JF-Expert Member
Jan 16, 2017
858
1,000
Asante mkuu maelezo yako mazuri yaliyoshiba vizuri,nimekuelewa

Kwahio pamoja na hivyo hata kwenye makalio unaweza kuchomwa tu kama huyo raisi alivyotaka? Au mpaka wafanye tathmini kujua kama chanjo itakuwa na ufanisi?
Efficiency hua ni ndogo na pia kuna madhara madogo anaweza kupata kwenye makalio kama muwasho, kuvimba n.k. Sidhani kama watamchoma hapo labda akitumia ubabe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom