Ni kwanini Rais Magufuli kila anapomtumbua waziri wa mambo ya ndani, hataji sababu kuu kuwa ni kutokana na Kuzorota kwa Usalama wa Raia?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,137
Tulimsikia Rais Magufuli wakati anamtumbua waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, akitaja sababu kuu ni kutokana na mkataba wa Lugumi, ambao kwa madai yake ulikuwa na ufisadi mkubwa

Tumemsikia tena majuzi, wakati akimtumbua Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akitaja sababu kuu, ni kutokana na kusaini mkataba wa vifaa vya Jeshi la zimamoto, wenye thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja

Lakini ikumbukwe kuwa jukumu kubwa la Jeshi la Polisi nchini, ambalo ndiyo lipo chini ya wizara ya mambo ya ndani, ni kulinda raia na mali zao

Siyo siri tena kuwa kipindi tunachopitia, chini ya uingozi wa serikali ya awamu ya tano, matukio ya watu kupotea, watu kutekwa, kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, imekuwa ni kitu cha kawaida sana, kiasi cha kufanya utawala huu wa awamu ya tano, kijiwekea rekodi mpya nchini kwetu, kuwa ndiyo utawala ambao wananchi wake kuwa katika wasiwasi sana na usalama wao

Ndipo hapo ninapojiuliza inakuwaje kwa Rais Magufuli kutotaja kabisa suala la usalama wa raia, wakati anawatumbua mawaziri wake wa ndani, wakati anajua wazi kuwa suala la usalama wa raia ndilo jukumu namba moja ya Jeshi letu la Polisi nchini?

Ina maana kuwa Rais wetu hakerwi na vitendo hivyo vya kutekwa kwa wananchi wake na watu wasiojulikana?

Wananchi tukichukulia kuwa Rais wetu hachukulii kipaumbele kwa usalama wa raia wake, tutakuwa tunakosea kweli?
 
Rais aliyeshindwa kutoa hata pole kwa Mbunge aliyeshambuliwa katika Awamu yake kwenye makazi ya Viongozi wa Serikali kwa zaidi ya Risasi 36 kipaumbele kiwe Usalama wa Raia?

Jiwe ni muuaji .
 
Back
Top Bottom