Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Kwa nini Raisi John Pombe Magufuli kila anapotoa hotuba zake anapenda kutukemea na kutoa amri na vitisho?
Jana akiwa anaawapisha mawaziri alitoa kauli hii =
"Hata kasomeni tu leo magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."
John Pombe Magufuli.
[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Hata katika familia, kama nyumba haina amani, baba na mama wanagombana, watoto wanagombana, watoto wakimuona baba ghafula wanapishana milangoni kama panya Kwa hofu kwamba baba kafika, nyumbani chakula cha shida, dhiki imejaa, kila kinachoguswa kina lawama, kila kauli iinayotoka kwenye kinywa cha baba inaigawa nankuivuruga familia, kila kukicha baba anasema "Mimi ndiyo baba humu ndani" anamuambia Mama "Mimi ndiyo mume wako", na mambo kadha wa kadha.. Halafu baba huyo huyo wanapokuja wageni Aisha ndugu, marafiki, majirani, au wafanyakazi wenzake nyumbani, anawalazimisha familia kuonesha nyuso za Furaha, kucheka, kuwa wasafi na kupaka mafuta usoni ili kuficha dhiki, na kuwauliza watoto mbele ya wageni kwamba " mmeisha kula? Kuleni wanangu msikae na njaa, halafu nanii wahesabu wenzako mpo wangapi mkanunue soda" ilhali tangu Jana watoto walikula chakula Kwa masimango na masengenyo. Hakika Baba katika familia ya namna kama hii huisubiri hukumu na adhabu kutoka Kwa Mungu, maana hakuna wa kumuweza ndani ya familia isipokuwa yeye mwenyewe. Anakuwa amelaaniwa yeye na sio familia.
Rais Magufuli tulikuheshimu sana, japo nisiwe mnafiki, walikupenda sana wachache uliowafurahisha Kwa matendo yako. Unachotaka kukijenga kwenye nchi yetu ni kitu kibaya sana. Tunafahamu fika namna nchi yetu ilivyo na utawala mbovu usiozingatia sheria kiasi cha kufikia hatua bastola kushikwa hadharani na askri wako wanaovalia kiraia wakiwatishia viongozi, kufikia hatua wawakilishi wako (wakuu wa mikoa) kuvamia vituo vya habari usiku wa manane wakiambatana na askari wenye silaha za moto, hali ya uchumi ni mbaya, miundombinu yetu ni duni, gharamaza maisha zinawaelemea wananchi, migogoro ya ardhi inapelekea watu kuuana, mifugo kuuliwa na mazao kuharibiwa: halafu vyombo vya habari visiripoti habari hizo kwasababu tunataka tuonekane tupo salama nchini ilhali hatupo salama, kwamba tuonekane hakuna migogoro ya ardhi ilhali wananchi wanauana na kuharibu mifugo na mazao kwasababu hiyo, kwamba vyombo vya habari viripoti yanayokufurahisha na kukunufaisha wewe kisiasa na visiripoti ukweli Kwa maslahi ya Umma... Hapana, hauko sahihi kabisa, unatukosea watanzania na unatunyanyasa Kwa namna Moja au nyingine.. Itafikia mahali wananchi wanakuwa wewe utalazimisha vyombo vya habari viandike kuwa wananchi wapo salama wanaendelea na ujenzi wa taifa. Hebu ujitathimini wewe kabla hujavielekeza vyombo vya habari .